Kwanini tunalea kizazi cha watoto ambao hawaguswi na suala la utunzaji wa mazingira?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Nimewiwa kulizungumzia hili, kwa kuwa jamii inaendelea kupoteza kabisa ule mguso wa kimazingira na umuhimu wake katika maisha yao.

Katika ngazi ya familia waathiriwa zaidi ni watoto wetu, Mtoto aambiwi wala kufundishwa kwa vitendo kupanda miti na kuitunza, kupenda wanyama na kuwahudumia wala kutunza nyumba na mazingira yake ikiwemo kupalilia na kufanya usafi.

Inasikitisha kuwa na kizazi ambacho mtoto kila aonapo mti mdogo wenye afya njema uwaza kuuharibu tu kwa kuuchuma kama fimbo kwa kuwa ndicho kitu pekee anachoelewa ni matumizi sahihi ya mti huo iwe ni shuleni au nyumbani daima uagizwa akalete fimbo ili aadhibiwe.

Chakusikitisha ni kuwa watoto hawa wanakuwa wakiwa na ile mentality ya uharibifu wa mazingira ndani yao, kwani mitaani kwao wanakoishi kila siku wanachoshuhudia ni utupaji taka ovyo na uchimbaji mchanga barabarani, matumizi yaliyokithiri ya mkaa, ukataji miti kiholela kupisha maendeleo ya vitu kwani miti na uoto kama nyasi uonekana kama kikwazo cha upitishaji wa huduma za kijamii kama maji na umeme, na pia uoto pekee ni matumizi mabaya ya eneo la ardhi.

Leo hii tunalea kizazi ambacho ukipanda miche yako lazima uwe mwenyewe ndiye mlinzi dhidi ya watoto kwa maana badala ya kuwaofia wanyama, watoto wetu ndiyo janga kuu.

Ukijisahau kidogo tu utakuta mtoto wa watu ashang'oa au kuvunjavunja mashina ya miti yako yuko comfortable kabisa hana wasiwasi anaichezea hapo hapo alipoichumia.

Na chakumfanya huna kwa kuwa watoto hao katika fahamu zao hawatambui hata kama kutenda hivyo ni kosa na wala hata jamii yenyewe haioni ikiwa suala kama hilo lina uzito wowote ule.

Anakuja mtu mzima kukuomba umruhusu achume dawa katika mti mmoja hapo nyumbani kwako, pasipo kusita unamruhusu nenda kachume huku ukiwa hauna shaka yeyote ile unaingia zako ndani, punde anarudi kukushukuru kishamaliza haja zake yeye anaondoka.

Unapotoka kwenda kushuhudia alichokifanya unabaki kutikisa kichwa na kufyonza tu, kwa maana ni uharibifu tu utakuta mtu badala ya kuchuma majani katika tawi kaamua kuondoka na tawi kabisa.

Mwingine yeye ni kudonoa-donoa tu viini vya shina la miti akitafuta majani malaini na amalize haja zake haraka aondoke, wengine atachimba mizizi yote anaacha kisha anakata ule mzizi mkuu ili achukue kipande kidogo tu
na kama haitoshi hata kufukia pia ni mtihani atapaacha jinsi alivyopafukuwa pasipo kujalisha mwendelezo wa uhai wa huo mti utakuaje na kwa bahati mbaya anakuwa pengine kaambatana na mwanaye ambaye anashuhudia namna miti inavyopaswa kutendewa hasa isipokuwa yakwako.

Vijijini hali ni mbaya zaidi, mtoto tokea kukuwa kwake anachoshuhudia jamii yake ikipambana nacho kama adui mkubwa huwa ni miti, vichaka na majani.

Muda wote maadui hao watatu (miti, vichaka na majani) popote pale wanapoonekana huwa wanapaswa kuondoshwa kwa sababu yeyote ile iwe kwa kufyekwa, kukatwa au kuchomwa moto kwa kisingizio cha kujipatia kipato, kuandaa eneo la mashamba, kusafisha mji, kuepuka mbu, wanyama nakadhalika.

Unategemea mtoto wa mchoma mkaa ambaye hajawahi kushuhudia hata mara moja baba yake akipanda mti zaidi ya kuikata na kuichomea mikaa na matofali kesho na kesho kutwa aje kuwa balozi mwema wa mazingira yake.

Tunasahau kuwa vitu vidogo vidogo vinavyoonekana kutokuwa na madhara ndiyo baadae upelekea ufa mkubwa usiozibika.

