Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,598
- 215,322
Niliangalia kipindi kimoja katika luninga, kilionyesha mila na desturi za watu wa Fiji, kwa kweli wale ni wenzetu kabisa.
Inasadikia miaka mingi iliyopita, Rufiji kuna watu walisafiri katika chombo kutumia Bihari. Katika safari ile, chombo kilipaigwa na dhoruba kali na kilipotea baharini. Kwa uwezo wa Mungu chombo kile kilitua katika kisiwa na waja wale walianza maisha pale.
Katika kipindi nilichoangalia wafiji wanapika wali wa nazi na samaki aina ya kamba kwa mchuzi wa nazi. Wanakula mihogo, magimbi na wali kama chakula kuku. Majani ya magimbi yanapikwa na kuchangwanywa na nyama. Hii ni desturi ya kawaida kwa watu wa Pwani.
Wanatengeneza halua kutumia mihogo na pia wanapika ndizi mzuzu mbivu za nazi. Halua na ndizi mzuzu hutumika kama chakula cha ziada baada ya mlo.
Sura zao pia ni kama za watu wa Ukanda wa Kusini. Hakika wale ni ndugu zetu kabisa.