Watoto wa vigogo na ajira BoT

Watoto wa vigogo na ajira BoT

Mbona watoto wa Nyerere hakuna kabisa, sio tu BOT bali hata sehemu nyeti za serikali.Wao walipatikana Jeshini na wengine sikuwahi wasikia wakifanya kazi inayoeleweka. Mwinyi naona watoto wake woote mashavu tu sehemu nyeti zote serikalini.
watoto wa kagame museveni kiir garang wanapatikana jeshini hawa wakwetu wanapatikana kwenye mabenki na kwenye show za diamond, JP yatimue yote ndo hayohayo yanashinda humu JF yakitukana.
 
Huyu ni mtoto wa Pombe Magufuli anayesema ni mtoto wa mkulima. Dogo yupo ndani ya mjengo pacha anakula maisha. Ni rafiki mkubwa wa dogo mwingine anayepiga mzigo ndani ya BOT anaitwa Jabir Kigoda. Hawa ndio wanaCCM wanaokula fadhila za chama na si wewe kutwa nzima unapiga makelele JF hata bando kulipata mpaka uvuje jasho. List inayofuata jiangalie wewe unayejiita mwanaCCM kama upo au mawanao wa mtoto wa shangazi yako kama yupo.. Wafuatao ndio wanaCCM;
1.Beatrice Bomani
2.Zakaria Kawawa
3.Salama Mwinyi
6.Salama Mahita
7.Rachel Msekwa
8.Jane Sitta
9.Jasmini Karume
10.Radhia Shein
11.Justina Nchimbi
12.Blasia Benjamin W. Mkapa
13.Jerome Diallo
14.Likele Ngasongwa
15.Andy Magufuli
16.Thomas Mongela
17.Jabir A. kigoda
18.Marry Mramba
19.Ismail Meghji
Mkuu magufuli hana mtotot mkubwa hivyo.
 
image.jpg


Hii ni Orodha ya baadhi ya Majina ya Watoto wa Vigogo ambao ama hawapo BOT lakini wanaendelea kulipwa mishahara ama uwepo wao ndani ya Taasisi hiyo hauna tija.
 
Haya ni majina yaliyopigiwa kelele sana kipindi cha Kikwete, lakini jamaa akawa anachekacheka na kukimbilia nje ya nchi.
Na wewe ulikuwa wa kwanza kunyamaza kimya, sasa unajitia mjuaji....na unataka kusheherekea majina mawili, what about the rest?.

kuna wakati huwa una akili na wakati mwingine unakua umempa mbwa akili zako akushikie.
 
Pamela Lowassa, ni daktari pale Muhimbili.
Mtoe kwenye hiyo List yako feki!
Sasa unataka nimtoe kwa sababu gani ilhali anaendelea kulipwa mshahara BOT? Ulimsikiliza vizuri Jana Mheshimiwa Rais? Umesoma mada yangu na kuelewa? Au umekurupuka tu kuchangia kwa vile tu kaguswa mtoto wa bosi wako?
 
....katika nchi hii ya magufuli, habari zako za kimombasa peleka huko!.
....ni hao tu ndo uliowaona?
#hapakazitu!
 
Mafisadi kweli wanaitafuna hiii nchi wao na wanao, Magu please do something, tuko nyuma yako kuondoa huu uozo,
 
Ila kiti kimoja tukubali, tanzania karibu kila sehemu, serikalini na binafsi asilimia kubwa watu kupata kazi kwa kiwa na connection na mtu eneo hilo, hivyo kama hao watoto wa vigogo waliumganishwa ila sifa wanazo na kazi wanapiga, sioni tatizo lao ila KUANZIA sasa kama vipi mfumo ubadilishwe ila ni ngumu sana, kubebana kupo pale pale! Cha msingi anayebebwa awe na sifa!
 
Watoto wa vigogo hawafiki 50 kumbe... Ila kuna wafanyakaz zaidi ya 1000.. Lakini tunawapigia kelele kutokana na wivu
 
Salma Mahita si alishaacha kazi kitambo..Mbona yuko kwenye list?
 
Back
Top Bottom