Watu wa Fiji ni ndugu zetu, mila na tamaduni zetu zinafanana

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,275
Niliangalia kipindi kimoja katika luninga, kilionyesha mila na desturi za watu wa Fiji, kwa kweli wale ni wenzetu kabisa.

Inasadikia miaka mingi iliyopita, Rufiji kuna watu walisafiri katika chombo kutumia Bihari. Katika safari ile, chombo kilipaigwa na dhoruba kali na kilipotea baharini. Kwa uwezo wa Mungu chombo kile kilitua katika kisiwa na waja wale walianza maisha pale.

Katika kipindi nilichoangalia wafiji wanapika wali wa nazi na samaki aina ya kamba kwa mchuzi wa nazi. Wanakula mihogo, magimbi na wali kama chakula kuku. Majani ya magimbi yanapikwa na kuchangwanywa na nyama. Hii ni desturi ya kawaida kwa watu wa Pwani.

Wanatengeneza halua kutumia mihogo na pia wanapika ndizi mzuzu mbivu za nazi. Halua na ndizi mzuzu hutumika kama chakula cha ziada baada ya mlo.

Sura zao pia ni kama za watu wa Ukanda wa Kusini. Hakika wale ni ndugu zetu kabisa.
 
hahaahaha kwahiyo watu wa FIJI kama RUFIJI au sio ila wale binadamu wa visiwa vya Pacific ni Wabongo machotara waliochangamka ukienda huko Vanuatu, Kiribati, Tonga, Fiji, Tuvalu, Papua New Guinea nk ni utakuta jamii zenye mfanano sana na jamii za hapo Madagascar, Mauritius, Seychelles, Comoro Zanzibar na hii East Africa yote na wana uswahili sana nilikua naangalia fact kuhusu Vanuatu yaani wale ni Wamakonde waliochangamka zamani walikula nyama za watu vile vile Konde waliacha kula watu wakahamia panya ila kiboko yao ni Wasakalava wa Madagascar wale washenzi walikua na mitumbwi ya vibwengo walikua wanapiga kasia baharini kama mazombi na wakifika kwenu mtaipata fresh uliza kilichowakuta watu wa Kilwa Kisiwani na Mafia walichofanywa na hao Sakalava canibals!
 
Mhhh.....chombo kutolewa Bahari hindi East Africa hadi pasifiki, ilikuwa dhoruba kweli kweli
Broo kuna makabila kama Wasakalava wa Madagascar hawa washenzi walikua canibals walikua na mitumbwi ya vibwengo yaani wanapiga kasia far distance walifika mpaka huko India na far East na wakiwakuta jamii zenu wanawapa kichapo na mnatafunwa!

Hahaaahaa
 
Wabongo kwa kujipendekeza tupo vizuri. Tunaojipendekeza kwao hata hawatutaki kama nchi za ukanda wa south africa.
 
Back
Top Bottom