Dini inayoua na kuchinja wasio wa Imani Yao.
Ukifuatilia vizuri utagundua Makhawarij wa ISIS wameua waislamu zaidi ya wasio waislamu, hivyo argument yako sio sahihi.
Kisa ili itawale yenyewe.
Itawale nini? Mioyo ya watu? Dunia? Kitabia? Moral Guidance? Au Sheria za Allaah ziwe juu? Juu ya hayo Tambua Halazimishwi mtu kuingia ktk Uislam.
Bahati Mbaya zaidi ikishamaliza makafiri inaanza kujiua wenyewe Kwa wenyewe.
Wapi Makafiri wamemalizwa? Una maana dunia ya sasa ina waislamu watupu ndo maana wanauana wao kwa wao? Zipo sehemu ambazo majority ni muslims na zina conflicts zinazopelekea kuuana, je zote ni za kidini? Hujaziona Siasa za Misri, Syria, Iraq zinavyoshape machafuko ambayo nyie mnayaona ya kidini? Above all Uislam una sheria zake na wote watakaoenda kinyume na Sheria hizo wako makosani regardless ya Imani yao, Rangi au utaifa, Si jukumu langu au Wewe kuwahukumu hilo ni la Allaah, bali jukumu letu kuwalingania wabaki ndani ya Sheria. Ni haramu kumwaga damu ya muislam bila ya kosa la kisheria, ni haramu kuua asie Muislam bila ya kosa la kisheria, ni haramu kuingia ktk vita muislam bila ya Taratibu maalumu zilizowekwa na Sheria ya dini ikiwamo ya ulazima wa waislamu kuwa chini ya Kiongozi mmoja anaewaongoza, Sheria hii pekee inawatoa BH, Al Shabab, Al Qaeda, Hamas na wengineo ktk twaa na wanapaswa wajirudi na kuamiliana na Kiongozi wao wa nchi mpk watakapopata taufiq ya kiongozi mmoja atakautuunganisha dunia.
Kweli hii inawasilimisha wengi Na inaenea Kwa kasi Kubwa Kwa kumaliza Wengine.
Kusilimu au kutosilimu ni matakwa ya mtu, Halazimishwi mtu katika uislamu, Imani Ipo moyoni mwako ikithibitishwa na vitendo vyako, ni juu Yako kuitumia akili yako kuvipitia Vitabu vyote Vya dini tofauti na hapo moyo wako utakapogota na ukaamini khair. Kumbuka tu ipo Siku ya mwisho ambayo Mola wetu atadhihirisha wazi nani Kweli aliamini, akapatia na nani aliekosea na kuiendea Njia yenye kuangamiza.
May peace be to the believers of Haq