Watoto wa vigogo na upendeleo wa ajira nyeti serikalini

Mwanakijiji,

Hivi ni lini hizo nafasi za kazi hapo BOT zilitangazwa japo magazetini ili watanzania wote wazione au ndiyo kupachikana tu ati kwa sababu baba ni waziri?.
Hivi kuna mtu anaweza kutuletea titles za hawa watoto hapo BOT ili tulinganishe education,experience zao na hizo position? maana kama ni wafagiaji au ni majanitors nafikiri wanaweza kuwa wanaqualify.
Halafu kuna huyu mtoto wa Makama anaitwa January Makamba ambaye mara tu baada ya kumaliza shule kapata kazi IKULU sasa hizo kazi
ni nani anawapatia? na kuna utaratibu gani unatumika kuwaajili hawa watoto ili tujue kuwa qualifications ni kuwa mtoto wa mkubwa tu!! au la?

-Wembe

Wewe hiyo kazi ulitaka apate nani sasa...?
 
mzee ES..........

kula 5 kaka.

mie naona kwa mtazamo wangu hii sio bandiko la kukaa kupoteza muda kuliongelea sioni lolote la maana hapa. kama wao wanafanya kazi huko ktk makampuni na ofisi nzito nzito na mie na wewe na wengine tuchakarike tutafute mbinu na sisi tuingie.
unajua tuchukulie mfano,wakati watoto wa wakubwa wakiomba kazi sehemu kama BoT,VODA,TRA etc,akina sisi watoto tunaojifanya wa mjini those days ndio tulikuwa bizi kinoma kutafuta I-20 kuelekea USA etc hata pengine zile I-20 nyengine zilikuwa za ulalamishi tu,so kwa maana hiyo tusilalamike tukawa tunawaonea choyo.
walokuwepo ULAYA etc basi na wao watese kivyao na hawa watoto wa VIGOGO tuwaache na wao watese kivyao haina haja kuoneana choyo ohhh eti amejiriwa vipi etc.

kama leo hii mfano sisi sote member wa JF tukiulizana humu njia tulotumia mpaka wengine wakafika USA,CANADA,UK,AUSTRALIA etc naamini hakuna hata mmoja wetu atakaesema ukweli tutabakia ohhh mie nilipata visa hivi ,vile etc,lakini ukweli 90% waliondoka kwa njia za KITAPELI TAPELI tu utasikia alishiriki ktk kazi za kanisa alivyofika USA amezamia na mengi mengine,humu kuna waloondoka kwa njia za SKAUTI those days yote yanajulikana hayo,kwani tunajuana vijana hu ndio ukweli.

leo hii kama tukiulizana zile skolaships tulosoma either UDSM au wengine walobahatika kwenda nje ya nchi,tumezipata vipi,basi naamini 95% yetu tulipigiwa simu tukaambiwa lete vyeti vyako after 2wks safari,huo ndio ukweli tusiwe tunadanganyana humu.

wachache sana walopitia ktk mchujo heavy lkn wengi wetu tumebebana tu either una mtu unamjua na mambo kama hayo.

HITIMISHO...........

Kama ni haya ya kweli basi tuwaache na wao hata kama wamepitishwa na wazee wao,kwani mie dini yangu inasema kuwa "SADAKA SIKU ZOTE HUANZIA NYUMBANI" unaanza kumsaidia wa damu yako kwanza then unasaidia wengine,so sijaona la ajabu lolote hapo watoto wa WAKUBWA kufanya kazi sehemu zenye vipato na msalahi makubwa makubwa.

tumezoea kila siku kulalamika,leo hii kama mtoto wa mkubwa fulani labda jina lake ABC angekuwa M**** ji kama nini, anatembea na wake za watu basi tungepiga kelele weee mpaka tukachoka,angekuwa labda MLAJI UNGA maarufu pale KARIAKOO same tungelalamika tu,lakini kwa nini hatuwapi BIG UP with BIG HUGS vigogo waliopo serikalini kuwaachukua watoto wao wakaajiriwa huko? mie,wewe yule na mwengineo yoyote yule kama tumesoma kweli na sisi tujaribu bahati zetu na sio kukaa KULALAMIKA TU.

usiku mwema
.
 
