Watoto wa kike vs wa kiume?

Watoto wa kike vs wa kiume?

Habari wanajamvi.!
Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana.
Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice.
Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?
Atulie tu
Mambo ya Genetics
X chromosome zinafanya kazi zaidi
 
Mtoto ni baraka ila mtoto wa kiume kazi yake ni kuendeleza uzao wako ,huna mtoto wa kiume maana yake uzao wako umefika mwisho hapo ulipo na kingine ni mrithi sahihi wa Boma.
 
ashukuru kupata,wengine hawaja barikiwa kabisa
Mungu akutie nguvu umeongea kitu kikubwa sana. Mi nina watoto watatu wa kike. Kiukweli, wanaume wengi wanatamani wawe na watoto wa kiume hata 1 tu ila kama amekosekana shukuru Mungu kwa ulio nao. Binafsi sitamani kuongeza wala sitamani mtoto wa kiume. Nitajitahidi niwasomeshe hawa, wakue najua wataniletea mtoto wa kiume tu either kwa kuolewa au kwa kuzaa Mjukuu wa kiume. Mambo mengine sio ya kujiumiza kwani hata ukisema utafute nje, nakuambia leo hata uzae na wanawake 10 tofauti. Wote watakuwa wa kike. Tumeshuhudia haya kwa baadhi ya jamaa.
 
Ukishajua kuwa Mungu ndio humbariki mtu mtoto, huwezi waza mambo ya jinsia, hata jinsia hukupa kwasababu zake..
Mwaka wa 2000's nikiwa na mtoto mmoja wa Kike, Mungu alisema nami kuna wengine 2 wanakuja na watakuwa 3 wote wa kike.

Binafsi kama mwanaume niling'unika Moyoni na Akaniambia. Si una ungunika na unataka wa kiume, sawa nitakupa wa kiume ila atakuwa Tanzi na mwiba kwako. Akanionesha yule mtoto alivyo.

Mi ni mweupe, mrefu na mnene na watoto zangu wote wa kike nimewafananiza nami na mke wangu yeye ni mweupe, mrefu mnene ila kwao kuna ndugu zake ambao ni weusi. Hahaaaaaa kajamaa kamefanana na mimi ila keusi na kafupi. Alinionesha kajamaa kanavuta bangi na kunywa Pombe ile Mbaya.

Kwa wakazi wa Mbeya pale Nanenane stendi kuna dogo anaitwa Manyau. Huyo mtoto kafanana useful, weusi na kila kitu kama manyau wa pale Nanenane Mbeya.

Nikajifunza, yatupasa tushukuru kwa kila jambo. Huwa nikitaka mtaniaga mke wangu namwambia, watatu wa kike wametosha na ndio wangu. Ukiongeza yule wa kiume ni wako.
 
Hizo ni ndoto . Afya ya akili ni muhimu sana amka kumeshakucha
 
Amina, asante kwa ushuhuda huu...

Ngoja na mimi nishuhudie wangu..

Mimi sijabarikiwa mtoto bado, wakati naomba na kutaka mtoto Mungu alisema nami kuwa nitapata mtoto wa kike na jina lake ataitwa Mariamu Makdalena.

Hii hali ilinishangaza sana mpaka Leo nashangaa jamani...
 
Inategemea na familia, mtoto ni mtoto..akiishi kusudi la kiMungu ni neema kubwa kwa familia
Case study: Mama flani kazaa wanne. Mmoja wa kiume, watatu wa kike. Wa kiume chapombe mbaya, wakike ndo wamemjengea na ndo wanamtunza. Wameolewa pazuri na kuanzia matibabu yake, safari zake, vyakula vya mwezi ni hao wa kike. Wa kiume anateswa na aliekua mke wake so kageukia pombe mno na hata kabla hajawa ex, alikua busy sana kwa upande wa mwanamke. Ninachosema tuombe Mungu uzao wetu usimame katika kusudi la kiMungu utakuwa faraja kwetu, ama la, hatutaona ladha ya maisha hata kadori.....
 
Wakiume ili kuendekeza ukoo
Ila kwa Bahati mbaya mara nyingi watoto wa kwanza niwakike
 
Habari wanajamvi.!
Nina shemeji yangu amebahatika kupata mtoto wa 4 jana.
Watoto wote ni mabinti, inaonesha hakufurahishwa kabisa na matokeo hayo. Hata tabasamu lake usoni nikaona limepotea!! Hadi mkewe (sister) akanotice.
Huwa ni kwa nini wanaume wengi wanapenda mtoto jinsia ya kiume? Kwamba kuna kipi cha ziada wanatarajia?
Mtoto wa kiume ni mlinzi na msimamizi wa mali na usalama wa kifamilia.
 
Yes, mtoto ni mtoto wako akiwa mtoto, akishakuwa mkubwa siyo mtoto wako tena, atakuwa mke wa mwanaume mwenzio.

Ukweli ni kwamba mwanaume kutokuwa na mtoto wa kiume ni doa....

Kule kwetu tuna swali huwa tunauliza pindi mtoto anapozaliwa tuu kwamba kaleta "Mnyafee" (Kaleta mtu wa wapi?). Hapo utapata majibu 2, kama mama kazaa dume utasikia kaleta "Mnyakhaya" (Kaleta mwenye mji). Kama amezaa jike utasikia kaleta "Mnyang'eantu" (Kaleta mtu wa miji ya watu).

Hata kwenye vitabu vitakatifu vinaonesha thamani ya mtoto wa kiume siyo sawa na mtoto wa kike. Watoto wa kiume ndiyo urithi wa baba katika uzao wake. Ukipata watoto wa kike tu ina maana kizazi chako ndiyo kimeishia hapo, ukifa na uzao wako unaishia palepale. Hao watoto wa kike wataolewa na watoto watakaozaa watakuwa na ubini wa huko walikoolewa.

