Kifupi watu inabidi wajue maana halisi ya dini...
Hizo sheria,Mungu alizoweka hajaweka kukupima kiwango chako cha utii kwako kwake,ameweka hili uweze kuishi dunia vizuri na watu wanaokuzunguka...
Usiue,kwani ukiua wewe, Mungu Ana hasara gani?kama sio utaozea jela tu.usizini,kwani ukizini, Mungu Ana hasara gani???Kama sio utakufa mwenyewe tu.mpende jiran yako,je ukimpenda Ni kwa faida ya Nani?kama sio wewe mwenyewe???
Mnakalili sana hizi dini,dini zipo pale kukufanya uishi maisha ya amani,upendo na furaha hapa duniani..
Matokeo yake,jitu linatumia dini kumdharau mwingine,kumnyima mtu kazi,kumwita mwenzake gaidi,kumuona mwenzake ndo mchafu sana yaani concept nzima ya dini imepotea,leo hii watu wanauana sababu Ni dini tofauti!sasa Nini faida ya dini Kama inakupa chuki?inakufanya umdharau mwingine, inakufanya ujitenge na wenzako!!!
Dini sio kwa ajili ya Mungu kwa ajili yako wewe uishi vizuri duniani kabla ya kwenda mbinguni.