Eng MOHAMED KULA KUMI KABISA:::

1)Kwanza tunalalamika kweli ila hizi nafasi wanazitangaza kama kawaida kwenye magazeti na wanomba norma process tatizo kwenye kupata ,

2)swala la kupata kazi jamani hii isiwe tabu hakuna asiejua kila shirika tukiingia hivi sasa tanzania kuna mtoto/ndugu/rafiki ama wa CEO, HR,Ama manager wa kitengo fulani,,hii ni kuwekana tu wazi wana apolo,

3))Kama wamekula shule na vyeti vinalipa jamani mnataka wakachongeshe pale BILLICANAS mje kulalamika wamefoji,,kebee kama wana vyeti halali wapeni,,swala la kupata kila mtu anatakiwa atumie njia binafsi jinsii ya kupata kazi,,kama huna mjomba mwombe mungu akupe ;;

4)))Mi nawapongeza hawa watu maana niilijaribu kupitia baadhi yao nkapata dondoo wengi wamekula shule nje ya nchi ,,hapa usiwalalamikie wao,,hizi ni neema za wazazi wao waliokumbuka shule kwanza kabla ya kujaza magorofa pale masaki,,je jamani nyie bandugu kama wamekula shule za wakabahatika kumaliza MLITAKA WAJILIPUE USA,AU UK, kama wengine waliousaliti utanzania na mpaka sasa wanafikiria jinsi ya kuja kwenye nchi ya mamayao,????hongereni walioamua kurudi na nyie mliongangani kubaki huko jamani njooni basi wengine waende ,,,maana siku hizi kama una jina PREDESHEE MWANAKIJIJI,,wanaangalia kuna wanavijiji wangapi uko na je unafaa kuongezeka???hivyo wasaidien jamani kwa kupishana tunajua wengine wana hamu ya kuja uku tatizo ni nauli weka tu a/c hapa mwanakijiji tusaide wenzetu hawa warudi kwao,,,mnaonaje tuanzishe mada ya "MTARUDI LINI"???
 
Inachekesha sana kuona kuwa watu wanajaribu kutoa mifano ya US na Tanzania, Eti mtoto wa Myers amewekwa kwenye nafasi ambayo hailingani na sifa zake. Do we really care about US? Hata kama ni vibaya, ina maana vibaya vya US vinatakiwa kufuatwa na Tanzania?
Tatizo ni kwamba viongozi wetu wanajaribu kupreach kuwa Tanzania kuna haki, lakini hiyo haki inaonekana kutendeka zaidi kwa wakubwa na familia zao, BOT ni mfano mzuri, kuna wengi wenye sifa wameachwa na wasio na sifa za kutosha wamepewa nafasi hili ndio tatizo, kwa hiyo kusema hao si watanzania hiyo sio hoja. Uwezo na sifa ni hoja, kwa hiyo kama wana sifa why not, na kama hawanasifa na kuna wenye sifa zaidi yao, hapo ndio kwanini inakuja.
LAKINI WAKATI MWINGINE TUNAKUWA WAJINGA WENYEWE, wewe ambaye sio Kigogo au Mtoto wa Kigogo, au in short kapuku kama mimi, UNGEUA YULE DEREVA WA DALADALA kama Dito sasa hivi ungekuwa umeuawa au kuwa gerezani, LAKINI DITO anapeta, lazima tuwe realists jamani, TANZANIA MNYONGE HANA HAKI, huo ndio ukweli, hata tufanye nini tutaendelea kuwa wanyonge tu!
 
Haki itakuja tendeka tukifikia hatua kama ya Kenya, ambapo watu watakuwa wamchoka, ndipo wanaovunja haki watakaposhughulikiwa, siku hiyo itafika tu. I have no doubt!
 
