Watoto kumsikiliza zaidi mama yao kuliko baba ni machungu

Wanawake baadhi uwaga na hii tabia yao moja ya kipumbavu sana..ya kumpandikiza mtoto chuki natamani wangejua jinsi mtoto akikua anavyoharibikiwa na kuwa na moyo wa chuki na visasi ambavyo mwisho wa siku anajuta kwanini anakuwa na roho ngumu ya kusamehe wanajamii waliomkosea kumbe machuki,mavisasi,mahasira sio hata asili yake ni vitu vya kupandikizwa na mzazi wake...
 
Tuwafundishe watoto tabia njema ikiwa ni kuheshimu uwepo wa baba. Tuwafundishe kuwapenda baba zao na si kuwaacha wa misbehave. Na wakina baba hata kama uko busy kiasi gani jaribu kuwa karibu na watoto hata siku moja kwa week unakaa nao kucheza nao na labda hata kutoka na kuzunguka nao. Unajua na watoto wanaelewa na wanapenda kujaliwa sasa kama baba hujali huna habari nao inakua rahisi hata mama kuwapandikiza mbegu ya chuki na watoto wakrespond haraka kwa sbb hawana ukaribu na baba yao. Ila kama unaonyesha upendo juu yao itakua ngumu sana kumchukia baba
 
Thanks!!
 
sanasana nyie KE
Baba ukiplay part yako vizuri hayo maneno ya sumu wanaolishwa na mama yao hawawezi kuyaamini.
Wanaume wengi hatupendi kuwa karibu na familia, ww ukifika ukali tu, mtoto kakosea kidogo fimbo, hujui maendeleo ya mtoto shule, mtoto anaomba hela ya daftari chenga nyingi kesho inakuwa kesho, ukifika nyumbani hata ukikuta watoto wanaangalia katuni, unabadilisha unaweka mpira, matusi na kuna wakati unagombana na mkeo watoto wanaangalia kwahiyo hata wanapolishwa maneno lazima waamini.
Tukiwa wastaarabu na kupenda familia zetu hayo maneno ya chuki hayawezi penya kwa watoto hata watoto wakiambiwa hawawezi kumuamini mama yao.
Ni hayo tu
 
Samahani kama wewe ni mzazi na mimi nini mzazi, mtoto anapotoka tumboni harufu ya kwanza ni ya mama. Mtoto asiponyonya titi la mama anapata mapungufu ingawa wenzetu wana formula ya maziwa kubalance. Maneno ya mama na ile kumbatia ni tosha kumpa mtoto ukaribu kwake. Kazi ya baba ni kuleta ingawa siyo wote na kufoka.
Mapenzi ya mtoto yanatoka kwamama ndo maaana watoto amboa mama zao waliwaterekeza kuwa hamnazo, huwa wanaishia mitaani na ikitokea mama akafariki, mara nyingi watoto wanapata shida. Baba yeye ni kuuliza watoto wameshindaje, hawaoshi kuona kama wana makovu, mabaka wala hawajala wiki. Yeye anategemea neema za watu wengine kuambiwa yanayotokea kwenye familia yake.
Wewe ndio wale wale
Watoto wanalelewa ubabani wako vizuri sana
 
Kumekuwa na utaratibu wa wanawake wanapokuwa katika migogoro na waume zao kuwalisha maneno watoto ili wamchukie baba yao matokeo yake watoto wanakuwa kiburi wanafuata maneno ya mama yao.

Wanakuwa jeuri shule hawaendi kwakuwa mama anawapenda sana wapo tayari kusema uongo kumlinda mama yao.

Wazazi tuwe makini katika hili kuwapaka mavi wanaume wenu huku mkijificha kwenye migongo ya watoto.
Nakuunga mkono kwa hili,ndio maana mara zote watoto wawe wa kiume au wa kike mara zote huwa upande wa mama zaidi kimapenzi na si baba..
 
Jana nilikuwa naangalia interview mpya Barack Obama amefanyiwa na David Letterman. Ipo Netflix.

