Watu wa Dar es Salaam muache hii tabia, mnakera

Hawa watu wa Dar itabidi wajirekebishe kwa kweli
 
Kusema kweli mimi Dar nilienda kwaajili ya shule....sasa nilienda kwanza then nikarudi kujiandaa huku nikiwa nimechukua namba ya mwenyeji mmoja anipokee maana niliogopa kupotea badala ya kupanda gari za mwenge nikapanda za buguruni....sasa siku naenda nikampigia yule mwenyeji ajiandae kunipokea akaniambia haina shida....mida ya saa tisa akazima simu....hadi nashuka ubungo mtu hapatikani...Sijui alijua nataka kufikia kwake??? nashukuru Mungu nilifika salama nilikokuwa naenda na yeye sikumuuliza kitu
 
mkuu pole na swaumu...mimi nampigia msela simu tukutane mahali tupate mbili tatu syori za hapa na pale siku iende wala sitaki kwenda kwake bado ananizungusha
Hahaha Pole Kilaza,
Aisee umenichekesha sana.
Nimefurahi sana kwa kuwa Muwazi na kuwa shuhuda.Na kuonyesha kwamba wewe umetoka mkoani kwa nia njema.

Wengi wanaoishi Dar huona kwamba mtu akitoka mkoani yoyote ana shida.Na wengie hufanya sifaa wakiwa Mikoani,sasa anajua kabisa wewe ukiona maisha yake halisi na ukilinganisha namasifa yake basi utamshusha hadhi.

Lakini ukweli ni kwamba Maisha ya Dar na tunavyokuja huko Mikoani yaani haviendani kabisaaa.
Hii ndio Bongo Bakora

Mie nakushauri we mpotezee tu,wengi wanaoishi Dar huwa wanarudi Mikoani wakiwa wagonjwa hasa wa ngoma.
 
Mkuu ukilegea sana utakuwa na wageni hata 10 kwa siku, matokeo yake utapoteza mda wako wa kutafuta. Isitoshe kama ni mawasiliano ya kawaida tu hata simu inatosha sana, si lazima kuonana uso kwa uso. Cha ajabu nchi za wenzetu walioendelea kuonana na mtu lazima kufanya appointment, tena kuonana kwao ni kimaslahi zaidi, si mambo ya ujomba, undugu na blabla
Kiafrika afrika ndugu
 
Nimecheka mbaya sana, we mtu kama unawajua vizuri wengi wakazi wa Dar hasa vijana wa 20's to 40's ni mawenge sana
 
Kusema kweli mimi Dar nilienda kwaajili ya shule....sasa nilienda kwanza then nikarudi kujiandaa huku nikiwa nimechukua namba ya mwenyeji mmoja anipokee maana niliogopa kupotea badala ya kupanda gari za mwenge nikapanda za buguruni....sasa siku naenda nikampigia yule mwenyeji ajiandae kunipokea akaniambia haina shida....mida ya saa tisa akazima simu....hadi nashuka ubungo mtu hapatikani...Sijui alijua nataka kufikia kwake??? nashukuru Mungu nilifika salama nilikokuwa naenda na yeye sikumuuliza kitu

hahahahahahah sipati picha kama nakuona ulivyo haha
 
We ukitaka umpate Mpigie Weekend na kama ni mtu wa Pombe basi mwambie upo na Jamaa zako Bar fulani.
Uone dakika kumi kaisha fika.Na cha ajabu anaweza kuja yeye na Company lake waje wapombeke.

Sasa akiishalewa anakuwa hana akili za kufikiria,sasa hapo ndio unapoamua kumkodia gari umpeleke kwake na wewe ukiwemo.Aisee ukifika huko ndio utajua mtu anavyoishi.Siku ya pili akijua lazima akuitie Polisi aseme kwamba umempeleka Kwamtogole na yeye anaishi Masaki.
 
Duuh...umemaliza yote we hujui km mjini chuo kikuu ndo umeisoma sasa Dar watu tunajuana wenyewe tunavyoishi wakuja ukija huku kwa kutaka company utachemsha Jiji la mishemishe hili
 
Kama sisi tunaotokea MWANZA ukishamwambia nimekuja na samaki, dagaa, mahindi na jiani nitapitia mkaa andaa kabisa usafiri.
Utaanza kupigiwa saa 10jioni mumefika wapi?

Sasa ufike hapo hauna kitu, utasikia ngoja nimucheki huyu jamaa wa usafiri-jumla

Tena nyie wa Mwanza ndio tunawaogopeni sana. Mnapiga mizinga balaa. Afu hata kuvuka barabara mpaka muombe msaada.
 
Hahaha Pole Kilaza,
Aisee umenichekesha sana.
Nimefurahi sana kwa kuwa Muwazi na kuwa shuhuda.Na kuonyesha kwamba wewe umetoka mkoani kwa nia njema.

Wengi wanaoishi Dar huona kwamba mtu akitoka mkoani yoyote ana shida.Na wengie hufanya sifaa wakiwa Mikoani,sasa anajua kabisa wewe ukiona maisha yake halisi na ukilinganisha namasifa yake basi utamshusha hadhi.

Lakini ukweli ni kwamba Maisha ya Dar na tunavyokuja huko Mikoani yaani haviendani kabisaaa.
Hii ndio Bongo Bakora

Mie nakushauri we mpotezee tu,wengi wanaoishi Dar huwa wanarudi Mikoani wakiwa wagonjwa hasa wa ngoma.

Sasa kama mnajua wana shida mnawatafutia nini? Si mpige kimya??
 
Hii n kweli! na huwez kupata mikoa mwingne kama dar!
 
Kusema kweli mimi Dar nilienda kwaajili ya shule....sasa nilienda kwanza then nikarudi kujiandaa huku nikiwa nimechukua namba ya mwenyeji mmoja anipokee maana niliogopa kupotea badala ya kupanda gari za mwenge nikapanda za buguruni....sasa siku naenda nikampigia yule mwenyeji ajiandae kunipokea akaniambia haina shida....mida ya saa tisa akazima simu....hadi nashuka ubungo mtu hapatikani...Sijui alijua nataka kufikia kwake??? nashukuru Mungu nilifika salama nilikokuwa naenda na yeye sikumuuliza kitu

Ungenawa uso kwanza uondoe tongotongo ndo uingie mjini. Mjini shule.

Mi naishi Bunju unanipigia simu tuonane nikupeleke Mbagala.... Utasubiri sana. Someni daladala zimeandikwa ruti kwa mbele.
 
Back
Top Bottom