Watu waliokufa kipindi ambacho hata dini ya ukristo na uislam hazijaanzishwa wako wapi kama tunajiaminisha kwa kusema dini humfanya mtu kuona pepo?

fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Messages
538
Points
1,000
fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2018
538 1,000
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
 
kama kazz

kama kazz

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2015
Messages
1,053
Points
1,500
kama kazz

kama kazz

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2015
1,053 1,500
hapo umezungumza kwa majibu wa biblia ambayo tuchukulie ni kama theory.. sasa tuje kwenye uhalisia hivi Mungu atuchome kwa moto ili afaidike nini zaidi?
Na tena mungu alivyo mweledi na mkaribu kwa unyeyekevu wake na Huruma zile za kutufunza kusamehe saba mara sabini ..Hawezi kutuchoma wala nini
 
fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Messages
538
Points
1,000
fierceman

fierceman

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2018
538 1,000
Kama ndio maswali yako kabla hujauliza jibu hili fierceman
Ikiwa tayari watu wapo mbinguni Yesu atakuja kufanya nini?. Elewa kwamba wapo wachache waliochukuliaa kama mfano kuwawakilisha watakao kutwa wako hai na wengine walifuguliwa kuwakilisha UFUFUO WA PILI.
Kuhusu eliya na Henoko hawa wanawawakilisha wale ambao hawataonja mauti kabisa Kristo atakapo kuja mara ya pili 1Thesalonike 3:14-18
Lakini wale waliofufuka na Kristo baada ya siku tatu hawa wanawakilisha wafu waliopo makabirini wanaosubiri kristo mara ya pili.

Kuna dogma nyingi sana zinadanganya haswa ibada ya wafu kwamba wafu wanateseka au waombewe au wapo pagatori na mengine mwengi ya kimizimu. Ukitaka ufahamu soma andiko hili Ayubu 22:21
sawa atakuja kuhukumu ulimwengu lakini si kwa wote kwa maana kuwa kama tayari umeshatangulia kusema kuwa kuna wawakirishi wa wafu na walio hai tayari wako mbinguni basi kumbe ni dhairi kuna ambao hukumu haitawahusu
 
lutemi

lutemi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Messages
1,203
Points
1,500
lutemi

lutemi

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2013
1,203 1,500
sawa atakuja kuhukumu ulimwengu lakini si kwa wote kwa maana kuwa kama tayari umeshatangulia kusema kuwa kuna wawakirishi wa wafu na walio hai tayari wako mbinguni basi kumbe ni dhairi kuna ambao hukumu haitawahusu
Brother fierceman of cause yes lakini hii haitupi mandating kwamba wapo watu motoni au wapo watu pagatori au wapo watu wameshahukumiwa tayari.
Hukumu bado
Na ujio wa kristo the big triumphs inakuja.
 
corasco

corasco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2016
Messages
3,042
Points
2,000
corasco

corasco

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2016
3,042 2,000
hakuna cha motoni wala hakuna cha peponi

#ila kuna kaburi, jeneza na mchwa..

hivi ulishawahi kuwaza kuwa je, Mungu ukituchoma motoni yeye atafaidika nini haswa?
Ha ha ha jamani
 
magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
800
Points
1,000
magagafu

magagafu

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
800 1,000
Mbona jibu lipo katika biblia! Hao watu watahukumiwa kwa dhamiri zao, mfano mdogo binadamu tunaua wanyama mioyoni mwetu hatujishuhudii Kama tumefanya kosa ila kuua binadamu mwenzio uwa tunajishuhudia ni kosa Sasa dhamiri yetu kule kutusuta ndio kosa lenyewe,kwaio kabla ya dini kuja dhamiri zetu ndio hukumu zetu
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,746
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,746 2,000
Hekaya za kipuuzi za wazungu na waarabu zinawapotezea wajinga fedha na muda wa kufanya mambo mengine
 
rajabkisauti

rajabkisauti

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Messages
490
Points
250
rajabkisauti

rajabkisauti

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2015
490 250
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Ha ya maswali naona yanajirudiarudia..
mtua hapati adhabu kama ujumbe haukumfikia.
 