David Letterman akawa anakisifia sana kitabu cha kwanza cha Obama "Dreams From My Father".

Walipozungumzia familia, upande wa wazazi, Obama akasema ingawa jina la kitabu limemtaja baba yake, mama yake alikuwa very generous na ndiye aliyekuwa na mchango mkubwa katika kumlea, kwani baba yake hakuwepo.

Alisema kwamba ingawa baba yake aliachana na mama yake, lakini mama yake hakuwahi kumpa habari mbaya za upande wa baba yake. Kila siku alivyokuwa mdogo mama yake alikuwa anamwambia habari nzuri tu, jinsi baba yake alivyokuwa na akili sana na jinsi yeye Obama alivyorithi akili za baba yake.

Barack Obama mtoto akasema mpaka baadaye alivyokuwa mkubwa ndiyo akaja kusikia habari mbaya za baba yake kutoka kwa watu wengine, lakini si kutoka kwa mama yake.

Nikapata kuheshimu sana saikolojia kubwa ya mama yake Barack Obama. Aliona haina maana kupanda mbegu ya chuki kwa mtoto. Hii ni moja ya sababu Obama alikuwa na amani kuliko ilivyotakiwa, ingawa hakukua na baba yake mzazi.

Huyu mama alikuwa na hekima sana. Unaweza kuona imekuwaje mwanawe ameweza kupambana na maisha mpaka kaja kuwa rais wa Marekani bila ya kupata malezi ya baba mzazi.

Huu ni mfano mzuri wa kuigwa. Siyo mama kagombana na baba, watoto wanalishwa sumu kisaikolojia mwanzo mwisho.
 
Mtasingizia maneno bureeee, wanaume mnajitenga sana malezi ya watoto.
Busy na simu mkisogelewa wakaliii muda wote yupo na mama ataachaje kumpenda na kumsilikiza mama.
Sio kina Mama wote
Kuna ndugu yangu aliachwa na mamaye akiwa na miezi miwili
Amekuwa ana shule na kazi nzuri
Hapatani kabisa na mama yake
 
Mkuu fanya utafiti vizuri then uje na mrejesho,,ngoja nikupe hint watoto huwapenda mama zao coz wanapata upendo kutoka kwa mama zao,,baba zao hawawajali na wako so cruel baadae wazee kama hawa ndio hufa wakiw peke yao uchochoroni,mwsho nakupa quotes

"I respected my father but i loved my mother"
......adolf hitrel.....

Sikiliza nyimbo ya 2pac inaitwa dear mama,kuna sehemu anasema mzee wake alipokufa yy hakuumia kabisa "coz my anger wouldnt let me feel for a stranger"
 
Jana nilikuwa naangalia interview mpya Barack Obama amefanyiwa na David Letterman. Ipo Netflix.

Walipozungumzia famikia, upande wa wazazi, Obama akasema mama yake alikuwa very generous.

Alisema kwamba ingawa baba yake aliachana na mama yake, lakinibmama yake hakuwahi kumpa habari mbaya za ipande wa baba yake. Kila siku alivuokuwa mdogo mama yake alikuwa anamwambia habari nzuri tu, jinsi baba yake alivuokuwa na akili sana na jinsibyeye Obama alivyorithi akili za baba yake.

Barack Obama mtoto akasema mpaka baadaye alivyokuwa mkubwa ndiyo akaja kusikia habari mbaya za baba yake kutoka kwa watu wengine, lakini si kutoka kwa mama yake.

Nikapata kuheshimu sana saikolojia kubwa ya mama yake Barack Obama. Aliona haina maana kupanda mbegu ya chuki kwa mtoto. Hii ni moja ya sababu Obama alikuwa na amani kuliko ilivyotakiwa, ingawa hakukua na baba yake mzazi.

Huyu mama alikuwa na hekima sana. Unaweza kuona imekuwaje mwanawe ameweza kupambana na maisha mpaka kaja kuwa rais wa Marekani bila ya kupata malezi ya baba mzazi.

