Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Jun 20, 2022
1,215
2,995
Wazazi tuache kuwadekeza watoto wetu ndo Mana matukio ya ubakaji na ulawiti yanaongezeka.

Leo nimeenda kumtembelea jirani yangu ni family friend nimemkuta yupo sebuleni na mtoto wake wa kiume wa darasa la sita afu mama amekaa kihasara tu mtoto anayaona mapaja ya mzazi wake baada ya kuingia Mimi ndo anajiweka vizuri ni malezi gani kwa mtoto wa kiume wazazi hasa wamama wajitafakari.

Single mother na nyie mna yenu sio kwamba tunawasema Sana mbadilike malezi yenu uzungu mwingi. Kuna jirani yangu ni single mother mtoto wake kila anachotaka yeye ni kumnunulia asililie kitu mtoto yuko nursery school wiki nzima mtoto hataki kwenda shule na mama yake anamchekelea tu sio malezi tunawapenda watoto wetu tuwalee na tuwape malezi kwa limit, samahani Kama nimekukwaza ukweli lazima tuambiane.

Na sisi wakina baba tunakosea tushirikiane na wake zetu kwenye malezi Mambo yasiofaa tuyakemee na tuache tabia ya kuvaa nusu uchi upo sebulani umekaa na watoto zako wa kike umevaa kibukta afu uko tumbo wazi haipendezi.

Wazazi, walezi, walimu,viongozi wa dini nk tushirikiane kwenye malezi ya hawa watoto wetu. Usipo muona mtoto kwa muda au hayupo mazingira ya nyumbani jiulize Yuko wapi uko aliko yupo salama na anafanya Nini.

TV, simu ni muhimu kwa watoto kama watajifunza ya maana tusiwaachie tu watoto waangalie wanachotaka
Nakumbuka home kipindi tuko wadogo ni kosa kubwa umekutwa unaangalia channel za tv zisizo na maadili Kama Trace nk au umeweka cd, vhs zenye age above 18+ inafanya watoto wadogo wafanye Yale wanayoyaona kweny tv, cm nk

Mtoto wa siku akiamka asubuhi hasa siku za wikiend Cha Kwanza kwenye tv kaweka channel anayotaka anaangalia bila wasiwasi enzi zetu muda kuangalia tv ulikuwa ni saa 4 asubuhi baada kumaliza kazi.

Malezi bora ni msingi mzuri wa watoto wetu kataa kudekeza. Tuwalinde watoto wetu.
 
Exactly mkuu watoto inabid waheshimu vitu ya mgeni na wawe na heshima na mgeni utakuw upo sebuleni unaangalia tv anakuja na kubadirisha channel anawek cartoon
Nagombana na wanangu mapema sana kuhusu hilo niepukane na aibu hii Mbele ya mgeni sio heshima hata kidogo hata mtt kuzoea mgeni kupita kiasi sio vizuri Hawakawii kuuliza mgeni unaondoka lini..au unakula sana
 
Wazazi tuache kuwadekeza watoto wetu ndo Mana matukio ya ubakaji na ulawiti yanaongezeka.

Leo nimeenda kumtembelea jirani yangu ni family friend nimemkuta yupo sebuleni na mtoto wake wa kiume wa darasa la
......a very useful thread kama tutake it into actions, asilimia kubwa ya wazazI wa mid 80s and 90s wana kaulimbukeni ka maisha ya wazungu kalikosababishwa na maendeleo ya technolojia.....wazazi wanajiona wa kisasa na kwamba wanaishi kizungu Kwa kukaa nusu utupu mbele ya familia au watoto.......

Hiyo ipo sana ndugu mtoa mada, wanawake wengi ndo wanapenda pigo za kushinda chumbani amevaa pant(kyupi) only na yuko na katoto kake kakiume.........na katoto unakaona kabisa kanajitambua fulani, lakini pia wengine utaona ameenda kuoga na ktoto kake kakiume bafuni........maadili yanavunjwa kwa kigezo kwamba hivyo ndo kuishi kishua na wengine huwa wanapost kabisa........
 
......a very useful thread kama tutake it into actions, asilimia kubwa ya wazazI wa mid 80s and 90s wana kaulimbukeni ka maisha ya wazungu kalikosababishwa na maendeleo ya technolojia.....wazazi wanajiona wa kisasa na kwamba wanaishi kizungu Kwa kukaa nusu utupu mbele ya familia au watoto.......hiyo ipo sana ndugu mtoa mada, wanawake wengi ndo wanapenda pigo za kushinda chumbani amevaa pant(kyupi) only na yuko na katoto kake kakiume.........na katoto unakaona kabisa kanajitambua fulani, lakini pia wengine utaona ameenda kuoga na ktoto kake kakiume bafuni........maadili yanavunjwa kwa kigezo kwamba hivyo ndo kuishi kishua na wengine huwa wanapost kabisa........
Exactly mkuu umeandika madini muhimu mkuu appreciate you🙌
 
Mitoto ya sku izi so soft na tabia za kipuuzi tu.. yani inalia machozi kabisa kwa kitu cha kingese sana...
Enzi hizo mitoto ilikua kulia ni shuhuli nzito kuchezea stiki ni kawaida tu ila sku hizo ukimchapa mtt fimbo moja tu hicho kilio chake majirani lazma waamke...

Too much uzungu kwenye malezi ndo kunaleta these week ass babies... kitoto kidogo kinahisi kinamiliki dunia yani eveything kwake ni yes tu hajui no
 
Back
Top Bottom