Tuheshimu Makabila na tamaduni za watu, mapungufu tuyaache

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Declaration of Interest, mimi ni mlMkinga lakini cha kushangaza nimekutana na Mchaga ananiuliza huendi ukinga?

Jibu rahisi lilikuwa wakinga tuna mila na tamaduni zetu tunazowasiliana na ndugu na jamaa wakati wote wa mwaka na muda wowote ukihitajika nyumbani unarudi na hii haitegemei siku.

Huyu jamaa wa kichaga sijui ni mchaga wa eneo gani maana kila akizaliwa mtoto mdogo anamchukua mke na mtoto hasa desemba kwenda kufanya utamaduni eti kuthibitisha mtoto ni wake au amepigwa na mke na shughuli yenyewe kwa mujibu wake anatafutwa mbuzi na kuchinjwa akiwa mbuzi amechuchumaa huku kawekwa jani mdomoni. Akipiga kelele mbuzi wakati anachinjwa eti mtoto amepigwa.

Kwanini nimeandika huu uzi na huo utangulizi

Mosi,Dunia imebadilika sana kwa sasa watu wanafanya tours na vacation nchi mbalimbali, leo hii kila siku wakinga maelfu wapo China na Dubai na wengine yamekuwa makazi yao huko na wanatusaidia kusafirisha mizigo?

Je, utawalazimisha watoke Dubai na China kwenda kunywa pombe makete wakati huo hali ya maisha ilikuwa mbaya lakini sasa kwenda Dubai ni sawa na kupanda daladala tu.

Pili, kiwango cha elimu kipo juu sana, ni ngumu sana kumkuta mkinga anafanya makafara ya mbuzi na ng'ombe. Haya mambo yalifanywa na babu zetu kwa kukosa maarifa na uelewa wa mafanikio. Nashangaa huyu ni mchaga msomi lakini anaamini vipimo vya kienyeji kuthibitisha uhalali wa mtoto kuwa ni wake.

Tatu, ni imani potofu kuwa tunaenda kijijini kukutana na wazee. Yaani unashindwa kukaa karibu na wazazi wako mwaka mzima eti unasubiri desemba siku tatu kumdanganya mzee na nyama za mbuzi, ni wazee gani hao wanaishi milele vizazi na vizazi. Unakutana na mchaga ana miaka 80 anakuambia anaenda kuona wazee. Ni wazee gani hao?
 
Back
Top Bottom