Huu ni mfano mzuri wa kuigwa. Siyo mama kagombana na baba, watoto wanalishwa sumu kisaikolojia mwanzo mwisho.
Nakubaliana na wewe,mimi ni baba na nina watoto ninaona haya mambo ndani ya familia yangu,lakini ni vigumu sana kubadilisha hii kitu,wanawake ni watu wenye ushawishi mkubwa sana,siwalaumu ndivyo walivyoumbwa...
 
Hii tabia ya wamama kupandikiza chuki watoto wamchukie baba yao kwa sababu ya wao kutofautiana nimeishughudia kwa macho yangu . Ukiangalia utagundua ameamua kuwatumia watoto kwa maslahi yake binafsi . Yaani kama kawauzia kesi wao ili liwe ni suala la familia nzima . Wale watoto wanaoingia kwenye mtego huu wanjichunguze sana na wabalace issue nzima kama si jitihada za baba wasingezaliwa pamoja na mama kuwa na jukumu kubwa la kubeba mimba na kuzaa . Hivi mtoto wa kiume unamchukia baba yako kisa umesikiliza maneno ya mama yako una akili kweli ? Kwa nini usimwambie kesi yenu inatakiwa isuluhishwe na wakubwa kwani mzigo unaopewa ni mzito sana ? Je, siku baba yako akikataa kushiriki arusi yako wakati unaoa utamwambia mchumba wako kuwa mama ameniambia baba yangu ni mbaya sana kwa hiyo ndio maana hatukumshirikisha atakuelewaje .
 
Ni kwa sababu 100% mtoto kama hawajambadilisha hospital ana uakika huyu ndo mama yake.

Mnachapiwa kisa muitwe baba, mtoto unajua kabisa sio wako ila kwa kuwa ulishawaambia ndugu kuwa ni wako unakufa kiume.mwanangu, mwanangu....

Kitanda hakizai halamu, kwenye uwezo wa kutoa matumizi ndo baba.

Mama ni mama, nani kama mama.

Baba ni baba ila sometimes sio baba.

Wenye janga kubwa hilo ni wale ambao hawana ndoa rasmi, ila na kwenye ndoa linawakumba ila kwa asilimia ndogo.

NOTE: sio wote jamani naomba munielewe.
Day after day napambana na hali ya kuwachukia wanawake hakika!
 
Kumekuwa na utaratibu wa wanawake wanapokuwa katika migogoro na waume zao kuwalisha maneno watoto ili wamchukie baba yao matokeo yake watoto wanakuwa kiburi wanafuata maneno ya mama yao.

Wanakuwa jeuri shule hawaendi kwakuwa mama anawapenda sana wapo tayari kusema uongo kumlinda mama yao.

Wazazi tuwe makini katika hili kuwapaka mavi wanaume wenu huku mkijificha kwenye migongo ya watoto.
Hili ni janga kubwa sana na linawahusu wanawake wengi sana... WAKIKOROFISHANA NA WAUME ZAO, BASI NIKUMSEMA VIBAYA BABA YAO MBELE YAO... na huwa wanajitahidi kuwasadikisha watoto kuwa BABA YAO NDO LUSIFA
 
Siku hizi wamama full kwenye facebook na instagram na whassup groups,watoto wanapenda baba dhao thana kuliko mama dhao kwani ndio wana muda nao.
Namalizia Kwa ile sentensi pendwa. POVU RUKSA. From....... Hole country.
 
Kama baba ni kulaa kulala au Mke wake kamzidi kipatoo hayoo Mambo ndo huwa yanatokea sanaa..!! Lakini kama baba mtafutaji na ana hela kuliko mama hata heshima inakuwepo yanii... Ndo maana wazee wenye akili wanataka Kama una shida usimwambie mama amwambie baba kuwa unashida ya helaa..Muombe mzee direct... Hii inaanza toka ukiwa mdogo mama akikupa kitu japo ni baba alileta wew utadhni kuwa ni mama ndo katoa...
 
Back
Top Bottom