salaniatz

salaniatz

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Messages
2,511
Points
2,000
salaniatz

salaniatz

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2014
2,511 2,000
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Dini (kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka: ad-din) inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji.Dini ni mfumo mzima wa uendeshaji maisha ya binadamu.Kwa hayo ni ilikuwepo tangu Adamu.Kwa hayo hakuna mtu asiye na dini (wapagani) bali yale anayoyaamini na kuyatenda na kuwatendea wengine ndio dini yake aliyoamua kuifuata kwa mafundisho ya akili yake yenye ukomo wa fikra kwa kufuata matamanio ya nafsi yake.Kuhusu uislamu hii ni dini iliyokuwepo tangu Adamu wala sio imeanzia Uarabuni bali Mtume Muhammad na mitume wengine tangu Adamu wametumwa (walikuwepo) ili kufikisha kwa watu zama hadi zama.Hii inatoka na kule sifa kubwa ya mwanadamu ni kusahau na pia kuingiliwa na fitna za shetani kuwafanya binadam kuisahau miongozo (lengo la kuumbwa binadamu).Kwa kule kusahau kwao na shetani kuwapeleka katika mahasi na kufuru baada ya miaka mingi kupita karne na karne basi watu huishilizia katika maangamivu ikiwa ni pamoja na kuabudia aliyekuwa mwenyezi mungu.Mitume na manabii wote tangu Adamu hadi Muhammad walihubiri imani juu ya mungu mmoja (naongelea mitume waliothibitishwa na mungu katika vitabu.

Maswali matatu ya msingi ni haya.
1.Je nikweli uislamu ni dini tangu Adamu (hajaianzisha Muhammad)?
2.Je vipi hukumu juu ya wale ambao hawajafikishiwa ujumbe wa uislamu?
3.Je nini hukumu ya wale waliofikishiwa ujumbe wa waislamu na wakaupinga?

Nitarudi baada ya muda kuyajibu hayo
1.Je nikweli uislamu ni dini tangu Adamu (hajaianzisha Muhammad)?
Kwanza tujue nini maana ya uislamu au kuwa muislamu
Maana ya Uislamu ni kujisalimisha kwa Allaah kwa Tawhiyd (kumpwekesha), kunyenyekea Kwake kwa utiifu na kujitakasa na Shirki na kujitenga mbali na washirikina. Huu ndio Uislamu katika kila zama na mahala na ndio Uislamu ambao Allaah Amewatuma kwao Mitume wote. Kila Mtume na wafuasi wao walikuwa juu ya Uislamu. Kila yule ambaye alijisalimisha kwa Allaah na akamtii na akatendea kazi Shari´ah Yake katika ule wakati wake, basi huyo ni “Muislamu”. Hali iliendelea kuwa namna hii mpaka pale Alipotumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikawa “Uislamu” ni yale aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka hapo Qiyaamah kitaposimama.
Historia ya dini ya kiislamu haikuanza na Mtume Muhammad (SAW) kama wanavyofikiria watu wengi bali imeanza tangu alipoletwa Nabii wa kwanza ulimwenguni, ambaye kwa mujibu wa Waislamu ni Nabii Adam alipoteremshwa ulimwenguni na kupewa mwongozo na Mwenyezi Mungu wa namna gani kuishi hapa duniani kwa njia nzuri ya wema na hisani kwa kushikamana na mafunzo yake Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake.

