Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi

Hata mimi niliwahi kumuacha mtu sababu ya ujinga wake. Alipofika ndio ananiambia niende nikamchukue,wakati anatoka mkoani hakuniambia.
Nikamwambia alale hapo, nitaenda kesho asubuhi kwa kuwa huku niliko kwa majira haya kuna Panya road.
Aligongwa na mbu usiku mzima nikaenda kesho saa 4 asubuhi.
Hilo lilikuwa fundisho, kwa sasa kila akitaka kuja lazima anipigie.
Una huruma sana me hata mwakani nisingemfata
 
Kiukwel hii hali sio dar pekee hata tulio nje ya tz hali hii inatupata sana ,, fikiria mtu mlikua jiran tu mmekua wote anatafuta namba yako anakupigia anasema yupo sehemu kaja kutafuta maisha ,,anaomba afikie kwako hapo hapo anakwambia yupo na rafiki yake ,,unafikiria ukiangalia unafamilia maisha yenyewe ya dollars yalivyokua high ,,,kinachofuata hapo unamblock kabisaa.
 
Nimepanga ka gheto kangu uchwara mitaa ya uswahilini hivi.
Siku moja shangazi yangu ambae hatujawasiliana kwa muda mrefu alinipigia simu na kuniambia Kuna ndugu yako humfahamu anakuja naomba afikie hapo kwako.
Nilikosa Cha kusema maana maisha yangu nayajua mwenyewe, ilibidi nimshirikishe bi mkubwa akanisaidia kuninasua kwenye ule msala.

Nb. Ndugu uliyeko mkoani unakuja Dar (kwa sababu zozote zile) hakikisha umejipanga vizuri na upunguze matarajio makubwa kwa ndugu zako walioko huku. Mtalaumiana.
 
Hata ingekua wewe unashindia mihogo na maji na unalala kwenye kachumba kadogo mvua ikinyesha maji yanajaa kama umelala kwenye mtungi ungekubali kupokea ndugu?

Mi siyo mtu wa daslam lakini nawapongeza kwa ujanja ujanja huo wa kuzima simu na kukimbia ndugu ukienda tu kuoga wanakwambia bafu halina mlango nenda na shuka uweke mlangoni, sasa akupokee na wewe atakulisha nini si mtachemsha matawi ya mpapai ndo iwe mboga
 
Kuna ndugu zetu walisema Mzee anataka kuja hosp
Tukawaambia sawa,ila sisi tunashinda kazini kama wanga saa 11 asbh tunaondokakurudi nj usiku saa3,hivyo kama ni kuja basi aje na kijana ambaye atamsaidia Mzee .
Wakaona tunawabania..
Kwahiyo wakaahirisha kuja kwetu..wakasafiri kimyakimya.

Kumbe kule Kaka yao alimtafuta schoolmate wake,ambaye hata walikuwa hawawasiliani...akamwambia awapokee ndugu zake hao.

Jamaa eti wamewasiliana vizuri, baadaye akapotea hewani.
Alipotea mazima.

Sisi hatuna hili wala lile,Saa2 usiku tunapigiwa simu na hao wasafiri kututaarifu kuwa wapo njiani ,tuende kuwapokea,,na wamekaribia Mbezi.
Imagine mtu hakukutafuta hata kukujulisha kama anasafiri,,anakuja kushtua tu usiku huohuo ukampokee.
Tulishakula ,tunajiandaa kulala.

Tukaanza kuhaha kupika upya,,it's tiresome.,kutafuta mboga na Nini.

Ndugu zetu wa mikoani muwe wastaarabu.,unaenda sehemu basi toa taarifa mapema.
 
Ndugu zetu wa mikoani muwe wastaarabu.
Hawakufanya vizuri. Popote mtu anapoenda iwe mjini au kijijini kutoa taarifa ni jambo jema. Unawapa wenyeji wako muda wamapokezi mazuri. Binafsi sijawai kukutwa na scenario ya hivi. Sipati picha mlikasirika kiasi gani. Na ukute fridge liko empty kabisa.
 
Hata ingekua wewe unashindia mihogo na maji na unalala kwenye kachumba kadogo mvua ikinyesha maji yanajaa kama umelala kwenye mtungi ungekubali kupokea ndugu?

Mi siyo mtu wa daslam lakini nawapongeza kwa ujanja ujanja huo wa kuzima simu na kukimbia ndugu ukienda tu kuoga wanakwambia bafu halina mlango nenda na shuka uweke mlangoni, sasa akupokee na wewe atakulisha nini si mtachemsha matawi ya mpapai ndo iwe mboga

Na mtu anaishi kwako halipi kodi na hajiongezi wala kusaidia chochote kulipa bill ya maji au umeme ni mwendo wa kuteleza
 
Shida ni moja, tunapenda sana kudeka kwa kutumia mifuko ya wengine.

Haya mambo ya kuja mjini umefunga safari tena ya ghafla halafu unataka mtu akukirimu ni aina nyingine ya uchawi tu.

Yaani hapo mtu anaoigia picha kuwa atakuja kukaa kwako miezi kadhaa na atakuwa akila bata 24/7. Kama mtu hajakualika usijipendekeze kutokea bila ridhaa.
 
Hawakufanya vizuri. Popote mtu anapoenda iwe mjini au kijijini kutoa taarifa ni jambo jema. Unawapa wenyeji wako muda wamapokezi mazuri. Binafsi sijawai kukutwa na scenario ya hivi. Sipati picha mlikasirika kiasi gani. Na ukute fridge liko empty kabisa.
Acha tu Mkuu.
Tukaanza kuhangaika kutafuta cha kupika😂
Imagine mtu toka ameanza safari, yupo kimyaa..
Anakuja kukutafuta usiku.. hata namba walikuwa hawana, wakaanza kumuomba mama.
Tunashangaa namba ngeni msg inaingia "Tupo Kibaha tunakuja"
Hajasema ni nani,
Hajaeleza tena chochote..

Ndio kuanza kuuliza tuje kuwapokea?
Wanasema Ndiyo.

Sisi tuliwapokea Kwa moyo kabisa na siku zote tuliwasaidia sana hadi wanaondoka..
Nadhani walivyoondoka walijijudge wenyewe.
Siku ya kuondoka wakasema tutakuja tena tutawakuta..
Sasahivi simu zinapigwa, msg za salamu... Naona wamejifunza kuandaa mazingira tena.
 
CCM nawatakia usiku mwemaa
1698777098627.jpg
 
Back
Top Bottom