Sielekei kufikiri kuwa kuyachambua na kuyajadili majina,matendo ya hawa 'watoto wa wakubwa'ndani ya JF kuhusu tenda wazipatazo serikalini,nk kutabadili mienendo,au utaratibu mzima wa utangazaji,utoaji wa tenda hizo,nafasi za kazi, bali hii itakuwa ni kuwaeleza watu tu kile wanacho hitaji kusikia.
Kwa namna moja ua nyingine tumewachagua sisi wenyewe 'Watawala hawa',watufanyiye mipango, maamuzi ili kunyambua maisha ya mtanzania wa kawaida.Ila mipango hii na maamuzi hayo hubaki kuwa SIRI kubwa kwa Watawala hawa ndani ya nafasi zao za uongozi,na wamejenga Ngome nzito kuzilinda SIRI hizi kutojulikana kwa watanzania wa kawaida,mf. mie najua asilimia 2tu ya SIRI hizo,sijui nyie wenzangu?Leo hii tunaona Ngome hiyo inavyo imarishwa na 'watoto wa watawala' hao,Scholarships,wanafunga harusi wenyewe kwa wenyewe,tenda za serikalini,nafasi nyeti makazini,na mbali ya hayo yote C.V zao zinapendeza mnooo!!haswa swali langu mimi ni je:TUFANYEJE ILI TUPENYEZE KTK NGOME HII ILI NASI 'TUJUE' WALAU ASILIMIA 50 YA SIRI HIZI??? SIYO 'KUSIKIA' TU!!!
**kumbuka ndege wenye mbawa za kufanana huruka pamoja.
 
PAMELLA LOWASSA
FILBERT SUMAYE
ZALIA KAWAWA
HARIETH LUMBANGA
SALAMA ALI MWINYI
RACHEL MUGANDA
SLVIA OMAR MAHITA
JUSTINA MUNGAI
KENNETH JOHN NCHIMBI
LIKU IRENE KATTE KAMBA
THOMAS MONGELLA
JABIR ABDALLAH KIGODA
VIOLETH PHILLEMON LUHANJO
KENNEDH JOHN NCHIMBI
BLASSIUS WILLIAM MKAPA

Jibu ni moja tu;hakuna hata mmoja wapo aliyesomea UDSM!! kaka hamna jungu hapo,CV zao ni nzito mnoo ehh!!
 
Inachekesha sana kuona kuwa watu wanajaribu kutoa mifano ya US na Tanzania, Eti mtoto wa Myers amewekwa kwenye nafasi ambayo hailingani na sifa zake. Do we really care about US? Hata kama ni vibaya, ina maana vibaya vya US vinatakiwa kufuatwa na Tanzania?
Tatizo ni kwamba viongozi wetu wanajaribu kupreach kuwa Tanzania kuna haki, lakini hiyo haki inaonekana kutendeka zaidi kwa wakubwa na familia zao, BOT ni mfano mzuri, kuna wengi wenye sifa wameachwa na wasio na sifa za kutosha wamepewa nafasi hili ndio tatizo, kwa hiyo kusema hao si watanzania hiyo sio hoja. Uwezo na sifa ni hoja, kwa hiyo kama wana sifa why not, na kama hawanasifa na kuna wenye sifa zaidi yao, hapo ndio kwanini inakuja.
LAKINI WAKATI MWINGINE TUNAKUWA WAJINGA WENYEWE, wewe ambaye sio Kigogo au Mtoto wa Kigogo, au in short kapuku kama mimi, UNGEUA YULE DEREVA WA DALADALA kama Dito sasa hivi ungekuwa umeuawa au kuwa gerezani, LAKINI DITO anapeta, lazima tuwe realists jamani, TANZANIA MNYONGE HANA HAKI, huo ndio ukweli, hata tufanye nini tutaendelea kuwa wanyonge tu!

Sikiliza weye...kuna kajitu kaliomba mfano ndio nikatoa jina Myers...sikuona popote pale mtu alipolinganisha kati ya Tanzania na Marekani. Punguza spidi dogo usije ukashikishwa ukuta bure....ooohooooo
 
Quote:-

"Halafu kuna huyu mtoto wa Makama anaitwa January Makamba ambaye mara tu baada ya kumaliza shule kapata kazi IKULU sasa sijui kuna utaratibu gani unatumika kuwaajili hawa watoto ili tujue kuwa qualifications ni kuwa mtoto wa mkubwa tu!! au la?"

