Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 51,991
- 69,386
True kabisa tena na mnavyowafundisha watoto kujenga chuki dhidi ya baba kisa tu ugomvi wenu, kimsingi hilo jambo sio zuri aidha litawaathiri kisaikolojia au baadae na pia utawapandikiza roho ya kisasi na chuki jambo ambalo kwa watoto sio vizuri...Kweli na hasa sisi wanawake. Tunapenda sana kujihesabia haki jamani.
Mkigombana yamalizeni kiutu uzima na sio kuwahusisha watoto kwa kuwa haileti taswira nzuri kifamilia na hata mbele ya jamii inayokuzungukeni..
Kesi za namna hii husababisha watoto kumsikiliza Mama tu na hata wakati mwingine kumpuuza/kumdharau Baba mzazi kisa tu, Mama aliwaambia watoto wamchukie Baba..
Hili jambo hupelekea mmomonyoko wa maadili(heshima/ustaarabu) kutokea kwenye jamii yetu kutokana na kuwa watoto wamekosa malezi ya upande wa mzazi wa kiume kitu ambacho sio kizuri..
Kiuhalisia mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote wawili na pia sio vyema kujenga mazingira ya kumchukia Baba au kuchukiana miongoni mwa wanafamilia.. Tuboreshe mahusiano yetu ya kifamilia tuishi vyema...Migogoro iwe sehemu ya kujifunza na tusiiendekeze,tuonyane na turekebishane kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla hasa kwenye suala la Maadili mema