Kama jamii ni wakati wa kubadilika na kuanza kuyajali mazingira yetu kwa vitendo kwa kuwaelekeza watoto wetu juu ya usahihi wa kutenda kwa kujali miti,vyanzo vya maji na uoto wa asili, kulinda na kutunza mazingira yao ili tuepuke kizazi kijacho kisichokuwa na huruma na mazingira, na mazingira nayo hayatokuwa na huruma nao.
 
Unapoint,
Ila hilo suala usiseme leo, ndivyo ilivyo miaka yote Africa, daima watu wanaamini suala la mazingira haliwahusu, na sio watoto tu ni wote, vijana kwa wazee,

Nadhani kama jamii inabidi tuanze kuelewa mabadiliko ya tabia ya nchi
 
Mi nachoona watoto wetu wavivu sana, tofauti na sisi enzi zetu, wengi kupenda Ela na kufakamia misosi na kuchezea simu, games, ndo wanachoweza sio kujituma kwa majukumu ya nyumbani, Kama kusema unasema unachoka kesho yaleyale tu.
Asilimia kubwa mtoto anajifunza kwa kuiga kile unachotenda mara kwa mara kama mtu mzima.

Haiwezekani wewe ukawa na haiba nzuri na mazingira kisha mwanao asitambue jinsi unavyoithamini miti na kulinda aina ya uoto wowote unaokuzunguka.

Lazima tatizo tunalo sisi wenyewe watu wazima, muda mwingi unautumia kupiga umbeya na stori za mabwana, maokoto na udangaji, kucheza staili mpya za nyimbo na kuwazungumzia celebrities wa mitandaoni n.k huku umeketi na mwanao anashuhudia siyo ajabu naye anachangia mada hizo.

Kwa maisha ya namna hii unapata wapi muda wa kumfundisha mwanao stadi bora za maisha na kufuatilia maendeleo yake ya kitaaluma,kimwenendo na kiakili.

Ikiwa kila akitoka shule ni rimoti mkononi au kishashika touch kaingia zake tik tok au insta anaangalia video za utupu na mashoga, mzazi huna habari na chochote atendacho mwanao kisha unakimbilia kwenye kichaka cha kuepuka lawama, cha watoto wa siku hizi...."
 
Nimewiwa kulizungumzia hili, kwa kuwa jamii inaendelea kupoteza kabisa ule mguso wa kimazingira na umuhimu wake katika maisha yao.

Katika ngazi ya familia waathiriwa zaidi ni watoto wetu, Mtoto aambiwi wala kufundishwa kwa vitendo kupanda miti na kuitunza, kupenda wanyama na kuwahudumia wala kutunza nyumba na mazingira yake ikiwemo kupalilia na kufanya usafi.

Inasikitisha kuwa na kizazi ambacho mtoto kila aonapo mti mdogo wenye afya njema uwaza kuuharibu tu kwa kuuchuma kama fimbo kwa kuwa ndicho kitu pekee anachoelewa ni matumizi sahihi ya mti huo iwe ni shuleni au nyumbani daima uagizwa akalete fimbo ili aadhibiwe.

Chakusikitisha ni kuwa watoto hawa wanakuwa wakiwa na ile mentality ya uharibifu wa mazingira ndani yao, kwani mitaani kwao wanakoishi kila siku wanachoshuhudia ni utupaji taka ovyo na uchimbaji mchanga barabarani, matumizi yaliyokithiri ya mkaa, ukataji miti kiholela kupisha maendeleo ya vitu kwani miti na uoto kama nyasi uonekana kama kikwazo cha upitishaji wa huduma za kijamii kama maji na umeme, na pia uoto pekee ni matumizi mabaya ya eneo la ardhi.

Leo hii tunalea kizazi ambacho ukipanda miche yako lazima uwe mwenyewe ndiye mlinzi dhidi ya watoto kwa maana badala ya kuwaofia wanyama, watoto wetu ndiyo janga kuu.

Ukijisahau kidogo tu utakuta mtoto wa watu ashang'oa au kuvunjavunja mashina ya miti yako yuko comfortable kabisa hana wasiwasi anaichezea hapo hapo alipoichumia.

Na chakumfanya huna kwa kuwa watoto hao katika fahamu zao hawatambui hata kama kutenda hivyo ni kosa na wala hata jamii yenyewe haioni ikiwa suala kama hilo lina uzito wowote ule.