Tuache kujipata mafuta kwa migongo ya chupa kwa misemo kama "mtoto ni mtoto". Yes mtoto ni mtoto akiwa mtoto, akishakuwa mkubwa siyo mwanao atakuwa mke wa mwanaume mwenzio.​
Uongo na upumbavu sababu ya kutokujua.
Mtoto DNA ni ile ile awe wa kike au wa kiume. Mtoto wangu wa kike hata akiolewa akaitwa jina lingine bado kabeba DNA yangu na watoto wake wana DNA yangu na watoto wa watoto wake wana DNA yangu vizazi na vizazi. Hata ukichukua kizazi cha 100 ukipima DNA na mimi utakuta kuna uhusiano. Hapo ulipo baba wa bibi wa bibi yake bibi yake mama yako akipimwa DNA na wewe itaonekana kuna uhusiano sawa sawa na babu wa babu wa babu wa baba yako hivyo kama ni urithi damu yako bado ndo itahusika. Tatizo labda jina ila as long as ni damu yako tatizo halipo.

Kuhusu kurithi jina ni mifumo tu ya kikabila na jamii ilipoweka huu mfumo ndipo hapo mtoto wa kike akakosa thamani ila katika uhalisia wa damu, damu yako ni damu yako itaendelea kuwa hivyo hata aitwe jina gani.
 
Ni

Nina mifano hai wala siongelei hadithi mkuu.
Mjomba angu alitengwa na mkewe,akatumia uanaume kukomaa,binti zake yaani wa kwanza akawa msitari wa mbele kumsojodoa baba yake,hatimaye binti wa pili kutoka mwishoni akashiriki kumpatia baba yake chai yenye sumu mndaaji akiwa ni mke na binti yake mkubwa.

Muda huo huo wakiume ndio wakamuambia mama yao ya kwamba hayo huyatendayo sisi wanao tukitendewa na wake zetu wewe utasimama upande gani?

Wakiume wakumuambia baba yao kuwa oa mke mwingine na sehemu ya pension jenga makazi yako na mama yetu mdogo.
Familia za kishetani zenye malaika
 
Mtoto ni baraka ila mtoto wa kiume kazi yake ni kuendeleza uzao wako ,huna mtoto wa kiume maana yake uzao wako umefika mwisho hapo ulipo na kingine ni mrithi sahihi wa Boma.
Huu ni uongo. Uzao hauendelezwi kwa jina bali DNA na DNA ya babu zako na bibi zako hazina tofauti.
 
Uongo na upumbavu sababu ya kutokujua.
Mtoto DNA ni ile ile awe wa kike au wa kiume. Mtoto wangu wa kike hata akiolewa akaitwa jina lingine bado kabeba DNA yangu na watoto wake wana DNA yangu na watoto wa watoto wake wana DNA yangu vizazi na vizazi. Hata ukichukua kizazi cha 100 ukipima DNA na mimi utakuta kuna uhusiano. Hapo ulipo baba wa bibi wa bibi yake bibi yake mama yako akipimwa DNA na wewe itaonekana kuna uhusiano sawa sawa na babu wa babu wa babu wa baba yako hivyo kama ni urithi damu yako bado ndo itahusika. Tatizo labda jina ila as long as ni damu yako tatizo halipo.

Kuhusu kurithi jina ni mifumo tu ya kikabila na jamii ilipoweka huu mfumo ndipo hapo mtoto wa kike akakosa thamani ila katika uhalisia wa damu, damu yako ni damu yako itaendelea kuwa hivyo hata aitwe jina gani.
Boss...unaweza kubari mwanao aitwe majina ya mwenye nyumba wako su jirani yako?(majina yote hadi ya ukoo)
 
Hizo ni ndoto . Afya ya akili ni muhimu sana amka kumeshakucha
Kwa umri wangu sio wewe tu wakala wa Shetani, hata Shetani mwenyewe hawezi nidanganya wala nipotosha kuhusu Mungu. Pole na hunipati ng'ooooooo. Kajaribu kwengine. Jini Mahaba mkubwa wewe.
 
Uongo na upumbavu sababu ya kutokujua.
Mtoto DNA ni ile ile awe wa kike au wa kiume. Mtoto wangu wa kike hata akiolewa akaitwa jina lingine bado kabeba DNA yangu na watoto wake wana DNA yangu na watoto wa watoto wake wana DNA yangu vizazi na vizazi. Hata ukichukua kizazi cha 100 ukipima DNA na mimi utakuta kuna uhusiano. Hapo ulipo baba wa bibi wa bibi yake bibi yake mama yako akipimwa DNA na wewe itaonekana kuna uhusiano sawa sawa na babu wa babu wa babu wa baba yako hivyo kama ni urithi damu yako bado ndo itahusika. Tatizo labda jina ila as long as ni damu yako tatizo halipo.

Kuhusu kurithi jina ni mifumo tu ya kikabila na jamii ilipoweka huu mfumo ndipo hapo mtoto wa kike akakosa thamani ila katika uhalisia wa damu, damu yako ni damu yako itaendelea kuwa hivyo hata aitwe jina gani.
Bwana mkubwa, binti yako ni mwanao akiwa mdogo, akishabalehe tayari ni mke wa mwanaume mwenzio...

Hilo ukubali usikubali ndiyo uhalisia..... Watoto watakaozaa hawako upande wako tena...

Mwanao wa kiume akizaa ndiyo uzao wako huo, hata wajukuu wa mwanao wa kiume taste yao ni tofauti na wa wanao wa kike..

Achana na nyenyenyee za DNA.
 
Back
Top Bottom