Masimulizi ya historia hii ya Uislamu yameelezwa katika vitabu vitakatifu vya Mitume mbali mbali waliokuja duniani na kadhalika katika Qurani Tukufu. Umma mbali mbali zilizopita huko nyuma zimetajwa katika Qurani na kuelezwa namna gani zilivyoangamizwa kwa kutokubali ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuwakataa Mitume yake nao wakaletewa adhabu kali ya upepo au mvua au mafuriko na kadhalika.
Inasemekana katika historia ya Uislamu kuwa Mwenyezi Mungu alileta Mitume na Manabii kiasi cha 124,000 kwa ajili ya kuwaongoza binadamu kutokana na giza la ujinga na ujahili na utumwa wa kuabudu miungu mingi kuwatia kwenye nuru na mwangaza wa elimu na maarifa na ujuzi wa kumjua Mwenyezi Mungu wao aliyewaumba na kuwafanya wawakilishi wake hapa duniani. Mitume hawa na Manabii waliletwa na Mola wao kuwafahamisha wanadamu ukweli na haki iko wapi na wengine katika wao wakapewa vitabu ili wawaongoze wenziwao katika wanadamu kuwaelekeza kwenye njia ya haki.
Visa vya Mitume na Manabii hawa vinatueleza mengi kuhusu hawa wajumbe watukufu wa Mwenyezi Mungu na kuwa wote walitumwa na Mola wao kutangaza Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye hana mshirika na pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki asishirikishwe na chochote au yeyote katika viumbe vyake wakiwa ni binadamu wenziwao au mizimu au majini au wanyama au vyenginevyo katika viumbe vyake.

Tupate rejea za vitabu juu uislamu tangu ulikuwepo tangu Adamu
Quran
2:132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.
3:52. Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu.
3:67. Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.
4:125. Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani.
5:44. Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.
6:161. Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
7:126. Nawe hukuudhika nasi ila kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola Mlezi wetu zilipo tujia. Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. (maneno haya waliyasema watu zama za firauni baada ya kufikiwa na ujumbe wa Musa)
10:72. Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu. (maneno ya Nuhu kwa watu wake)
10:84. Na Musa alisema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu.
12:101. Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa utawala, na umenifunza tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao mema.(maneno ya Yusuph huko Misri)
22:78. Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.
27:42. Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu.
42:13. Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.
51:36. Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!(wanayasema haya wale nalaika waliotumwa sodoma na gomora kumwambia Ibrahim)
*2:183.“Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga (Swawm) kama walivyofaradhishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.”

Biblia
Siwezi kukwambia utumie biblia ipi au toleo gani bali nakushauri toleo la zamani lina ahueni katika kubainisha haya hasa ile kubwa yenye ramani na misamiati nyuma.
Neno Uislamu/Muslim katika lugha ya kiarabu linamaanisha kunyenyekea kuwa mnyeyekevu hivyo mtu anaposemwa yeye ni mnyenyekevu maana yake mtu huyo ni muislamu ("Muslim" is an Arabic word meaning "submitter" to God).Islam is derived from the Arabic root "Salema": peace, purity, submission and obedience.
Wanyenyekevu(waislamu) walikuwepo tangu Adamu
*Hesabu 12:3 (Mose alikuwa mtu mnyenyekevu kuliko watu wengine wote waliokuwa duniani.)
*Mhubiri 10:4 Mtawala akikuwakia hasira, usijiuzulu; makosa makubwa huweza kufutwa ukiwa mnyenyekevu.
*Methali 15:33 Kumcha Mwenyezi-Mungu ni shule ya hekima; kabla ya kuheshimika ni lazima kuwa mnyenyekevu.
*Methali 16:19 Afadhali kuwa mnyenyekevu na kuwa maskini, kuliko kugawana nyara na wenye kiburi.
*Methali 29:23 Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe, lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima.
*Luka 1:48 Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu. Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
*Mathayo 11:29 Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu.
*Isaya 66:2 Mimi mwenyewe nilivifanya vitu hivi vyote, na hivi vyote ni mali yangu. Lakini ninachojali mimi ni mtu mnyenyekevu na mwenye majuto, mtu anayetetemeka asikiapo neno langu.

