Watoto wa kike vs wa kiume?

Kuna jamaa yangu yeye kapiga 4 kwa mke,akaona ajaribu ugenini matokeo hayakubadilika,akaona ampandishe cheo mkewe sasa hivi mtoto ana mwaka 1 tangu azaliwe na kufanya awe na watoto 6 wa kike kutoka kwa wanawake wa 3.

Pembeni huwa nasikia kuwa huwa anachepuka na kuoa ili ajaribu bahati ya kuchanganya jinsia lkn ndio hivyo.

Kuna mwingine tayari anao watatu,sasa yeye huyu akiona safu yangu ya ulinzi anaanza kuniomba nimpatie seminar.

Yote kwa yote mtoto ni mtoto,tujaribu na kujitahidi kuwapa malezi bora na stahiki ili kuwaepusha na mabaya ya dunia kadri iwezekanavyo.

NB:
Pamoja na mipango inayotajwa kuwa ni ya God,lkn mwanaume kumfikiria vibaya mwanamke eti kisa mnazaa jinsia moja tu siyo sahihi na siyo sawa kwani yeye ana xx wakati sisi wanaume ambao siyo mashoga tuna YX.
Watu ambao hawana akili Ni mzigo kwa kweli😂. Jinsia ya mtoto wa kiume asilimia 95 inatoka kwa Y ya baba. Then asilimia zilizobaki Ni siku za mwanamke (ratiba ya kufanya ngono)
 
Habari wanajamvi.!
Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana.
Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice.
Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?
Ambia jamaa aache ujinga kuna wengine hawana hata huyo moja wa kumuita baba....anachukia na akati ndo uwezo wa mbegu zake? Mbeleni atajua kwanini Mungu aliamua kumpa mabinti
 
Watoto wa kiume ni kuendeleza familia tu kiuzao ila angejua mtoto wa kike deal sana, ni sisi ndo hatusahau makwetu na wazazi pia, wa kiume akioa tu majukumu huongezeka tena kwa usawa tuliomo naona hata malezi ya mtoto wa kike yana nafuu sana,, utahangaika kulea jembe lako then mwisho linakuwa shoga, bora usizae tu
 
Wanaume wengi tunapenda watoto kiume sababu ya kuendeleza majina ya ukoo,

--tunaona tumepata rafiki ambaye atakuja kutusaidia baadae kwa njia moja au ingine.

Lakini kumbe ndivyo sivyo..

Mtoto wa kike ndy mwenye mapenzi makubwa sana kwa baba yake kuliko mtoto wa kiume.

Mtoto wa kiume akishaoa anakuwa tayari anaona wazazi especially baba kwamba ni mzigo.
Mtoto wa kike hata akishaolewa lakini bado ataendelea kuwasidia wazazi wake especially baba..

Mtoto wa kiume ni wa mama
Mtoto wa kike ni wa baba.

Ukwl mchungu.
 
Nadhani shida ni hapo kwenye kuendeleza jina
 
Mtoto wa kiume akishaoa anakuwa tayari anaona wazazi especially baba kwamba ni mzigo.
Mtoto wa kike hata akishaolewa lakini bado ataendelea kuwasidia wazazi wake especially baba..
Kinachotokea hapo ni kwamba mtoto wa kiume ukishaoa, inabidi upambane kujionyesha kwa WAKWE kwamba upo vizuri kifedha. So unakuta muda mwingi unatumia kuwafurahisha wakwe, mashemeji nk. Na usipokua makini wakwe na mashemeji wanaweza kukugeuza msukule ukajikuta unasahau kabisa mambo ya nyumbani kwenu!
Kwa upande wa mwanamke yeye akishaolewa huo unakua ni muda wake wa KUVUNA na kwavile mara nyingi mwanamke hana majukumu mengi, basi ni rahisi kwake kuwakumbuka wazazi kwa kile anachopata.
 
Back
Top Bottom