Watoto kumsikiliza zaidi mama yao kuliko baba ni machungu

Kumekuwa na utaratibu wa wanawake wanapokuwa katika migogoro na waume zao kuwalisha maneno watoto ili wamchukie baba yao matokeo yake watoto wanakuwa kiburi wanafuata maneno ya mama yao.

Wanakuwa jeuri shule hawaendi kwakuwa mama anawapenda sana wapo tayari kusema uongo kumlinda mama yao.

Wazazi tuwe makini katika hili kuwapaka mavi wanaume wenu huku mkijificha kwenye migongo ya watoto.
watoto wako wanamsikiliza zaidi mkeo zaidi yako? mbona ni shida? mimi hilo kwangu halipo hadi sasaivi wananisubiri nirudi home kwa hamu na nikifika ni kwamba Baba amefika, wananipenda, ninawapenda na kuwaelekeza na vilevile wanaheshimu kuwa hapa kuna baba kaingia. fimbo wanakula vilevile, zawadi wanapata vilevile, nikilala nje wanashinda wakiuliza baba anarudi lini tumemmisss...upo hapo?
 
wale walio kwenye ndoa muda mrefu watalikubali hili. Mama anawachochea watoto kuwa watakuja kuletewa mama mwingine ili aje kuwatesa, wanamuona baba yao kana gaidi
 
Baba ukiplay part yako vizuri hayo maneno ya sumu wanaolishwa na mama yao hawawezi kuyaamini.
Wanaume wengi hatupendi kuwa karibu na familia, ww ukifika ukali tu, mtoto kakosea kidogo fimbo, hujui maendeleo ya mtoto shule, mtoto anaomba hela ya daftari chenga nyingi kesho inakuwa kesho, ukifika nyumbani hata ukikuta watoto wanaangalia katuni, unabadilisha unaweka mpira, matusi na kuna wakati unagombana na mkeo watoto wanaangalia kwahiyo hata wanapolishwa maneno lazima waamini.
Tukiwa wastaarabu na kupenda familia zetu hayo maneno ya chuki hayawezi penya kwa watoto hata watoto wakiambiwa hawawezi kumuamini mama yao.
Ni hayo tu
ila kweli mkuu tutimize wajibu wa kimalezi
 
Kati ya Ujinga mrefu ndo huo,, kindly wamama hawawafundishi kwa kuwaambia direct baba yenu mmbaya ila wanaplay victim hao usiombe yaani anaeka ile picha kwamba amenyanyaswa japo inawezekana kweli lakini sio busara Kujionyesha kwa mtoto wakati mwingine wanaondoka wenyewe makwao lakini huko waendako Sasa na watoto shida zote wanawaangushia watoto Kwani ulifukuzwa, baba ananafasi kubwa sana kwa watoto hata kama mna tofauti
 
Kati ya Ujinga mrefu ndo huo,, kindly wamama hawawafundishi kwa kuwaambia direct baba yenu mmbaya ila wanaplay victim hao usiombe yaani anaeka ile picha kwamba amenyanyaswa japo inawezekana kweli lakini sio busara Kujionyesha kwa mtoto wakati mwingine wanaondoka wenyewe makwao lakini huko waendako Sasa na watoto shida zote wanawaangushia watoto Kwani ulifukuzwa, baba ananafasi kubwa sana kwa watoto hata kama mna tofauti
Wewe mwanamke una akili sana big up
 
Nikweli kabisa ushahidi ninao mimi kwa mama mkwe wangu hadi muda huu ndoa yangu na mwanae iko 25/100% hatarini!
 
Mama atabaki kua mama tu
Binafsi pamoja na huu uzee wangu nakiri mama ananafasi kubwa ya kiushawishi kuliko baba.
Yote haya yanasababishwa na vitu vidogo ambavyo baba huvipuuza na mama kutumia fursa kujipatia maujiko hatimaye watoto huwa na mapenzi naye
 
Back
Top Bottom