Watoto wa kike vs wa kiume?

msakhara

JF-Expert Member
May 26, 2019
271
370
Habari wanajamvi.!
Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana.
Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice.
Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?
 
Habari wanajamvi.!
Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana.
Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice.
Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?
ashukuru kupata,wengine hawaja barikiwa kabisa
 
Habari wanajamvi.! Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana. Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice. Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?

Fahari ya baba ni mtoto wa kiume, ndiye atakaye endeleza jina la ukoo wake.
Raha/Faraja ya baba ni mtoto wa kike maana huweza kugusa mtima wake.
Wote wanahitajika kwenye maisha ya mwanume.

N.B Takwimu zinaonyesha ndoa yenye watoto wa kiume wengi hudumu muda mrefu kuliko ndoa zenye watoto wa kike wengi au watupu
 
Wengi huona kuwa mtoto wa kiume ni kama mwanae (mshkaji) wake wa baadae, atampa kampani nk hili unaweza kuliona au hata kuuliza jinsi baba alivyo comfortable pale anapoamua kutoka na mwanae wa kiume kuliko wa kike Kuna Hali Fulani hivi unaihisi, halafu Kuna uwazi (baba anapata wasaa wa kufunguka vitu vingi) Fulani hivi akikaa baba na mtoto wake wa kiume na ndo baba (kiongozi) wa familia baadae, watoto wa kike wote watakuwa ni mali ya mwanaume mwingine wakishaolewa baadae si unajua afrika mtoto wa kike akishaolewa watoto wake karibu wote bond itakuwa Kwa baba Yao hata wewe ni shuhuda wa hili wengi wetu tumeegemea sana upande wa baba zetu, hivyo Kuna loneliness baadae unaweza jikuta Babu hakuna mjukuu hata mmoja anayekutembelea wakati wa likizo zaidi ya simu mojamoja, wajukuu ikifika likizo tu hao Kwa Babu na bibi upande wa baba mara nyingi Huwa hivi Kwa jamii nyingi isipokuwa chache tu...

Baba anajivunia kimoyomoyo na kuvimba mtaani kuwa Nina dume la nyani na Mimi, hivyo anaweza kumshape mwanae wa kiume na kumpa vitu vingi vya kurithi kama vile mawazo, ushauri hata njia za kupita kwenye mafanikio pia coz yuko na mshikaji (mwanae).
 
Noma sana..ila hongera.

Umewahi wish otherwise?
Kuna jamaa yangu yeye kapiga 4 kwa mke,akaona ajaribu ugenini matokeo hayakubadilika,akaona ampandishe cheo mkewe sasa hivi mtoto ana mwaka 1 tangu azaliwe na kufanya awe na watoto 6 wa kike kutoka kwa wanawake wa 3.

Pembeni huwa nasikia kuwa huwa anachepuka na kuoa ili ajaribu bahati ya kuchanganya jinsia lkn ndio hivyo.

Kuna mwingine tayari anao watatu,sasa yeye huyu akiona safu yangu ya ulinzi anaanza kuniomba nimpatie seminar.

Yote kwa yote mtoto ni mtoto,tujaribu na kujitahidi kuwapa malezi bora na stahiki ili kuwaepusha na mabaya ya dunia kadri iwezekanavyo.

NB:
Pamoja na mipango inayotajwa kuwa ni ya God,lkn mwanaume kumfikiria vibaya mwanamke eti kisa mnazaa jinsia moja tu siyo sahihi na siyo sawa kwani yeye ana xx wakati sisi wanaume ambao siyo mashoga tuna YX.
 
Back
Top Bottom