Watu wa mji wa Mbeya wamekuwa ni watu wa ajabu sana. Wanafanya siasa za kitoto sana zisizo za kistaarabu.
Kwa sasa ukizungumzia Mbeya ni kama unazungumzia mji wa 'masela ma..' awa watu walimzomea mpaka rais wa nchi na sababu hawana.
Mji sasa unaongozwa na mawazo ya Sugu na mnamuita rais wenu.. Just imagine?
Nyie siasa za vyama vingi mnachukulia ni ugomvi na fujo kwenu huko sasa kila kitu mmechukulia siasa ata timu yenu inakufa sababu ya siasa za kipuuzi.
Sasa nimeshanga mpaka hizi kampeni kazi yenu ni kuzomea zomea wagombea msiowunga mkono. Sasa sielewi ukishazomea ndio utapata nini na fujo tangu mzianze mmepata nini.
Mbeya inasikitisha imekuwa inawaiga watu wa arusha. Watu wa arusha wanajulikana hao hatuna tatizo nao cha arusha ndio tatizo. Sasa nyie mtaishi hivyo mpaka lini.
Sasa naomba mchukue ushauri wangu mbadilike, msijifanye nyie mnauchungu na chama kuliko watu wa Kilimanjaro.
Msipobadilika mwaka huu mtailaumu serikali maana Mzee Jakaya kawalea sana. Badilisheni siasa zenu ziwe za kijanja or else.
Pole mkuu naona unaandika huku machozi yakikutoka kuona mtu unaemsupport anazomewa. Huwezi kuwa pangia watu wamshangilie nani au wamzomee nani, wao wameua.
Ingekuwa wanamshangilia usingiazisha huu uzi, wapo wengi tu wanao shangilia bila sababu lkn mbeya sababu nikuwa hawaitaki ccm.