Nitaweka mambo na matendo yaliyobainishwa katika biblia ambayo hayo ni katika dalili za uislamu kuwepo zama kabla ya Muhammad (sw).
Walisujudu(pajila uso chini),Kurukuu (kuinama),Takbiratul ihram (Kuinua mikono juu)
Waislamu Kufanya Harakati Fulani Katika Maombi. Harakati Za Maombi Mbalimbali Katika Biblia
*Kutoka kwa Yesu: “Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali:” (Biblia, Mathayo 26:39)
*Kutoka kwa Musa: “Kisha Musa akainama mbio kuelekea chini na kusali” (Kutoka 34:8 Biblia)
*Kutoka kwa Musa na Haruni: “Musa na Haruni wakaenda kutoka katika Kanisa mbele ya mlango wa hema na wakapiga nyuso zao chini” (Biblia, kitabu cha Hesabu 20:06)
*Kutoka kwa Ibrahimu: “Kisha Ibrahimu akaanguka chini kwenye uso wake ...” (Biblia, Mwanzo 17:03)
*Kutoka kwa Yoshua: “Kisha Yoshua akaanguka chini kwenye ardhi juu ya uso wake na akainama ...” (Yoshua 5:14 Biblia)
*Kutoka kwa Ezra na watu wake: “Na wakapiga magoti wakamwabudu Bwana kwa uso kwenye ardhi “ (Nehemia 8:06 Biblia)
*“Popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila hasira wala ubishi” (Biblia 1 Timotheo 2:08)
*“Eliya akainama chini ya ardhi na akainamisha uso wake kati ya magoti yake” (Ya kwanza Wafalme 18:42 Biblia)
*“Na Bwana akasema na Musa, akamwambia:” Nenda mbali na mkutano huu, nami baada ya muda nitawaangamiza “. Kisha wakapiga magoti juu ya nyuso zao. “(Biblia ya nne Musa 16:44-45)

Salamu yakiimani
Waislamu Husalimiana Kwa Kusema “Assalamu ’Alaykum”, Maana Yake: “Amani Iwe Juu Yenu(kwenu,yako)

Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu ziliniwasilia. Kisha akawatolea Simeoni. (MWA. 43:19-34)
*Lakini Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Amani iwe nawe! Usiogope, hutakufa.”(Waamuzi 6:23)
*Huyo mzee akamwambia, “Amani iwe nanyi! Nitawapa mahitaji yote. Ila msilale huku uwanjani.”(Waamuzi 19:20)
*Mtamwambia kwamba Daudi anakusalimu hivi: ‘Amani iwe kwako, kwa jamaa yako na yote uliyo nayo.(1 Samueli 25:6)
*Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza wasalimuni hivi: ‘Amani iwe katika nyumba hii!’(Luka 10:5)
*Walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia “Amani iwe nanyi.”(Luka 24:36)
*Hapo Roho akamjia Abishai, mkuu wa hao watu thelathini, naye akasema, “Sisi tu watu wako, ee Daudi, tuko upande wako, ee mwana wa Yese! Amani, amani iwe kwako, na amani iwe kwa yeyote akusaidiaye! Maana akusaidiaye ndiye Mungu wako.” Ndipo Daudi akawapokea na kuwafanya maofisa katika jeshi lake.
*“Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake kwa salamu ya amani” (Biblia Mathayo 10:12)


Waislamu Mara Nyingi Hutumia Neno - “Inshaa- Allaah” Ambalo Maana Yake Ni - “Mungu Akipenda (Mungu akitujalia)” - Maneno Haya Pia Tunapata Katika Biblia
*Hilo tutafanya, Mungu akipenda.(Waebrania 6:3)
*Bali alipokuwa anaondoka, alisema, “Mungu akipenda nitakuja kwenu tena.” Akaondoka Efeso kwa meli.(Matendo 18:21)
*daima katika sala zangu. Namwomba Mungu akipenda, anipatie nafasi nzuri ya kuja kwenu sasa.(Waroma 1:10)
*Hivyo, Mungu akipenda, nitaweza kuja kwenu na moyo wa furaha, nikapumzike pamoja nanyi.(Waroma 15:32)
*Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya.(1 Wakorintho 4:19)
*“Ninyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena. Mngalipaswa kusema: “Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki au kile” (Yakobo 4:14–15 Biblia)

