Watoto wa kike vs wa kiume?

Watoto wa kike vs wa kiume?

Noma sana..ila hongera.

Umewahi wish otherwise?
Kuna jamaa yangu yeye kapiga 4 kwa mke,akaona ajaribu ugenini matokeo hayakubadilika,akaona ampandishe cheo mkewe sasa hivi mtoto ana mwaka 1 tangu azaliwe na kufanya awe na watoto 6 wa kike kutoka kwa wanawake wa 3.

Pembeni huwa nasikia kuwa huwa anachepuka na kuoa ili ajaribu bahati ya kuchanganya jinsia lkn ndio hivyo.

Kuna mwingine tayari anao watatu,sasa yeye huyu akiona safu yangu ya ulinzi anaanza kuniomba nimpatie seminar.

Yote kwa yote mtoto ni mtoto,tujaribu na kujitahidi kuwapa malezi bora na stahiki ili kuwaepusha na mabaya ya dunia kadri iwezekanavyo.

NB:
Pamoja na mipango inayotajwa kuwa ni ya God,lkn mwanaume kumfikiria vibaya mwanamke eti kisa mnazaa jinsia moja tu siyo sahihi na siyo sawa kwani yeye ana xx wakati sisi wanaume ambao siyo mashoga tuna YX.
Watoto wa kiume ni rahisi kushawishiwa na mama yao kumtenga baba.
Yawezekana lkn kama baba ulikuwa mbali nao na hutimizi wajibu wako kwa uwazi.
 
Habari wanajamvi.!
Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana.
Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice.
Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?
Wanaona mtoto wa kiume ndiyo mrithi wa kweli.

Wa kike wataolewa na kuchukuliwa na familia za waume wao, wa kiume ndio watakaoendeleza familia ya baba, hata jina wa kike watabadili na kuitwa majina ya waume zao, au kuzaa wajukuu wenye majina ya ubini wa baba zao, si wa baba za mama zao.

Ni mfumodume compounded.

Unatakiwa kuwa poa hata ukikosa mtoto kabisa. Unafurahia maisha ya kukosa watoto, wewe na mkeo.

Kukosa tabasamu kwa sababu umekosa mtoto wa kiume ni ubaguzi wa kijinsia, ni kukosa shukurani.

Ujinga zaidi, hapo mara nyingi anayelaumiwa ni mwanamke, kwa nini hajazaa mtoto wa kiume, wakati, kibaiolojia, mwanamme ndiye anafanya mtoto awe wa kiume au kike.


A child's biological sex (male or female) is determined by the chromosome that the male parent contributes. Males have XY sex chromosomes while females have XX sex chromosomes; the male can contribute the X or Y chromosome, while the female must contribute one of their X chromosomes.

Kuna dada mmoja alizaa watoto watatu wa kike, ilifikia mpaka anapigwa na mumewe kwa kutozaa mtoto wa kiume, wakati kibaiolojia mume ndiye anaamua mtoto awe wa kike au wa kiume.

GenderdeterminationPI.jpg
 
Habari wanajamvi.!
Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana.
Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice.
Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?
Sio sisi tu wababa hata wake zetu huwa wanapenda sana watoto wa kike, ila Cha ajabu aisee ukiwapata hao watoto wa kike, sisi wababa huwa tunawapenda sana mabinti mabinti zetu.

Ila kwetu sisi kwenye dini yenu ukijaaliwa watoto wa kike ni neema kubwa sana, tena ukawalea vizuri mpaka wakaolewa, peponi yako aisee.
 
Yes, mtoto ni mtoto wako akiwa mtoto, akishakuwa mkubwa siyo mtoto wako tena, atakuwa mke wa mwanaume mwenzio.

Ukweli ni kwamba mwanaume kutokuwa na mtoto wa kiume ni doa....

Kule kwetu tuna swali huwa tunauliza pindi mtoto anapozaliwa tuu kwamba kaleta "Mnyafee" (Kaleta mtu wa wapi?). Hapo utapata majibu 2, kama mama kazaa dume utasikia kaleta "Mnyakhaya" (Kaleta mwenye mji). Kama amezaa jike utasikia kaleta "Mnyang'eantu" (Kaleta mtu wa miji ya watu).

Hata kwenye vitabu vitakatifu vinaonesha thamani ya mtoto wa kiume siyo sawa na mtoto wa kike. Watoto wa kiume ndiyo urithi wa baba katika uzao wake. Ukipata watoto wa kike tu ina maana kizazi chako ndiyo kimeishia hapo, ukifa na uzao wako unaishia palepale. Hao watoto wa kike wataolewa na watoto watakaozaa watakuwa na ubini wa huko walikoolewa.

Tuache kujipata mafuta kwa migongo ya chupa kwa misemo kama "mtoto ni mtoto". Yes mtoto ni mtoto akiwa mtoto, akishakuwa mkubwa siyo mwanao atakuwa mke wa mwanaume mwenzio.​
 
Kikubwa ni kuendeleza tu ukoo na ufahari kuwa umepata mlinzi na kiongozi wa ukoo. Japo kwa experience yangu, mtoto wa kwanza akiwa wa kike huwa ana faida sana haswa kwenye kusaidia malezi na kuongoza wadogo zake.

Watoto wa kike huwa na umama ndani yao Ila kwa wakiume huwa tofauti na haswa akioa mwanamke ambaye haipendi ukoo wake. Story huwa inaishia hapo
 
Ole

Ole mama yake awe anamtuma kwa michepuko yake halafu michepuko ya mama iwe ya binti.
Ole mke na binti yake waungane kumtenga baba.
Kwa mabinti ni kitu ambacho hakitatokea, unless unajichanganya, akufume na michepuko. Hivi unajua wakati mwingine huwa kuna ugomvi kati ya mama na mabinti zao, kisa baba. Hapa JF kuna mabinti ambao mama zao ni paka na panya kisa kuwa karibu na mabinti zao (siyo wachagga - mtoto wa baba).
 
Ni
Kwa mabinti ni kitu ambacho hakitatokea, unless unajichanganya, akufume na michepuko. Hivi unajua wakati mwingine huwa kuna ugomvi kati ya mama na mabinti zao, kisa baba. Hapa JF kuna mabinti ambao mama zao ni paka na panya kisa kuwa karibu na mabinti zao (siyo wachagga - mtoto wa baba).
Nina mifano hai wala siongelei hadithi mkuu.
Mjomba angu alitengwa na mkewe,akatumia uanaume kukomaa,binti zake yaani wa kwanza akawa msitari wa mbele kumsojodoa baba yake,hatimaye binti wa pili kutoka mwishoni akashiriki kumpatia baba yake chai yenye sumu mndaaji akiwa ni mke na binti yake mkubwa.

Muda huo huo wakiume ndio wakamuambia mama yao ya kwamba hayo huyatendayo sisi wanao tukitendewa na wake zetu wewe utasimama upande gani?

Wakiume wakumuambia baba yao kuwa oa mke mwingine na sehemu ya pension jenga makazi yako na mama yetu mdogo.
 
Back
Top Bottom