January Makamba, alimaliza Masters Boston, akarudi bongo akasota mpaka alipopata his way kwenye kampeni ya urais wa Kikwete, akiwa tayari ameshaajiriwa foreign, kwenye hilo hakuwa peke yake kuna watoto wengi wa wananchi wa kawaida walioshiriki kwenye kampeni za urais, maan Mzee Makamba hana huo utajiri kabisaa,

Baada ya kampeni kuisha rais binafsi aakamua kuwa anamuhitaji kutokana na ku-prove kuwa anaiweza kazi yake ya kumtayarishia hotuba na kuzisahihisha kwa kasi ya haraka sana, mind you kuna wengine wengi walipoewa hiyo nafasi wakahsindwa na ninawajua kwa majina, lakini Kikwete akawa mstaarabu akaishia kuwapa nafasi kama kwenye balozi zetu, lakini hakuwatupa tu kama mbwa!

Besides, nafasi za kazi za Butiku na Apiyo, zilikuwa uamuazi wa rais ambaye pia anaruhusiwa kisheria kuchagua wasaidizi wake na kwa sababu anazozijua mwenyewe period, sifa zote za Mwalimu in part zilikuwa zinatengenezwa na hawa kina Butiku, labda utolewe mfano mwingine huu wa Januari Mkamba kuwa msaidizi wa rais na kufanya kazi yake ipasavyo nakuwashinda wengine watoto wa wananchi wa kawaida, samahani kwamba kwa maoni yangu haujitoshelezi kukidhi matakwa ya hii hoja ya msingi kwenye hii topic!

Mnyonge Mnyongeni, lakini kama kawaida ya JF huwa tunatoa haki kwanza!
 
Wakuu hebu tuwekeeni nafasi zao huko BOT tuone hapa kama ni kweli walipewa tu, tusiendelee kuanidkia mate na wino upo, wekeni nafasi zao huko BOT tuone kama kuna waliopewa tu!

Kurushiana maneno bila fatcs, sio ustaarabu na inaondoa utamu wa topic tuweke facts!
 
mzee ES..........

kula 5 kaka.

mie naona kwa mtazamo wangu hii sio bandiko la kukaa kupoteza muda kuliongelea sioni lolote la maana hapa. kama wao wanafanya kazi huko ktk makampuni na ofisi nzito nzito na mie na wewe na wengine tuchakarike tutafute mbinu na sisi tuingie.
unajua tuchukulie mfano,wakati watoto wa wakubwa wakiomba kazi sehemu kama BoT,VODA,TRA etc,akina sisi watoto tunaojifanya wa mjini those days ndio tulikuwa bizi kinoma kutafuta I-20 kuelekea USA etc hata pengine zile I-20 nyengine zilikuwa za ulalamishi tu,so kwa maana hiyo tusilalamike tukawa tunawaonea choyo.
walokuwepo ULAYA etc basi na wao watese kivyao na hawa watoto wa VIGOGO tuwaache na wao watese kivyao haina haja kuoneana choyo ohhh eti amejiriwa vipi etc.

kama leo hii mfano sisi sote member wa JF tukiulizana humu njia tulotumia mpaka wengine wakafika USA,CANADA,UK,AUSTRALIA etc naamini hakuna hata mmoja wetu atakaesema ukweli tutabakia ohhh mie nilipata visa hivi ,vile etc,lakini ukweli 90% waliondoka kwa njia za KITAPELI TAPELI tu utasikia alishiriki ktk kazi za kanisa alivyofika USA amezamia na mengi mengine,humu kuna waloondoka kwa njia za SKAUTI those days yote yanajulikana hayo,kwani tunajuana vijana hu ndio ukweli.

leo hii kama tukiulizana zile skolaships tulosoma either UDSM au wengine walobahatika kwenda nje ya nchi,tumezipata vipi,basi naamini 95% yetu tulipigiwa simu tukaambiwa lete vyeti vyako after 2wks safari,huo ndio ukweli tusiwe tunadanganyana humu.

wachache sana walopitia ktk mchujo heavy lkn wengi wetu tumebebana tu either una mtu unamjua na mambo kama hayo.

