Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Watu wengi wanaoishi Dar es salaam wakipigiwa simu na ndugu zao wa mikoani, hawataki kusema ugumu wa maisha ulioko Dar es salaam badala yake wanasifu uzuri wa jiji na raha zilizoko kwenye jiji hilo namba moja nchini Tanzania. Kupelekea kuwafanya na ndugu walioko mikoani kutaka kufunga safari wakihisi Dar es salaam kuna maisha raha mstarehe.
Ndugu hao wakishafunga safari na kufika stand ya mabasi Magufuli basi wanatelekezwa, na hao ndugu zao wa Dar uwazimia simu. Jambo ambalo limesababisha watu wengi wa mitaani kuongezeka jijini, ambapo kwa siku stand ya Magufuli upokea makumi ya watu waiokuwa na pa kwenda miongoni mwao ni hao waliotelekezwa na ndugu zao.
Kama uwezi kuwa mwenyeji wa mtu, si bora umwambie tu, atafute alternative kuliko kumtia moyo ya kuja kuishi Dar es salaam na kisha kumtelekeza. Kama maisha yamekuchapa, mwambie tu ukweli kwamba maisha yangu hayako sawa. Hili abaki mkoani, kuliko kujichanga nauli alafu unamtupa stand.