JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Tukio hilo limetokea tarehe 18 Februari 2024 majira ya saa tatu usiku wakati mtu huyo aliyejifanya mganga wa jadi alipofika nyumbani kwa familia ya Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibia mke wake Fatuma Abdalla (52) aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la miguu. Aliwanywesha dawa iliyowalewesha familia nzima, wakapoteza fahamu na akawaibia simu 5 za mkononi na kuondoka.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mganga huyo pia limemkamata kwa mahojiano mtu mmoja anayefamika kwa jina la Jalala Ally Said anayedaiwa kushirikiana na mganga huyo.
Wagojwa walilazwa na kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni mpaka sasa wagonjwa 13 wamesharuhusiwa na wengine watatu waneendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Tukio lingine limetokea tarehe 9 Februari, 2024 huko eneo la Tuangoma, Mbagala ambapo mtu mmoja aliyejifanya mganga wa jadi aliwanywesha dawa zilizowalevya na baadae kupoteza fahamu watu watano na kuwaibia pikipiki namba MC474, simu 3 za mkononi na Tsh 30,000.
Jeshi la Polisi linawatahadharisha wananchi kuhusiana na kuwepo kwa watu wanaojifanya waganga wa jadi ambao huwalewesha watu na wanafamilia kwa ujumla na baadae kuwaibia.