HITIMISHO...........

Kama ni haya ya kweli basi tuwaache na wao hata kama wamepitishwa na wazee wao,kwani mie dini yangu inasema kuwa "SADAKA SIKU ZOTE HUANZIA NYUMBANI" unaanza kumsaidia wa damu yako kwanza then unasaidia wengine,so sijaona la ajabu lolote hapo watoto wa WAKUBWA kufanya kazi sehemu zenye vipato na msalahi makubwa makubwa.

tumezoea kila siku kulalamika,leo hii kama mtoto wa mkubwa fulani labda jina lake ABC angekuwa M**** ji kama nini, anatembea na wake za watu basi tungepiga kelele weee mpaka tukachoka,angekuwa labda MLAJI UNGA maarufu pale KARIAKOO same tungelalamika tu,lakini kwa nini hatuwapi BIG UP with BIG HUGS vigogo waliopo serikalini kuwaachukua watoto wao wakaajiriwa huko? mie,wewe yule na mwengineo yoyote yule kama tumesoma kweli na sisi tujaribu bahati zetu na sio kukaa KULALAMIKA TU.

usiku mwema
.

This is the damn and crazy replied i ever see in my entire life. Wewe unadhani ni Watanzania wangapi wako US and EU? Jeee wanamake percante ngapi ya watanzania wote? Hawa watoto wa so called vigogo wana qualification za kutosha? That is the only question that every one need to know. I know personal watoto wa kigogo wamekuja US wamesoma degree zao za kuunga unga kisha wamerudi bongo na wako BOT. Labda nikuulize swali " Jee Unajua kazi za Bank Kuu?.

Majority yetu hatujui implication ya bank kuu in country economy, na hili limesababisha watu kufungua midomo yao pasipo kujua nini wanaongea.
Bank kuu wameweka requirement ya graduate school degree, so kama mtu amemaliza form four na yupo kazini what u think? Does it need to attend MIT to figure out? or Does it need to be a NASA scientist to solve the puzzle?

Labda let me brief wale wasio jua nini maana ya bank kuu. I will speak from big picture, sababu we cant get into details hapa.

Bank kuu ndio chombo kinacho simamia fedha ndani ya nchi. Sasa usimamiaji wa fedha kwa ufasaha unasababisha kupunguza mlipuko wa bei yaani Inflation, kupunguza idadi ya watu wasio na kazi (unemployment rate), kucontrol riba na kuchanyata muongezeko wa uchumi na N.K

Sasa basi, kama bank kuu imejaa vilaza ambao wako pale kutokana na migongo ya baba zao, then nini matatizo yake. Kwanza, kufanya maamuzi kutokana na influance za wanasiasa (baba zao). Madhara yake ni kuprint more money, which will increase supply of the money in the system, which have effect on inflation, which will cause interest rate to rise, rises of interest rate will reduce investors desire to borrow more money for new investements, which will cause increase in unemployment. Sasa hilo ni tatizo moja tuu, kuongeza pesa kwenye mzunguko.

Alan Greenspan alisema siku moja, " Nchi za dunia ya tatu haziwezi kuendelea sababu Bank kuu zao hazijetegemei zenyewe". Meaning the central bank is not independent, yaani waziri wa fedha ana influance, raisi ana influance, watoto wao wana influance, sasa what do u think?

Bank kuu ndio msimamizi wa uchumi mzima wa nchi, bank kuu inaitaji watu wenye vichwa vya uchimu na upeo mkubwa sana wa finance, na sio mbumbumbu walio weka picha zao hi5.com wakiwa wamevaa gun pocket. Labda tuanzishe mdahalo utakaojulikana Monetery Policy, then wasiojua ni nini bank kuu will be able to see what is real responsibility of central bank.
 
Mtanganyika,
I like the word "Kilaza" i once used it while was at college.
Well from the Bigger pic... naona kweli we need to see through what is happening at BOT.
Kama hawa hawa watoto wa wakubwa wameingia ktk sehemu nyeti km hiyo bila kujali wana qualifications zipi i see a weakness in the whole system... na nakusapport unaposema Central Banks hazina uwezo wa kujitemea ktk Afrika.
Mimi ningependa kujua apart from the list of name can we add another column may be two na tupate qualification and positions these guys hold at BOT?

