Haya mambo mbona hata huku kwetu Karatu yapo.
Hayo ni maono yako. Wewe ni miongoni mwa waliozaliwa Aghakhan au Marie Stoppes. Kama umejitahidi sana labda umezaliwa Ocean Road au Muhimbili. Sijui kama unaijua Sewa Haji Hospital. Sanasana unajua, kama unajua, kuwa Sewa haji ni wodi mojawapo pale Muhimbili kwa sasa.
Endelea kukua kijana. Maana huwezi jua labda mama yako alikuwa girlfriend wangu, kama alikuwa kashafika mjini.
mkuu ukiona wewe unalala, usifikiri kila mtu anapo pa kulala. kuna watu hawajui kesho watakula nini huko majuuu...nishaombwa sana hela na diaspora nikiwa huko, ikabidi nianze kuwakimbia, kila nikimwona nakula kona.
Wapo bussy kuuza vichwa, miguu, firigisi na utumbo wa broila
Wako hivyo hivyo hao , utawasikia mara pesa mkoani taabu, ndorooooobo zenu. Mnaishia kumiliki gari mikweche na nyumba za kupanga
aaahh! isiwetabu mjini watu wanatafuta pesa hatutafuti mtu..by theway Ndoroooobo mwenyewe na wenzako wa mkoani wanaopenda kutafutwa.
Watu wa Dar bwana,
Kabla hujaenda ukimpigia simu anakwambia karibu sana kaka ukija usiache kunitafuta. Ukifika ukampigia kwanza anakuuliza umefikia wapi, unamwambia nipo Kawe, utasikia nipo Kibaha kuna issue nashughulikia ntakuchek kesho.
Kesho ndo hutaiona simu yake ng'oo. Ukimpigia simu kumwambia kesho naondoka, utaskia mbona fasta kaka, daah sema umekuja bahati mbaya sana hivi nipo taiti kiaina ila ukija tena tutamit tu.
Woote sound zao hizo hizo, utadhani mwalimu wao mmoja.
Halafu wao wakija huku wanapopaita mikoani, Anataka uwe nyuma yake 24/7, utadhani mnatafuta wadhamini. Stori zake sasa. Hivi huku mikoani mnaishije? hakuna mzunguko wa hela kabisa.
Hiyo mizunguko ya hela huko Dar ingekuepo si wote mngekuwa Bakhressa. Tusiharibiane swaumu aisee, acheni hizi tabia.
Kweli aisee watu wa Dar mnazinguana sana.
[/QUOTE
hii post ina ukweli kabisa.