Watu wa Kusini mtaacha lini kula ngozi ya ng'ombe?

Wajameni watu wa Lindi na Mtwara na wilaya zake zoooote acheni Tabia ya kula ngozi ya ng'ombe mkiifanya eti supu,yaani juzi nimeenda Kijiji flani nikakuta jungu liko juani Tena kijiweni mchana kweupe nikauliza Kuna nini mle nikajibiwa supu, kipande mia tatu viwili miatano nikasema niwekee vya afumbili,Loooo!!!!

Kufumba na kufumbua kuliona supu lenyewe ngozi tupuu mchuzi mweusii alafu wenyewe mmejazana tele mmelizunguka jungu wake Kwa waume eti mnagombea ngozi Tena zingine mmechomeka stiki ukigusa tu mwenye jungu utamskia ngozi hiyo Ina mtu imechaguliwa kaka huoni stiki hiyo!

Nikaishiwa pozi nikashindwa kula ngozi na ngozi zingine mmeweka kwenye kiroba eti Kwa ajili ya kesho !!sasa nawauliza nyie watu wa Lindi na mtwara kwani nyie ng'ombe hamna huko vijjini Hadi mpike ngozi kufanya supu?kibaya kilichoniuma mkasema Hela niliyotoa hamrudishi acheni hizo bhana
Ndugu yangu kwa uichoakiandika hapa watanzania tuna maisha mazuri sana. Nimekutana na wakongo na watu wa west afrika huku nilicokiona aisee. Nilienda kwenye event yao ya vyakula vya kiafrika. Watu wanakula zile funza za magogo ya miti. Na viwavi pia ni chakula pendwa nilibaki nashangaa.
 
Nilienda kijiji cha Luchelegwa Ruangwa Lindi pale barabarani aloo ngozi ya ng'ombe imepikwa kama supu🤣🤣🤣🙌
 
Wajameni watu wa Lindi na Mtwara na wilaya zake zoooote acheni Tabia ya kula ngozi ya ng'ombe mkiifanya eti supu,yaani juzi nimeenda Kijiji flani nikakuta jungu liko juani Tena kijiweni mchana kweupe nikauliza Kuna nini mle nikajibiwa supu, kipande mia tatu viwili miatano nikasema niwekee vya afumbili,Loooo!!!!

Kufumba na kufumbua kuliona supu lenyewe ngozi tupuu mchuzi mweusii alafu wenyewe mmejazana tele mmelizunguka jungu wake Kwa waume eti mnagombea ngozi Tena zingine mmechomeka stiki ukigusa tu mwenye jungu utamskia ngozi hiyo Ina mtu imechaguliwa kaka huoni stiki hiyo!

Nikaishiwa pozi nikashindwa kula ngozi na ngozi zingine mmeweka kwenye kiroba eti Kwa ajili ya kesho !!sasa nawauliza nyie watu wa Lindi na mtwara kwani nyie ng'ombe hamna huko vijjini Hadi mpike ngozi kufanya supu?kibaya kilichoniuma mkasema Hela niliyotoa hamrudishi acheni hizo bhana
Mlo wa ngozi ni lishe bora, wachina wanakula ngozi ya punda na ni very health food. Ukienda kwenye hotel unakutana na gelatin ambayo hutengenezwa kutokana na ngozi
 
Ndugu yangu kwa uichoakiandika hapa watanzania tuna maisha mazuri sana. Nimekutana na wakongo na watu wa west afrika huku nilicokiona aisee. Nilienda kwenye event yao ya vyakula vya kiafrika. Watu wanakula zile funza za magogo ya miti. Na viwavi pia ni chakula pendwa nilibaki nashangaa.
West Africa na china mlo wa ngozi ni special delicacy - sticky rice ni mlo wa heshima
 
Msimu huu wa bamvua tumetoka kuchokoa kumbwa na aina nyingine ya seashells kama vile simbi, makome, mwezi, malikalula na viokolo. Hivi vyote kama ungeviona kwa macho ndiyo ungeshangaa zaidi na vinaliwa fresh tu na wakazi wa huku.
 
Ndugu yangu kwa uichoakiandika hapa watanzania tuna maisha mazuri sana. Nimekutana na wakongo na watu wa west afrika huku nilicokiona aisee. Nilienda kwenye event yao ya vyakula vya kiafrika. Watu wanakula zile funza za magogo ya miti. Na viwavi pia ni chakula pendwa nilibaki nashangaa.
Watu wengi esp. Wabongo wa Dasilama tunayo bado mengi ya kushangaa. Labda hii ni kutokana na kujifungia hapo Dar au hatujishughulishi kutaka kujua na ya huko kwingine. Funza uliowataja hata hapa Tz wanaliwa ila sema sio chakula popular huko mjini. Kule Ludewa pembezoni mwa ziwa Nyasa kuna aina fulani ya viwavi (Catepillars)hutokea ziwani na wavuvi huwanasa kwa wingi na huuzwa wakiwa wamevirigwa kama tonge kubwa la ugali- ni watamu sana.
 
Nasikia hata watu wa Kondoa wanakula Ngozi ya Ng'ombe
 
Ulikosa hata sikio? Aisee nilikuta mchaga mwingine ana genge lake huko singida kijijini kabisa, kuna lingozi alinionyesha limechemshwa sijui ni la sehemu gani ya ngombe, wenyewe wanaliita KOMBAT, nililitafuna mazee, ila hadi leo sijui ilikuwa ni ngozi ya kiungo gani cha ngombe.
 
Kulitoke league ya shule (Mbuzi cup) pale Maji ya Chai na HKL kuntu wakabeba Mbuzi,sasa aliliwa Mbuzi na ngozi kwa msisitizo wa jamaa mmoja kutoka Mtwara.

Ngozi ni nyama,mbona kwa Donald trump,tuna kula mpaka ngozi,kiroho Safi kabisa.
 
Msimu huu wa bamvua tumetoka kuchokoa kumbwa na aina nyingine ya seashells kama vile simbi, makome, mwezi, malikalula na viokolo. Hivi vyote kama ungeviona kwa macho ndiyo ungeshangaa zaidi na vinaliwa fresh tu na wakazi wa huku.
Safi kabisa - Nimeipenda hiyo comment👆👆. Wengi wamejikaririsha kwamba chakula au mboga ni Ugali, Wali, Mihogo, Mh. Mkuu wa meza, n.k. wanajizima data hawatambui kwamba wapo pia hawa nao huliwa: fuko, panya pori almaarufu kama Fudi au samaki nchanga(Sio wale wakaao ndani ya nyumba wanakula mpaka nguo),ndege pori eg. kwelea-kwelea, nzige/senene, mchwa n.k.
 
Nenda Nigeria ukajionee ngozi inavyoliwa
 
Back
Top Bottom