Watu wa Dar es Salaam muache hii tabia, mnakera

Watu wa Dar es Salaam muache hii tabia, mnakera

Kilaza

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
3,324
Reaction score
1,379
Watu wa Dar bwana,

Kabla hujaenda ukimpigia simu anakwambia karibu sana kaka ukija usiache kunitafuta. Ukifika ukampigia kwanza anakuuliza umefikia wapi, unamwambia nipo Kawe, utasikia nipo Kibaha kuna issue nashughulikia ntakuchek kesho.

Kesho ndo hutaiona simu yake ng'oo. Ukimpigia simu kumwambia kesho naondoka, utaskia mbona fasta kaka, daah sema umekuja bahati mbaya sana hivi nipo taiti kiaina ila ukija tena tutamit tu.

Woote sound zao hizo hizo, utadhani mwalimu wao mmoja.

Halafu wao wakija huku wanapopaita mikoani, Anataka uwe nyuma yake 24/7, utadhani mnatafuta wadhamini. Stori zake sasa. Hivi huku mikoani mnaishije? hakuna mzunguko wa hela kabisa.

Hiyo mizunguko ya hela huko Dar ingekuepo si wote mngekuwa Bakhressa. Tusiharibiane swaumu aisee, acheni hizi tabia.

Kweli aisee watu wa Dar mnazinguana sana.
 
Wako hivyo hivyo hao , utawasikia mara pesa mkoani taabu, ndorooooobo zenu. Mnaishia kumiliki gari mikweche na nyumba za kupanga
 
Kilaza

HAH HAH HAH HAH HAH HAH HAH umenifanya nvunje mbavu na swaumu hi
 
Last edited by a moderator:
KIONGOZI ni kama ulikuwa nami moyoni,binafsi nimeishi Dar kwa miaka 10 nikisoma na kufanya kazi,nimekuwa nikiwathamini sana ndugu na jamaa wanaokuja wakitokea mikoani.Ni miaka minne sasa nipo nje ya Dar,ajabu ninapokwenda huwa natamani kuwaona jamaa na marafiki,ninapowapigia simu wengi wao wanakuwa na majibu hayo hayo!!...SIJUI NI UGONJWA GANI HUU?..Mara nipo bize,mara tuonane kesho,mara nitakupigia baadae,mara simu hazipokelewi,mara nipo katika foleni,mara....daaah!!ISIWE TAABU Nafahamu wengi wao ni HOFU ya kuonekana wamechoka ama kuogopa kumkarimu mgeni wa Mikoani.Nakupongeza rafiki yangu Tall (Tabata Kimanga) na Fulgence wa Mwanagati kwa kutokuwa na tabia hiyo!!!
 
Hiyo ni tabia yao kabisa wanajidai busy sana hawa jamaa. Hahahaaa
 
Back
Top Bottom