Ni hayo tu... truth will always prevail
 
FMES asante kwa ufafanuzi, kwa hiyo ile DVD ya hotuba aliandaa January! mh! na Salva alishindwa kutwambia kuwa wale wageni walioanguka na helikopta walikuwa wageni wa mzee. Hivi tanzania hatuwezi kupata watu kama Tareq Aziz na Dr.Alfred Mutua?
 
Mimi namfahamu mmoja ya hawa watoto wa vigogo wanaofanya kazi benki kuu.Na nakumbuka jinsi alivyo apply,kukimbizia kila siku,physically na kupiga simu mpaka akapata kitu kama miezi 3 baadae.Nakumbuka furaha aliyokuwa nayo siku alipopata taarifa kuwa kapata hio kazi.Ana qualifications za kutosha na anastahili hio kazi,huyo ni mmoja ninayemjua mimi,siwezi kuwasemea wengine.
Miaka ya themanini,mtoto mmoja wa Mwalimu aliamua kuacha kazi ya maana sana Tanesco(alisomea ectrical engineering,na alikuwa kinara sana chu) na kurudi kijijini kwao kusaidia kukijenga kile kijiji,(according to him)Leo hii yule bwana kama angekuwa bado yuko Tanesco angekuwa ni director,nasikia sasa hivi haieleweki hata anafanya nini huko kijijini kwao.Sasa sijui tunataka na hawa nao warudi vijijini...Nani hapa ambaye kweli hatamsaidia mwanawe kupata kazi sehemu ambayo yeye anajua ataweza kufanikiwa.Yaani leo nimsomeshe mwanangu,then kuna oppurtunity ya kumuweka Benki Kuu kwa sababu namjua mtu pale niache kwa sababu watu watasema...shiiiii!Hii sio kwa watoto wa vigogo tu,hata hao wa walalahoi nao wanapata kazi hivyohivyo,mifano ipo mingi tu.Hapa kuna shangazi,hapa kuna rafiki yake mama,baba..hapa kuna kaka,shemeji and so forth.
 
Jamani hili swala hapa ni tete na linatouch nerves za wengi. Lakini wengi naona tunaweka majibu mepesi kwa hoja nzito.

Napenda kuwaasa watanzania wenzangu, Kenya kwa sasa wanavuna wazee wao akina Kenyatta, Moi, na wengineo walichopanda walipokuwa kwenye nafasi. Ukabila ambao ulianza mwaka 1963 baada ya uhuru kwa watu fulani kuwasaidia ndugu zao, ndo matokeo yake tunayaona leo, at the end of the day majority wana feel defranchized katika mikondo yote ya uchumi wa nchi yao! Ni kwa sababu watu wenye nafasi walikuwa "wanawasaidia" ndugu zao-after all si walikuwa na vyeti? hivyo hivyo tunavyoona leo nchini kwetu.

Kuwapa ajira watoto wa vigogo BOT, Ikulu, Tanesco, TRA nk sio hoja kubwa sana kwa kuangalia kwamba watu wana visomo stahiki, lakini tunaset bad precedent, wakina Kalumanzira wa Kasulu na Ludewa ambao watafeel kwamba wako alianated kwa mda mrefu, watakapo amua kudai haki yao, Tanzania haitakalika. KAMA MTANGANYIKA ALIVYOSEMA, LET US LOOK AT THINGS IN A BIGGER PICTURE. Personally najua wengi walio BOT wamesoma lakini wako pale kwa influence ya wazazi wao. Hilo halipingiki. Na ukweli ni kwamba sio kazi zote za BOT zinatangazwa rather wanasema kwamba wana "pool" ya CV ambako wanachagua humo! How do I get in that pool, mi sijui!

