Ekam
Member
- May 26, 2018
- 67
- 42
Habari wana jamvi? Poleni na mihangaiko ya kimaisha.
Kwanza kabisa nianze kwa kusema nimekuwa na hili swali fikirishi sana kuhusu dini hizi mbili Uislam na Ukristo na mpaka sasa sijapata majibu yenye kujitosheleza kabisa.
1. Kwa nini hizi dini mbili zimekuja kutoka nje ya bara la Afrika?
2. Kwa nini hakuna mtume mweusi? Mitume yote utasikia na kusoma kwenye vitabu hivyo yaani Quran na Biblia kuwa walikuwa waarabu au wayahudi nk lakini hakuwa mtu mweusi
3. Kwa nini maandiko ya dini hizi yanataka waumini wake waamini kuwa race hizo zilizopokea dini hizo ni bora kuliko race zingine? ?
4. Kwa sisi tunaoamini katika dini hizi mbili, tunaamini tukifa tunaenda kukutana na mungu alietuumba nk kila dini ina mafundisho yake kuhusu maisha baada ya kufa. Swali langu liko hapa Je ni lugha ipi itakayotumika huko mbinguni??? Mfano waislam tunaamini kuna maisha ya kaburini na kuna maisha ya kisimamo cha hukumu yaani kiyama ( mtanisahibisha kama nimekosea) na pia kuna maisha imma ya motoni au peponi je ni lugha gani itakayotumika katika maisha hayo baada ya kufa.??
Ni maswali ninayojiuliza pasipo kupata jibu. Kwa kuwa hili ni jukwaa la wajuzi wa mambo mengi naomba kupata majibu ya maswali yangu kwa anaefahamu.
Ahsanteni.