Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,597
Wanabodi,
Naangalia TBC, vipindi maalum kuelekea miaka miwili ya rais Magufuli madarakani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini, TIC. Geofrey Mwambe, na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Gedfrey Simbeye, wamempongeza rais Magufuli kwa hatua mbalimbali anazochukua katika kuelekea kuijenga Tanzania ya viwanda, vita dhidi ya rushwa na ufisadi, na vita vya ulinzi wa rasilimali za taifa, anaboresha zaidi mazingira ya biashara nchini, hivyo Tanzania kuendelea kuwa ni nchi kivutio izaidi kwa wawekezaji.
Mwambe amesema, tangu Magufuli ameingia madarakani, wawekezaji wameongezeka na hukuna hata mwekezaji mmoja aliyekuwepo ameondoka, na kwa hatua hizi anazoendelea kuchukua kulinda rasilimali zetu, wawekezaji serious wataongezeka.
Simbeye amesema kitu cha kwanza rais Magufuli alichofanya baada tuu ya kuingia ikulu ya Magogoni, mkutano wake wa kwanza ni kuzungumza na wafanyabiashara ikulu. Rais amewahakikishia wafanyabiashara wote genuine, mazingira mazuri ya kufanya biashara, na hatua alizochukua kwenye vita dhidi ya rushwa, na ufisadi, hizi hatua anazochukua sasa kulinda rasilimali zetu kwa kubadili sheria na kujadiliana upya na wawekezaji ili Tanzania tufaidike zaidi, kutavutia wawekezaji serious ambao wawekezaji hao watafaidika na Watanzania tutafaidika.
NB. Kuna tatizo nimelinote humu jf kwa baadhi yetu, wanachukia na kukasirika kila rais Magufuli akipongezwa kwa mazuri yoyote. Wao kazi yao ni kupinga tuu kila kitu. Naomba kutoa hoja, kwa vile wanaompongeza rais Magufuli, wanampongeza kwa hoja, hivyo naomba wale wote wanaopinga pongezi hizi kwa rais Magufuli kuhusu uwekezaji, pingeni kwa hoja na sio tuu kupinga kwa chuki!.
Nawaomba sana wana jf, tuwe objective katika kulitendea haki jukwaa hili, kwa kubishana kwa hoja, kwenye mazuri tupongeze kwa hoja na kwenye kukosoa, tukosoe kwa hoja.
Jumapili Njema.
Paskali