Upotevu wa Watoto, Waziri Katambi atoa kauli

Upotevu wa Watoto, Waziri Katambi atoa kauli

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,361
Reaction score
18,645
Serikali imetoa kauli juu ya suala la upotevu wa watoto ambao umekua ukiripotiwa katika Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii ambapo imewaasa wazazi kuwa makini na kushiriki ipasavyo ulinzi wa watoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya elimu na michezo.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobass Katambi akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Unguja, Shadia Haji Omar aliehoji upotevu wa watoto na hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi na upatikanaji wa taarifa zitakazosaida upatikanaji wa watoto hao.

Waziri Katambi amesema pia serikali iko mbioni kuwa na mifumo maalumu ya kiusalama ya kufuatilia matukio mbalimbali ikiwemo kamera maalumu kwenye maeneo mbalimbali ambazo zitasaidia upatikanaji wa watoto hao pamoja na Mali zilizopotea.
 
Back
Top Bottom