Anakuja mtu mzima kukuomba umruhusu achume dawa katika mti mmoja hapo nyumbani kwako, pasipo kusita unamruhusu nenda kachume huku ukiwa hauna shaka yeyote ile unaingia zako ndani, punde anarudi kukushukuru kishamaliza haja zake yeye anaondoka.

Unapotoka kwenda kushuhudia alichokifanya unabaki kutikisa kichwa na kufyonza tu, kwa maana ni uharibifu tu utakuta mtu badala ya kuchuma majani katika tawi kaamua kuondoka na tawi kabisa.

Mwingine yeye ni kudonoa-donoa tu viini vya shina la miti akitafuta majani malaini na amalize haja zake haraka aondoke, wengine atachimba mizizi yote anaacha kisha anakata ule mzizi mkuu ili achukue kipande kidogo tu
na kama haitoshi hata kufukia pia ni mtihani atapaacha jinsi alivyopafukuwa pasipo kujalisha mwendelezo wa uhai wa huo mti utakuaje na kwa bahati mbaya anakuwa pengine kaambatana na mwanaye ambaye anashuhudia namna miti inavyopaswa kutendewa hasa isipokuwa yakwako.

Vijijini hali ni mbaya zaidi, mtoto tokea kukuwa kwake anachoshuhudia jamii yake ikipambana nacho kama adui mkubwa huwa ni miti, vichaka na majani.

Muda wote maadui hao watatu (miti, vichaka na majani) popote pale wanapoonekana huwa wanapaswa kuondoshwa kwa sababu yeyote ile iwe kwa kufyekwa, kukatwa au kuchomwa moto kwa kisingizio cha kujipatia kipato, kuandaa eneo la mashamba, kusafisha mji, kuepuka mbu, wanyama nakadhalika.

Unategemea mtoto wa mchoma mkaa ambaye hajawahi kushuhudia hata mara moja baba yake akipanda mti zaidi ya kuikata na kuichomea mikaa na matofali kesho na kesho kutwa aje kuwa balozi mwema wa mazingira yake.

Tunasahau kuwa vitu vidogo vidogo vinavyoonekana kutokuwa na madhara ndiyo baadae upelekea ufa mkubwa usiozibika.

Kama jamii ni wakati wa kubadilika na kuanza kuyajali mazingira yetu kwa vitendo kwa kuwaelekeza watoto wetu juu ya usahihi wa kutenda kwa kujali miti,vyanzo vya maji na uoto wa asili, kulinda na kutunza mazingira yao ili tuepuke kizazi kijacho kisichokuwa na huruma na mazingira, na mazingira nayo hayatokuwa na huruma nao.
Juniors generation "Facebook, Telegram, Twitter, Instagram # Utandawazi but Utunduwazi.com"

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Unapoint,
Ila hilo suala usiseme leo, ndivyo ilivyo miaka yote Africa, daima watu wanaamini suala la mazingira haliwahusu, na sio watoto tu ni wote, vijana kwa wazee,

Nadhani kama jamii inabidi tuanze kuelewa mabadiliko ya tabia ya nchi
Na ni kitu ambacho ni basic kabla ya vyote, watu wanapaswa wawe sensitive na mazingira kuliko hata jinsi wanavyothamini kula ila kwa kuwa hatujajengwa kuwa na jamii ya namna hiyo inatuwia vigumu mno waafrika kwa ujumla wake kuelewa kile tunachokitenda na athari zake licha ya wachache kuwa na ufahamu ila huwa tunahisi hayo ni mambo ya muda mrefu au pengine kwa namna moja au nyingine hayatugusi moja kwa moja hivyo cha maana ni kutimiza matakwa yetu ya muda mfupi basi hayo mengine tumwachie Mungu.
 
Kuna shida nyingi sana Tanzania, mpaka ziishe ndo nitawaza mguso kwa watoto wa mazingira.
Unahisi unashida kiasi gani mpaka ushindwe kumkanya na kumpatia elimu mtoto unapokuta akiharibu miti,kuponda mawe ovyo na kutesa wanyama, kuchimbua,kukata au kufungua connecter za mabomba ya maji ili wachezee maji yanayomwagikia ardhini au kuokota taka hatarishi na kuchezea.

Wakati mwingine unakutana na mtoto anachana makaratasi na kuyadondosha kila mahali pasipo kutambua kuwa anachafua mazingira ili nalo linahitaji mpaka uwe vizuri kiuchumi ndipo ulithibiti.

Sasa kwa kuwa hali ni ngumu ndiyo umtwike mwanao rundo la takataka usiku akamwage barabarani?