Waislamu Wanachukua Wudhuu (Kutawadha) Kabla Ya Kuswali.
*“Na Musa na Haruni na wanawe baadaye akanawa mikono na miguu kwa maji kutoka humo. Mara nyingi walipokuwa wakenda ndani ya hema ya kukutania, au kuja mbele ya madhabahu, Walikuwa wakijiosha, kama Bwana alivyomwagiza Musa. (Kutoka 40:31-32 Biblia)
*Birika la kutawadhia utaliweka katikati ya hema la mkutano na madhabahu na kulijaza maji.(Kutoka 40:7)
*“Wale ambao hujitolea na kujisafisha kwa maombi katika bustani, wakiongozwa na mtu ambaye anasimama pale katikati ...” (Isaya 66:17 Biblia)
*Birika la kutawadhia na tako lake pia utaliweka wakfu kwa namna hiyohiyo.(Kutoka 40:11)
*Aliliweka birika la kutawadhia katikati ya hema la mkutano na madhabahu, na kutia maji ya kutawadha.
*“Utatengeneza birika la shaba la kutawadhia lenye tako la shaba, uliweke katikati ya hema la mkutano na madhabahu, na kutia maji ndani yake.(Kutoka 30:18)
*Shaba yote nyeusi aliyotumia Solomoni kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na vikalio kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu haikuweza kupimwa kwa uzito.(2 Wafalme 25:16)
*Wakaldayo walivunja vipandevipande nguzo za shaba ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, pamoja na vikalio vyake, birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwamo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaichukua shaba nyeusi mpaka Babuloni.
Biblia Inataja Nyumba Ya Sala (Maombi), Hii Inakuwa Tafsiri Ndani Ya Kiarabu Na Kiswahili Masjid Ni Msikiti
*Alitengeneza pia birika kumi za kuoshea vitu vilivyotumika katika tambiko za kuteketezwa. Tano kati ya bakuli hizo aliziweka kusini na tano upande wa kaskazini. Tangi lilitumiwa na makuhani kunawia.(2 Mambo ya Nyakati 4:6)

Nao walifunga kama sehemu ya ibada
*“Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa” (Mathayo 5:06 Biblia)
*“Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga... ..” (Mathayo 6:16-18 Biblia)
*Kisha nikatangaza kwamba watu wafunge hapo kwenye mto Ahava, ili tujinyenyekeze mbele za Mungu wetu, na kumwomba atuongoze katika safari yetu, sisi na watoto wetu na mali zetu zote.(Ezra 8:21-23)
*Isitoshe, wakawaweka rasmi wazee kwa ajili yao katika kila kutaniko,wakatoa sala na kufunga,nao wakawakabidhi kwa Yehova* ambaye walikuwa wamemwamini.(Matendo 14:23)
* Basi Yesu, akiwa amejaa roho takatifu, akaondoka Yordani, naye akaongozwa na roho kwenda nyikania kwa siku 40, akijaribiwa na Ibilisi.Kipindi hicho chote hakula chakula, basi muda huo ulipokwisha, akahisi njaa.(Luka 4:1, 2)
*12 “Hata sasa,” asema Yehova, “rudini kwangu kwa mioyo yenu yote,Kwa kufunga na kulia na kuomboleza.......15 Pigeni pembe Sayuni!Tangazeni watu wafunge; waiteni watu kwenye kusanyiko takatifu.
*“Hili ni sharti ambalo mnapaswa kulifuata milele: Siku ya kumi ya mwezi wa saba, nyinyi wenyewe na hata wageni wanaoishi miongoni mwenu, ni lazima mfunge siku hiyo na kuacha kufanya kazi.(Walawi 16:29)
*Kisha wanafunzi wa Yohane Mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?”(Luka 18:12)
*Watu wengine wakamwambia, “Wafuasi wa Yohane Mbatizaji hufunga mara kwa mara na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa.”(Luka 5:33)
Waislamu wanafunga funga za Hiari (Funga za Juma tatu na Alhamisi)
*“Mtu anaweza pia kufunga kwa hiari katika nyakati za Agano Jipya kwa kawaida juu ya Jumatatu na Alhamisi. Kwa kufanya hivyo kila wiki ilikuwa ni ishara ya maalumu ya uchamungu. (Biblia, Luka 18:12)

