Watu wa Arusha tuache mambo ya kibaguzi na kikabila

Watu wa Arusha tuache mambo ya kibaguzi na kikabila

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,314
Reaction score
43,918
Ninaandika hii post kwa masikitiko na hasira baada ya kusoma mtandaoni post za mwandishi maarufu kwa jina la Zungu kutokea mkoani Arusha. Kwenye machapisho yake kaonekana kukerwa na kumshambulia mtu mwingine anayetumia jina la MATEJOO kwenye utambulisho wake, wenyewe wanasema kuji-brand. Ikumbukwe huyu Zungu ni mtu ambaye amekuwa akitumia jina la mtaa wa MATEJOO kama utambulisho wake.

Kwangu mimi sioni tatizo mtu kutumia jina la sehemu alipozaliwa kujitambulisha.. Kwa mfano akitajwa Babalevo moja kwa moja jina la KIGOMA litakujia. Wengine ambao wakitajwa yatakujia jina la maeneo yao ni Diamond (TANDALE), Yericko Nyerere (MBUTU BLOCK E), na Afande Sele (MORO). Tatizo ni pale kina Zungu na vijana wengine wa Arusha kuporomosha kashfa na maneno mengine ya kuvunjiana heshima kwa wale ambao hawakuzaliwa na kukulia Arusha. Ni ujinga mtupu unaoashiria ubaguzi na ukabila. Kina Zungu hawana tofauti na wazulu wa Xenophobia.

Hii akili kama ya kina Zungu ndo imesababisha Arusha tuwe na wabunge wasio wazawa wa Arusha kuanzia Lema na waliomfuatia hadi leo. Hata Meya wa Arusha sio mzawa wa pale. Huu ukabila ni tatizo. Nakumbuka kwenye uchaguzi wa UVCCM pia kulikuwa na mambo ya ukabila.

Ninawasihi Zungu na wengine wenye mambo ya kibaguzi kuacha mara moja. Badae mtaanza kubaguana kwa kuona waliozaliwa Matejoo ni bora kuliko wa Kaloleni au Njiro. Pia watu wa Arusha tupambane kupata maendeleo na sio huu upuuzi wa ukabila na ubaguzi. Huko Matejoo nadhani ndo makao makuu ya gongo Tanzania. Sijawahi kuona sehemu kunauzwa gongo kama tejo. Hta Dadii pia ndo maskani kwake. Matejoo, Ngarenaro, Unga Ltd yote, Daraja mbili hadi Sinoni kunanuka umaskini uliokithiri. Eti Nako2nako wanaiita Kaloleni, Bronx ambapo kuna hadi nyumba za udongo.
 
Kwenye hili kuna ukweli, nimeishi Arusha over 10 yrs, si wote ila vijana wengi wa hiyo mitaa wana “usela mavi“ uliopindukia, ukitaka kuamini subiri muda kidogo utawaona hapa.
 
Kwenye hili kuna ukweli, nimeishi Arusha over 10 yrs, si wote ila vijana wengi wa hiyo mitaa wana “usela mavi“ uliopindukia, ukitaka kuamini subiri muda kidogo utawaona hapa.
Usela mavi limekuwa janga la Arusha. Aliyekuwa mbunge wa Arumeru mashariki kupitia CHADEMA enzi hizo alidai iwepo jamhuri ya kaskazini.. yaani ujinga mtupu.
 
Huyo Yericko nae ni wa kutolea mfano? Au kwakuwa ni chawa mwenzio lazima umtaje? Matacore yako
 
Huyo Yericko nae ni wa kutolea mfano? Au kwakuwa ni chawa mwenzio lazima umtaje? Matacore yako
Jifunze kujiheshimu. Hakuna haja ya kuandika comment zenye matusi mtandaoni hapa JF. Kwa hii comment yako umedhihirisha kabisa wewe ni K♡ma.
 
Jifunze kujiheshimu. Hakuna haja ya kuandika comment zenye matusi mtandaoni hapa JF. Kwa hii comment yako umedhihirisha kabisa wewe ni K♡ma.
Kati ya mimi na wewe nani kaandika tusi kubwa? Matacore yako once again and again
 
Back
Top Bottom