Je, unashindwa nini kumwelewesha mwanao juu ya athari za kimazingira na kiafya kwa kusikiliza miziki kwa sauti kubwa pale unapokuwepo au usipokuwepo?
 
Shuleni kila mwanafunzi alipewa mti wake autunze kwa kuumwagilia na kuwekea mbolea, nyumbani mzee alileta miti kazi yangu ni kuimwagilia saizi hawapewi labda maeneo ya kupanda miti yamekuwa machache
Na ndicho haswaa tunachokiongelea, kuwa imefikia sehemu jamii kwa ujumla wake imelipa kisogo suala hili kama vile halina umuhimu tena, siyo mashuleni, kiimani au katika malezi.

Suala la mazingira halina kipaumbele tena bali limeachiwa wanasiasa na wahamasishaji wanapotaka ku-gain attention ya watu walitumie kama sehemu ya kuonesha kuguswa nalo wakati matendo yao yakiwasaliti.
 
Nakumbuka nikiwa darasa la sita niling'oa mche wa mti fulani hivi nikaenda kuupanda nyumbani uwanjani. Aisee ni miaka kadhaa sasa kila nikirudi pale nyumbani cha kwanza ni kuuangalia huo mti
Watoto wetu wa leo tunawanyima fursa nzuri za namna hii maishani, hamna raha na ridhiko moyoni kama kuona kile ulichopanda utotoni kwa mkono wako mwenyewe kimemea na kustawi vyema na sasa ni kielelezo na kumbukumbu nzuri kwako juu ya kile ulichokifanya katika mazingira yako.
 
Juniors generation "Facebook, Telegram, Twitter, Instagram # Utandawazi but Utunduwazi.com"

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
siyo kosa lao lakini hawa ni generation "Z" na generation "ALPHA" huo ndiyo wakati wao sahihi japo bado wanapaswa kuelekezwa na watangulizi wao juu ya vile ambavyo teknolojia au fedha haiwezi kuvibadili au kuwafanyia.
 
Watoto wetu wa leo tunawanyima fursa nzuri za namna hii maishani, hamna raha na ridhiko moyoni kama kuona kile ulichopanda utotoni kwa mkono wako mwenyewe kimemea na kustawi vyema na sasa ni kielelezo na kumbukumbu nzuri kwako juu ya kile ulichokifanya katika mazingira yako.
Watoto wetu wa leo tunawanyima fursa nzuri za namna hii maishani, hamna raha na ridhiko moyoni kama kuona kile ulichopanda utotoni kwa mkono wako mwenyewe kimemea na kustawi vyema na sasa ni kielelezo na kumbukumbu nzuri kwako juu ya kile ulichokifanya katika mazingira yako.
Swadakta
 
Mkuu mada ni nzuri sana lakini nadhani haya mambo yanaenda kikanda zaidi.

Kwa mfano mikoa ya iringa na njombe hasa wilaya za mufindi,kilolo,makambako na wanging'ombe suala la kupanda miti kila mtoto wa kuanzia miaka minne analifahamu na faida zake pia. Labda kwenye hizo mada za wanyama na usafi wa kutunza maeneo ya makazi.
 
Nimewiwa kulizungumzia hili, kwa kuwa jamii inaendelea kupoteza kabisa ule mguso wa kimazingira na umuhimu wake katika maisha yao.

Katika ngazi ya familia waathiriwa zaidi ni watoto wetu, Mtoto aambiwi wala kufundishwa kwa vitendo kupanda miti na kuitunza, kupenda wanyama na kuwahudumia wala kutunza nyumba na mazingira yake ikiwemo kupalilia na kufanya usafi.

Inasikitisha kuwa na kizazi ambacho mtoto kila aonapo mti mdogo wenye afya njema uwaza kuuharibu tu kwa kuuchuma kama fimbo kwa kuwa ndicho kitu pekee anachoelewa ni matumizi sahihi ya mti huo iwe ni shuleni au nyumbani daima uagizwa akalete fimbo ili aadhibiwe.

Chakusikitisha ni kuwa watoto hawa wanakuwa wakiwa na ile mentality ya uharibifu wa mazingira ndani yao, kwani mitaani kwao wanakoishi kila siku wanachoshuhudia ni utupaji taka ovyo na uchimbaji mchanga barabarani, matumizi yaliyokithiri ya mkaa, ukataji miti kiholela kupisha maendeleo ya vitu kwani miti na uoto kama nyasi uonekana kama kikwazo cha upitishaji wa huduma za kijamii kama maji na umeme, na pia uoto pekee ni matumizi mabaya ya eneo la ardhi.