Tatizo hapo ni mfumo wa viongozi wetu ambao hauangalii longterm impact ya kuajiri mtoto wa Sumaye, Rupiya, Lowassa, Lumbanga, Mkapa sehemu moja nyeti kama hiyo (maana kwa nchi zetu maskini BOT ndo sehemu kila mtu anaangalia! Hata mjinga lazima ata raise eyebrows!

Well, haraka haraka tukiangalia vyeti watoto hawa wamepata opportunity za kusoma nje na kwingineko, lakini je, is what we are doing good for the Tanzania ya miaka ishirini ijayo?

Kenya nadhani imetupa fundisho kwamba hasira za wananchi zikifikia peak, madhara yake ni makubwa mno. Nyerere angeamua watoto wake leo wangekuwa wameshika nafasi nyeti za uongozi Tanzania! But the old man, aliangalia maslahi ya Tanzania ya miaka mia moja mbele.

Tuache majibu mepesi kwa hoja zinazohitaji kufikiri kwa kina. Kikwete kumuajiri mtoto wa Makamba Ikulu, haina tatizo, lakini raisi wetu angeangalia bigger picture angelijua hili kwamba at one point in time, watu wataliquestion. Jamani msisahau kwenye nchi yetu ina watu million arobaini!!!

Unafikir Koffi Anan alipowashiwa moto wa mtoto wake kupewa tenda UN ilikuwa bure? hata kama Kofi alikuwa hajui na mwanawe alikuwa na qualifications husika, lakini the mere fact kwamba mzee ni boss, inaleta hisia tofauti!

All I can say is, tunachokifanya leo, hatuwezi kujua madhara yake in 50 years to come. Tuwe wepesi wa kusoma alama za nyakatina sio kung`ang`ania majibu ambayo hayatufikish popote. Tanzania tumefika hapa tulipo kwa kuwajali na kuwaona akina Kalumanzira kama raia halisi kama akina Mkapa na Lowassa. Hii amani ipo kwa sababu watu wanavumilia, lakini tusiuchukulie huo uvumilivu for granted! Watu wanafikiria na wanaona, sio wajinga as the elite tend to think and believe.
 
Mimi binafsi ningefurahi kama hawa watoto wangepewa ukatibu tarafa kibondo ili wajue hali halisi ya watanzania ambayo na hakika wengi wao hawaijui maana wamekuwa coddled tangu wadogo. Ningekuwa kigogo, ningempeleka mwanangu huko kwa angalau mwaka mmoja ili hapo atakapokuja kunirithi aelewe anaowaongoza wakilia njaa maana yake nini! Wamarekani wamevuna waliyoyapanda walipomchagua Bush W. Huyu na mama yake hawakuweza kuelewa machungu ya walioarithiwa na Katrina. Clinton aliyetoka ukoo maskini(relatively) anaheshimika kwa watu weusi na wengine wasio na kipato kwa maana anaelewa njaa yao! Sasa hawa watoto waliolelewa Masaki au Toronto, kusomea International School, University Havard shida ya mTanzania kwao itakuwa academic. Na hawa ndio watakaoachiwa nchi. Masanja yuko sahihi, tusiwe flippant kwenye hili, tutakuja juta.
 
This is the damn and crazy replied i ever see in my entire life. Wewe unadhani ni Watanzania wangapi wako US and EU? Jeee wanamake percante ngapi ya watanzania wote? Hawa watoto wa so called vigogo wana qualification za kutosha? That is the only question that every one need to know. I know personal watoto wa kigogo wamekuja US wamesoma degree zao za kuunga unga kisha wamerudi bongo na wako BOT. Labda nikuulize swali " Jee Unajua kazi za Bank Kuu?.

Majority yetu hatujui implication ya bank kuu in country economy, na hili limesababisha watu kufungua midomo yao pasipo kujua nini wanaongea.
Bank kuu wameweka requirement ya graduate school degree, so kama mtu amemaliza form four na yupo kazini what u think? Does it need to attend MIT to figure out? or Does it need to be a NASA scientist to solve the puzzle?

Labda let me brief wale wasio jua nini maana ya bank kuu. I will speak from big picture, sababu we cant get into details hapa.