Waislamu Hawali Nguruwe, Damu, Au Wanyama Wafu.
*“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga ya”(Biblia Walawi 11:7-8)Baadaye katika aya ya 21 ya sura hiyo tunasoma yafuatayo: “usile kitu kilichokufa chenyewe.
*“... Na wale wenye kula nguruwe na uchafu mwingine, ndiyo, pia panya, watapotea wote, asema Bwana”. (Isaya 66:17 Biblia)
*“Bali tuwapelekee barua kuwaambia wasile vyakula vilivyotiwa najisi kwa kutambikiwa sanamu za miungu; wajiepushe na uasherati; wasile mnyama yeyote aliyenyongwa, na wasinywe damu.”(Biblia Matendo 15:20)
*“Ni lazima tu subiri si kwa kula damu. Kwa sababu damu ni roho na roho usile na nyama. Unapaswa kumwaga kwenye ardhi kama maji “. (Kumbukumbu 12:23-24 Biblia)
*“Na kama mtu wa nyumba ya Israeli, au mmoja wa wageni ambao wanaishi kati yao, akinywa damu yoyote, nami nitaweka uso wangu dhidi yake ambae anakunywa damu na kumkatilia kwake mbali na watu wake” (Mambo ya Walawi 17:10 Biblia)
*“Na hakuna damu yoyote mtayokunywa, ama kwa ndege au mifugo, bila kujali wapi mlipo. Kila mtu anaekunywa damu yoyote, huyo atakatiliwa mbali na watu wake “. (Walawi 7:26-27 Biblia)
*Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku. Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu.(Isaya 65:4)
*Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wapo watu wanaojitakasa na kutawadha wapate kuingia kwenye bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu. Watu hao hakika watakufa wote pamoja.(Isaya 66:17)
*Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku. Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu.(Isaya 65:4)
*Pia msile nguruwe, maana ijapokuwa kwato zake zimegawanyika sehemu mbili, yeye hacheui; hao ni najisi kwenu, msile nyama zao wala msiguse mizoga yao.(Kumbukumbu 14:8)

Ni Haramu Kwa Waislamu Kunywa Pombe.
*“Uasherati na pombe lazima uondoshe akilini” (Hosea 4:11 Biblia)
*Je, wamesahau kwamba watu wabaya hawataurithi Utawala wa Mungu? Msidanganyike! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti. wevi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang'anyi, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu. (Biblia Kwanza Wakorintho 6:9-10)
*Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza(Waefeso 5:18)
*Kwa hiyo Eli akamwambia, “Utaendelea kulewa hadi lini? Achana na kunywa divai.”(1 Samueli 1:14)
*Usiitamani divai hata kwa wekundu wake,hata kama inametameta katika bilauri,na kushuka taratibu unapoinywa(.Methali 23:31)

Katika Uislamu ni haramu Riba. Biblia pia inakataza Riba
*“Unaweza kukopa fedha kwa ajili ya maskini yeyote kati yenu, kati ya watu wangu, hivyo ni lazima si kitendo dhidi yake kama walaji riba. Wala kuongeza juu yake faida yoyote” (Biblia, Kutoka 22:25)
*“Usichukue faida yoyote ya ndugu yako, ama ya pesa au chakula au kitu kingine chochote ikawa umechukua riba” (Biblia, Kumbukumbu la Torati 23:19)
*“Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopeshawenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!”. Biblia (Luka 06:34)
*“... faida na kuchukua riba - Je, ndo ataishi? Hapana, lazima wafe, lakini kwa sababu yeye kashiriki katika maovu hayo, atakuwa katika adhabu na kifo. damu yake atakuja juu yake “. (Biblia Ezekieli 18:13)

Swadaqah ya kondoo mwanamke akijifungua. (hakika)
*“Na siku yake ya kujisafisha ikifika, ikiwa ni mvulana au binti, atachinja kondoo mwenye umri kwa sadaka ya kuteketezwa ... (Mambo ya Walawi 00:06 Biblia)

