Watu waliokufa kipindi ambacho hata dini ya ukristo na uislam hazijaanzishwa wako wapi kama tunajiaminisha kwa kusema dini humfanya mtu kuona pepo?

fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Messages
538
Points
1,000
fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2018
538 1,000
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
 
nduza

nduza

Senior Member
Joined
Feb 7, 2019
Messages
150
Points
250
nduza

nduza

Senior Member
Joined Feb 7, 2019
150 250
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Me sisemi kitu
 
comred

comred

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Messages
1,734
Points
2,000
comred

comred

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2011
1,734 2,000
Wafia dini wengi ni mambumbumbu..
Akili zao wote wamemkabidhi mbumbumbu mmja wanaomwita mchungaji/nabii/mwalimu/nk

Wanabebana na Vitabu vya natural science (bible/quran)..kama mapambo hata kuelewa kilichomo ndani hawaelewi..nikuvisoma kama story book tuu nakurudia kilichoandikwa
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,498
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,498 2,000
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Ntajibu kwa muktadha wa Biblia ila Maalim Hammaz na salaniatz na chabuso watanisaidia kwa upande wa Quran.

Biblia ambao hao unaosema walileta dini ndio wanayotumia kama Rejea kutuaminisha dini yao, inaeleza kuwa Dunia nzima ilikuwa chini ya uangalizi wa Mungu (YHWH kiebrania).

Inaelezwa kuwa hao wanadamu wakiongozwa na Adam walimsaliti kwa kumsikiliza Hasimu wake mkubwa yaani shetani hivyo kama adhabu akawatimua kutoka katika himaya yake na akakata mahusiano nao.

So ikawa hivo anachagua mtu mmoja mmoja wa kujaribu kuanza naye upya ufalme wake hapa duniani... Ila nao Wanasaliti. Ikaendelea hivyo mpaka kwa Abraham akamchagua yeye na kizazi chake yaani wayahudi.... Nao wakasaliti.

Baada ya huu usaliti wa wayahudi wa kugeukia miungu wengine kupitia John 1:12 aliamua kuwageukia dunia nzima sasa bila kujali kabila au rangi.... Ndio maana injili (Hiyo dini ya Mungu YHWH) Ikahubiriwa dunia nzima kutokea wakati huo hadi ikawafikia waafrika ambao nao walikua na miungu yao hapo kabla.

Hivyo basi kwa muktadha huu dunia nzima ilikuwa na chance ya kuwa na dini ya Mungu mmoja ila kwa kuwa shetani aliwadanganya DUNIA NZIMA rejea Ufunuo 12:9 na 18:2 basi ndio ikawaponza na vizazi vyao. Kama ambavyo maamuzi mabovu ya viongozi wetu wa awamu ya kwanza ndio yametufanya tuwe maskini leo basi hao waliokufa kabla ya Mungu kuamua kugeukia mataifa yote tena na sio wayahudi kama zamani; nao watahukumiwa kwa sababu ya maamuzi mabovu ya mababu zao kumsaliti Mungu YHWH wa Biblia.

NB: Dini hazikuja baadae sana zilikuwepo miaka na miaka ila sema dini za Abrahamic/Mashariki ya kati (Islam/Jewish/Christianity) ndio zimekuja Afrika baaadae sana ila haimaanishi hazikuwepo huko nyuma kipindi tunatambika. Kama na sisi tungeamua kusambaza dini zetu huko ulaya na uarabuni leo hii penginepo ng'wanamalundi angekuwa nabii wao wanamwabudu.
 
Bulaya001

Bulaya001

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2018
Messages
3,923
Points
2,000
Bulaya001

Bulaya001

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2018
3,923 2,000

hapo umezungumza kwa majibu wa biblia ambayo tuchukulie ni kama theory.. sasa tuje kwenye uhalisia hivi Mungu atuchome kwa moto ili afaidike nini zaidi?
 
kawoli

kawoli

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Messages
4,004
Points
2,000
kawoli

kawoli

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2014
4,004 2,000
Kabla ya ustaarabu na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano haijakuwa, hapa namaanisha kusoma na kuandika pamoja na usafiri wa nchi kavu na majini, Mungu aliweka wateule wake kwenye kila jamii ya mwanadamu ili wawaongoze binadamu hao kulingana na vile Mungu anaona inafaa.
Ndio maana kila jamii ina kitu inachoamini ni Mungu. Mungu hajawahi kumuhukumu mtu kulingana na dini isipokuwa yale aliyomuagiza binadamu ayafanye.
 
fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Messages
538
Points
1,000
fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2018
538 1,000
Kabla ya ustaarabu na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano haijakuwa, hapa namaanisha kusoma na kuandika pamoja na usafiri wa nchi kavu na majini, Mungu aliweka wateule wake kwenye kila jamii ya mwanadamu ili wawaongoze binadamu hao kulingana na vile Mungu anaona inafaa.
Ndio maana kila jamii ina kitu inachoamini ni Mungu. Mungu hajawahi kumuhukumu mtu kulingana na dini isipokuwa yale aliyomuagiza binadamu ayafanye.
kwa hiyo kumbe ni matendo mema yamfanyayo mtu kwenda mbinguni na si dini...sasa kwa nini watu warumbane kisa dini?
 
kawoli

kawoli

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Messages
4,004
Points
2,000
kawoli

kawoli

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2014
4,004 2,000
Mungu hana dini. Wala mitume wake aliowaweka yeye hawakuhubiri dini. Dini zimekuja badae Sana.
 
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Messages
3,177
Points
2,000
M

Magobe T

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2008
3,177 2,000
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Mimi naelewa hivi: Imani ni uhusiano wa ndani (inner relationship) kati ya Mungu na mwanadamu na dini ni 'external expression' (mwonekano wa imani mtu kwa nje). Kwa maneno mengine, uhusiano wa mtu na Mungu (imani) unaonekana kwa nje kupitia dini. Wanadamu wote duniani (hata kwa nchi kama Korea Kaskazini na China) wana imani na dini. Yaani kila jamii ya watu wana idea of God kwa namna yoyote ile na ndiyo maana katika jamii zote za wanadamu yale mambo wanayoyaona ni mema ni mema hata kwa jamii nyingine na yale wanayoyaona ni mabaya ni mabaya pia kwa jamii nyingine. Hii inaonyesha universality ya Amri 10 za Mungu - kila jamii ya wanadamu wanazo na wanaweza kuzi'express' kwa namna tofauti, lakini in essence ni zilezile. Hivyo, wokovu ni kwa wanadamu wote - wale 'watakaoamini wataokoka' na 'wasioamini wataangamia'.
 
Forum statistics

Threads 1,304,151
Members 501,282
Posts 31,504,691
Top