Bank kuu ndio chombo kinacho simamia fedha ndani ya nchi. Sasa usimamiaji wa fedha kwa ufasaha unasababisha kupunguza mlipuko wa bei yaani Inflation, kupunguza idadi ya watu wasio na kazi (unemployment rate), kucontrol riba na kuchanyata muongezeko wa uchumi na N.K

Sasa basi, kama bank kuu imejaa vilaza ambao wako pale kutokana na migongo ya baba zao, then nini matatizo yake. Kwanza, kufanya maamuzi kutokana na influance za wanasiasa (baba zao). Madhara yake ni kuprint more money, which will increase supply of the money in the system, which have effect on inflation, which will cause interest rate to rise, rises of interest rate will reduce investors desire to borrow more money for new investements, which will cause increase in unemployment. Sasa hilo ni tatizo moja tuu, kuongeza pesa kwenye mzunguko.

Alan Greenspan alisema siku moja, " Nchi za dunia ya tatu haziwezi kuendelea sababu Bank kuu zao hazijetegemei zenyewe". Meaning the central bank is not independent, yaani waziri wa fedha ana influance, raisi ana influance, watoto wao wana influance, sasa what do u think?

Bank kuu ndio msimamizi wa uchumi mzima wa nchi, bank kuu inaitaji watu wenye vichwa vya uchimu na upeo mkubwa sana wa finance, na sio mbumbumbu walio weka picha zao hi5.com wakiwa wamevaa gun pocket. Labda tuanzishe mdahalo utakaojulikana Monetery Policy, then wasiojua ni nini bank kuu will be able to see what is real responsibility of central bank.

mDANganYIka.....sorry my PC key board T imekufa

wewe tatizo lako una choyo ndani ya roho ya roho yako ndio kinachokuumiza.

wakati watoto wa vigogo wanasota pale BoT kufanya kazi,sisi tulikuwa resi kali kutafuta I-20 mbona unakimbia hiyo point.

hivi huko BoT hao watoto wote wa vigogo sifikirii kama wana post kubwa kubwa naamini nafasi zao kawaida tu.

labda tupate list ya staffs wote wa BoT HQ na job descriptions zao ndio tutaweza kujua JEE WANASTAHIKI ama Lah,otherwise HAKUNA CHA KUJADILI HAPA.
 
Hapa mDanganyika nani? Unaamini wote walio nje walienda kwa hizo 1-20? Speak for yourself, my brada! Nani amekuambia kuna kusota BOT? Au TRA? Wangekuwa redio Tanzania, labda. BOT hakuna msoto kwa hali ya Tanzania! Pale hata mesenja anapeta. Kama taratibu zilikiukwa katika ajira zao ni lazima pakemewe.
 
Engineer Mohd acha kutokota ktk CHUNGU..si kila alie Nje amekuja kwa I-20, wengine ndo kwanza twasikia kwako au umemezeshwa na wenzako au kuna mshikaji wako pale BOT. mie nashauri nafasi za kazi serikalini zifuate taratibu za KUTANGAZWA na watu wagombee...unaposema eti Mtoto wa kigogo ana qualification alikuwa anafuatilia nafasi miezi 3 ndio kaipata SIO right na sio hoja. Kwanini afuatilie BOT asiende MLIMANI kufundishwa au kufanya kazi kule.(mfano tu).
UTARATIBU Tunaoujenga unaweza kutucost siku za USONI pale ambapo aliedhulumiwa akajua kuwa anadhulumiwa.
Binafsi niliomba nafasi pale BOT ya IT. zilitangazwa. nilipopeleka barua wakasema ohh nyie matokeo yenu bado. Ofcourse matokeo ya Mwaka wa mwisho yalikuwa bado, unajua mnapomaliza UDSM mnatafuta kazi kwa UDI na UVUMBA. lkn mnaruhusiwa kutafuta kazi. Cha AJABU na CHA KUSIKITISHA wapo vijana 2-3 ambao tulikuwa CLASS moja UDSM wao walipata kazi hapo.nikajua anhaaa...kumbe....(PEOPLE ARE NOT INTERESTED WITH YOU, THEY ARE INTERESTED WHO KNOWS YOU)...
 
Back
Top Bottom