Watu wa Kusini mtaacha lini kula ngozi ya ng'ombe?

Watu wa Kusini mtaacha lini kula ngozi ya ng'ombe?

Naona sasa kuna ugomvi wa kikanda mara yule kaanzisha uzi wa wasukuma wanakula saana, mara watu wa kanda ya ziwa wa chale hadi kwenye tako, huyu nae kaamka na watu wa kusini kila ngozi ya ng'ombe! Dah!
 
Wajameni watu wa Lindi na Mtwara na wilaya zake zoooote acheni Tabia ya kula ngozi ya ng'ombe mkiifanya eti supu,yaani juzi nimeenda Kijiji flani nikakuta jungu liko juani Tena kijiweni mchana kweupe nikauliza Kuna nini mle nikajibiwa supu, kipande mia tatu viwili miatano nikasema niwekee vya afumbili,Loooo!!!!

Kufumba na kufumbua kuliona supu lenyewe ngozi tupuu mchuzi mweusii alafu wenyewe mmejazana tele mmelizunguka jungu wake Kwa waume eti mnagombea ngozi Tena zingine mmechomeka stiki ukigusa tu mwenye jungu utamskia ngozi hiyo Ina mtu imechaguliwa kaka huoni stiki hiyo!

Nikaishiwa pozi nikashindwa kula ngozi na ngozi zingine mmeweka kwenye kiroba eti Kwa ajili ya kesho !!sasa nawauliza nyie watu wa Lindi na mtwara kwani nyie ng'ombe hamna huko vijjini Hadi mpike ngozi kufanya supu?kibaya kilichoniuma mkasema Hela niliyotoa hamrudishi acheni hizo bhana
Suna ya maswahaba wa mtume hiyo ...sitaki maswali
 
Back
Top Bottom