Watoto wa maskini walioajiriwa serikalini wanatumika kuwaadhibu wazazi na ndugu zao waliowasomesha wakiamini wanalinda nchi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Wanaoangaika na maskini wa nchi ni watoto wa maskini walioajiriwa serikalini. Viongozi wa TANAPA wameliwa vichwa kwa sababu tu wamegusa maslahi ya royal family.

Viongozi wa TANAPA wameona namna wanasiasa wasivyo na fadhila; wamepambana na Masai wakiamini watapanda vyeo wameambulia fedhea ya kuingizwa kwenye vyeo visivyo na tija NCHINI.

Wanasiasa wa Tanzania kwa sasa wana royal families zao ambapo kazi kubwa wanayofanya nikuwatumikisha watoto wa wakulima waonekane wabaya wakati watoto wao wakionekana ni wazuri.

Watoto wao hakuna sehemu wameonekana ngorongoro wala Mbarali wakishinikiza wafugaji na wakilima waadhibiwe. Hakuna mtoto wa waziri wala mbunge aliyeshiriki udhulumati; hakuna mtoto wa mwanasiasa na mfanyabiashara ambaye ni polisi au askari misitu.....wao wamewawekea maeneo maalum watoto wao.

Lakini kupitia amri kutoka juu maskini ambao ni watoto wa wakulima na wafugaji ndio wamekuwa wakitumiwa kuwaadhibu wazazi wao kisa wakiaminishwa kwamba huo ndio uzalendo. Maskini waamsheni watoto wenu mliowasomesha waache kuwatesa.
 
"Viscous cycle of poverty"

Unakubali kutumiwa, unatumika vibaya ama unatumika visivyo, kisha unafedheheshwa, na hatimaye unabaki umechanganyikiwa.

Used, misused, abused, and confused.
 
Back
Top Bottom