Waislamu Hutahiriwa
*“Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba '(Biblia, Luka 2:21)
*“Na Mungu akamwambia Abrahamu:”Utunze agano langu, wewe na uzao wako baada yako, na vizazi vyote. Na hili ndilo agano kati ya mimi na wewe na uzao wako baada yenu, ambaye mtazishika kila uume kati yenu kutahiriwa katika govi zenu, na hii itakuwa ni ishara ya agano kati ya mimi na wewe. Vizazi, kila mtoto wa kiume kati yenu atatahiriwa, wakati ni umri wa siku nane, kama walivyofanya mtumishi wa kuzaliwa katika nyumba yako na yeye ambaye kanunuliwa kwa fedha za kigeni kutoka kwa watu ambao si wa ukoo wako. Utahiriwa ni kwa mtumishi wenu na aliozaliwa katika nyumba yako na yule uliemnunua kwa fedha. Na ndiyo ahadi yangu katika mwili wako wazi kuwa agano la milele. Lakini mmoja wa watoto wa mataifa mengine mtu mmoja ambaye govi haijawahi kutahiriwa, naye atatengwa na watu wake. Yeye kavunjwa ahadi yangu. (Biblia, Mwanzo 9-14)
*“Na Ibrahimu alichukua mtoto wake Ismail na watumishi wake wote, mzaliwa wa nyumba yake na watu waliokuwa ------------ kwa fedha, kila uume kati ya watu wa Ibrahimu, na kutahiriwa siku hiyo govi yao ambayo Mungu alimwambia. Na Abrahimu alikuwa na miaka tisini na tisa. Wakati govi yake ilitahiriwa na mtoto wake Ismail alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu wakati govi yake ilitahiriwa. Tarehe ya siku hiyo Ibrahimu katahiriwa, na mtoto wake Ismail. Na ya watu wote katika nyumba yake, mzaliwa wa watumishi wake wa nyumbani na wale ambao walikuwa ------------ kwa fedha kutoka mataifa ya nje, walikuwa wametahiriwa pamoja naye “. (Mwanzo 17:23-27 Biblia)
*“Na Ibrahimu katahiriwa mtoto wake Isaka alipokuwa na umri wa siku nane, kama Mungu alivyomwamuru”. (Biblia, Mwanzo 21:04)
*“Agano la Kale liliteuliwa na Mungu kama ishara ya pekee kwa watu wa Israeli, na kama ukumbusho wa ahadi zao pamoja naye. (Kutoka 17:09 a, 3 Mwanzo 0:03, Yohana 7:22) Pamoja na kwamba mistari yote ya Wayahudi inashuhudia hivyo ikawa ni “moto” na utata suala ambalo lilisaidia kugawa watu baada ya kipindi cha Yesu.

Kuoa Wake Zaidi ya mmoja
*“Akichukua mke mwingine, basi asifanya upungufu wowote katika mlo wa zamani, mavazi au sheria za ndoa”. (Biblia, Kutoka 21:10)
*“Kama mtu ana wake wawili, mmoja anayempenda na mwingine ambaye hamuoni ...” (Biblia, Kumbukumbu la Torati 21:15)
*“Yeye alikuwa na wake wawili ...” (Biblia, Samuel 01:02)
*“Kwa hiyo, Daudi alifika huko pamoja na wake zake wawili ...” (Biblia ya Samuel 02:02)
*“Lakini wakati wa usiku aliamka na kuchukua wake wake wawili na watu wake wawili wahuduma na wanawe kumi na mmoja….” (Biblia, Mwanzo 32:22
*Lameki alioa wanawake wawili (Mwanzo 4:19)
*Watu wengi maarufu katika Agano la Kale walikuwa mitala. Ibrahimu, Yakobo, Daudi, Sulemani, na wengine, wote walikuwa na wake wengi. Katika 2 Samweli 12:8, Mungu, akizungumza kupitia ya nabii Nathani, alisema kwamba kama wake na mahawara wa Daudi hawakuwa wa kutosha, naye angempa Daudi zaidi. Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300 (kimsingi wake wa hali ya chini), kulingana na 1 Wafalme 11:3.

