Watu wa Dar es Salaam muache hii tabia, mnakera

Watu wa Dar es Salaam muache hii tabia, mnakera

na nyie si mbaki huko mikoani kwenye maisha mazuri? au mkija DAR mfanye issues zenu kisha muondoke bila kutafuta hao watu wa DAR kwani mtapungukiwa nini??!
 
Watu wa Dar bwana,

Kabla hujaenda ukimpigia simu anakwambia karibu sana kaka ukija usiache kunitafuta. Ukifika ukampigia kwanza anakuuliza umefikia wapi, unamwambia nipo Kawe, utasikia nipo Kibaha kuna issue nashughulikia ntakuchek kesho.

Kesho ndo hutaiona simu yake ng'oo. Ukimpigia simu kumwambia kesho naondoka, utaskia mbona fasta kaka, daah sema umekuja bahati mbaya sana hivi nipo taiti kiaina ila ukija tena tutamit tu.

Woote sound zao hizo hizo, utadhani mwalimu wao mmoja.

Halafu wao wakija huku wanapopaita mikoani, Anataka uwe nyuma yake 24/7, utadhani mnatafuta wadhamini. Stori zake sasa. Hivi huku mikoani mnaishije? hakuna mzunguko wa hela kabisa.

Hiyo mizunguko ya hela huko Dar ingekuepo si wote mngekuwa Bakhressa. Tusiharibiane swaumu aisee, acheni hizi tabia.

Kweli aisee watu wa Dar mnazinguana sana.
Mkuu ujasiri wa kuwatafuta hao jamaa waliojaa dhiki unautoa wapi? Dar wana shida asikwambie mtu. Ila siku nyingine ukienda mchukulie Sato kama unatoka kanda ya ziwa, Mchele kama unatoka Mbeya (tena ule wa Kyela), utaona jinsi anavyokuja fasta!! Mboga yenyewe akinunua 1/2 kilo ya nyama anajaza viazi mviringo eti ndo mboga hiyo! Sijui wanaishije hawa!!
 
Back
Top Bottom