Leo hii tunalea kizazi ambacho ukipanda miche yako lazima uwe mwenyewe ndiye mlinzi dhidi ya watoto kwa maana badala ya kuwaofia wanyama, watoto wetu ndiyo janga kuu.

Ukijisahau kidogo tu utakuta mtoto wa watu ashang'oa au kuvunjavunja mashina ya miti yako yuko comfortable kabisa hana wasiwasi anaichezea hapo hapo alipoichumia.

Na chakumfanya huna kwa kuwa watoto hao katika fahamu zao hawatambui hata kama kutenda hivyo ni kosa na wala hata jamii yenyewe haioni ikiwa suala kama hilo lina uzito wowote ule.

Anakuja mtu mzima kukuomba umruhusu achume dawa katika mti mmoja hapo nyumbani kwako, pasipo kusita unamruhusu nenda kachume huku ukiwa hauna shaka yeyote ile unaingia zako ndani, punde anarudi kukushukuru kishamaliza haja zake yeye anaondoka.

Unapotoka kwenda kushuhudia alichokifanya unabaki kutikisa kichwa na kufyonza tu, kwa maana ni uharibifu tu utakuta mtu badala ya kuchuma majani katika tawi kaamua kuondoka na tawi kabisa.

Mwingine yeye ni kudonoa-donoa tu viini vya shina la miti akitafuta majani malaini na amalize haja zake haraka aondoke, wengine atachimba mizizi yote anaacha kisha anakata ule mzizi mkuu ili achukue kipande kidogo tu
na kama haitoshi hata kufukia pia ni mtihani atapaacha jinsi alivyopafukuwa pasipo kujalisha mwendelezo wa uhai wa huo mti utakuaje na kwa bahati mbaya anakuwa pengine kaambatana na mwanaye ambaye anashuhudia namna miti inavyopaswa kutendewa hasa isipokuwa yakwako.

Vijijini hali ni mbaya zaidi, mtoto tokea kukuwa kwake anachoshuhudia jamii yake ikipambana nacho kama adui mkubwa huwa ni miti, vichaka na majani.

Muda wote maadui hao watatu (miti, vichaka na majani) popote pale wanapoonekana huwa wanapaswa kuondoshwa kwa sababu yeyote ile iwe kwa kufyekwa, kukatwa au kuchomwa moto kwa kisingizio cha kujipatia kipato, kuandaa eneo la mashamba, kusafisha mji, kuepuka mbu, wanyama nakadhalika.

Unategemea mtoto wa mchoma mkaa ambaye hajawahi kushuhudia hata mara moja baba yake akipanda mti zaidi ya kuikata na kuichomea mikaa na matofali kesho na kesho kutwa aje kuwa balozi mwema wa mazingira yake.

Tunasahau kuwa vitu vidogo vidogo vinavyoonekana kutokuwa na madhara ndiyo baadae upelekea ufa mkubwa usiozibika.

Kama jamii ni wakati wa kubadilika na kuanza kuyajali mazingira yetu kwa vitendo kwa kuwaelekeza watoto wetu juu ya usahihi wa kutenda kwa kujali miti,vyanzo vya maji na uoto wa asili, kulinda na kutunza mazingira yao ili tuepuke kizazi kijacho kisichokuwa na huruma na mazingira, na mazingira nayo hayatokuwa na huruma nao.
SI Unit ya uharibifu wa mazingira na ukataji hovyo wa miti ni WASUKUMA, hawa watu wasipoangaliwa kwa jicho la tatu miongi miwili ijayo nusu ya Tanzania itakua jangwa
 
Mkuu mada ni nzuri sana lakini nadhani haya mambo yanaenda kikanda zaidi.

Kwa mfano mikoa ya iringa na njombe hasa wilaya za mufindi,kilolo,makambako na wanging'ombe suala la kupanda miti kila mtoto wa kuanzia miaka minne analifahamu na faida zake pia. Labda kwenye hizo mada za wanyama na usafi wa kutunza maeneo ya makazi.
Nafikiri ufahamu huo utakuwa umechagizwa na uwepo wa shughuli za kiuchumi zitokanazo na miti katika maeneo husika, na ukifuatilia kwa umakini katika uelewa wa ndani, siyo kuwa wanapanda miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira bali ni kwa ajili ya biashara tu na siyo kupanda mti kwa hiari nakutegemea faida za kibaiolojia pekee.
 
Back
Top Bottom