Walifuga ndevu
*“Msikate pande yote ya nywele zenu ya vichwa, wala msikate pande ya ndevu zenu. (Biblia, Walawi 19:27)
*Katika Biblia imetajwa katika maeneo mengi, kwamba manabii na waumini walikuwa na ndevu. Tazama kwa mfano Ezra 9:03, Mambo ya Walawi 21:05, Nehemia 13:26

Kwa mapitio hapo juu tumejifunza kwamba uislamu sio dini mpya bali ni muongozo uleule uliokuwa tangu Adam wala Muhammad sio mwanzilishi bali ni Muhuwishaji(mzinduaji) baada ya watu kuwa wapotevu.Zaidi ni kwamba Muhammad kapewa kitabu cha muongozo (quran) ili kupata updated za mafunzo ya muongozo wa mwenyezi mungu na kutubainishia mengi ambayo mitume wengine hawakubainisha zama zao.

YN.16:7-15
Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi (Muhammad) hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu(amekwisha kufika).8Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu (hakuna dini inayochambua dhambi na hukumu zake zaidi ya uislamu wala hakuna wanayemuita roho mtakatifu aliyebainisha haya).9Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi (waliishia kutaka kumuua); 10kwa habari ya haki (mambo ya haki ni kiama,kufa na kufufuliwa dalili za kiama Muhammad kazitaja), kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.12Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia (yesu hakukamilisha ujumbe wote wa mungu), lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa(hata sasa hukmu za uislamu wanazipinga hasa kwa mwamvuli wa haki za binadamu haki za wanawake,wenye imani ndio wenye kuyastahimili hukmu za Mwenyezi Mungu).13Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza (Muhammad amefikisha) awatie kwenye kweli yote (waumini wa kiislamu wanaijua haki na batili zote); kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe(quran 53:3.Wala hatamki kwa matamanio),lakini yote atakayoyasikia atayanena (atakayoyasikia ni yale aliyosikia mtume kutoka kwa malaika jibril,quran 53:4.Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa) na mambo yajayo atawapasha habari yake (Muhammad keshatabiri yaliyokwisha kutokea na yatakayotokea mbele yetu ikiwa ni pamoja na yale yatakatokea baada ya kufufuliwa kiundani zaidi hatua kwa hatua). 14Yeye atanitukuza mimi (Muhammad kamsifu sana yesu na kumsimulia mengi juu yake ikiwa ni pamoja na namna mwenyezi mungu alivyomuokoa juu ya fitna za shetani dhidi ya kifo cha laana msalabani,wakababatiziwa mtu mwingine wakijua ni yesu),kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu (Muhammad kahubiri aliyotumwa Yesu juu ya mungu mmoja asiye na mshirika na kuzisimamia amri zake) na kuwapasha habari (Muhammad katupasha habari zote yaliyopita,yaliyoko na yajayo kadiri alivyofunuliwa na Mwenyezi Mungu).15Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari (Muhammad hajaja na habari mpya wala dini mpya bali ametwaa yaleyale ya mitume waliopita kabla yake).
Kuhusu swali la kwanza 1.Je nikweli uislamu ni dini tangu Adamu (hajaianzisha Muhammad)? majibu na rejea ndio hizo na hitimisho ni kwamba UISLAMU sio dini mpya wala kuanzishwa na Muhammad bali ilikuwepo tangu Adamu.

Nipatapo muda inshallah nitaendelea na majibu ya swali la pili hatimaye nala tamu nikiamini nitakuwa nimejibu vyema swali la msingi la mtoa mada......Muwe na siku njema
 
chongoe

chongoe

Senior Member
Joined
Mar 22, 2019
Messages
113
Points
250
chongoe

chongoe

Senior Member
Joined Mar 22, 2019
113 250
Kila kitu kimeletwa na muumbaji, binadamu wa kwanza adamu, kwa sisi waislam, pia nabii ,kuanzia hapo mungu akaweka sheria zake, kupitia mitume, wake ili tutekeleze ibada ,jibu langu ,kwako ni kuanzia nabii Adam, mpaka leo aliekufa,na ataekufa ,atakufa uislam tayari ushakuwepo ,sijui upande wa pili wakujibu
 

Forum statistics

Threads 1,304,159
Members 501,282
Posts 31,504,846
Top