Ajali ilivyoua wanafamilia watatu wakienda kuzika Dar

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1698764107425.png

Watu watatu wa familia moja wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana mkoani Mtwara huku ikibanikia watatu hao ni familia moja waliokuwa wanakwenda kwenye maziko jijini Dar es Salaam.

Dereva aliyekuwa anaendesha gari iliyokuwa imebeba wanafamilia hao anadaiwa kukimba huku moja wa mashuhuda wa ajali hiyo Juma Zuberi akisema kuwa ni ngumu dereva kutoroka kwa kuwa naye alikuwa mwanafamilia na pia mwanamke aliyefariki ni mkewe.

Amesema kuwa katika msiba huo dereva amepoteza mkwe na mke ambapo inaonyesha kuwa alipata kiwewe kilichomfanya akimbie.

“Siyo jambo dogo umebeba familia ya watu saba alafu unaiangusha na unaua ndugu zako akiwemo mkeo na baba yake unashuhudia inauma na inachanganya nafikiri alichanganyikiwa,” amesema Zuberi.

Sarah Mgumba ambaye ni majeruhi, amesema kuwa alipokea taarifa ya mama yake mzazi kufariki akiwa njiani hivyo wakajiandaa kuwahi maziko ndipo walipata ajali.

“Nimefiwa na mama Dar es Salaam nilipopata taarifa nilifanya mawasiliano na ndugu yangu waliniambia kuwa wana usafiri tukiwa watu wanane na dereva wote ni ndugu tulitoka kwa pamoja ili tuwahi msiba, sijui chanzo cha ajali nilichoshtukia ni ajali nachomolewa kwenye gari nikiwa na majeraha,” amesema Mgumba.

Habiba Selemani ambaye ni majeruhi amesema kuwa walipata taarifa ya msiba wa wifi yake ambapo aliwasiliana na watoto wa kaka yake ili kuwahi maziko ya mama yao.

“Tulikuwa tunakwenda msibani wifi yangu amefariki, ikabidi tukusanyane ndugu ili tuweze kuondoka tuwahi maziko, tulipofika Mikindani nilisika mlio hata sijui nini kilitokea yaani shemeji yangu, ndugu yangu, mke wa mtoto wetu pia walifariki hapo hapo,” amesema Selemani.

Majeruhi mwingine Mohamed Yusuph amesema kuwa alijikuta akiwa chini tayari wamepata ajali, hakuhisi chochote wala kuona chochote alijikuta tayari amepata ajali.

“Kwa kweli sikumbuki nilijikuta nikiwa tayari chini nimepata ajali imetokewa nilikuwa nawahi mazishi, lakini baada ya ajali nilishuhudia watu watatu wakipoteza maisha ambao ni shangazi, mjomba na shemeji yangu iliniuma kwa kuwa tulikuwa tunawahi mazikoni,” amesema Yusuph.

Deogras Peter ambaye ni majeruhi na dereva bodaboda, amesema kuwa alikuwa upande wake na alikuwa akitokea Dangote kuja mjini ndipo akakumbana na ajali hiyo.

“Nilikuwa natokea Dangote kuchukua mzigo nilipofika kilimani nikaona kuna gari ya Dangote imepaki wakati nataka kuipita kuna gari ndogo ikatoka kwa nyuma ikiwa katika mwendo kasi na kwa kuwa tulikuwa upande wetu alishindwa akatupiga ubavuni na kuturusha kwenye mtaro,” amesema Peter.

Kufuatia ajali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abbas ametoa pole kwa familia hiyo ambayo imepoteza watu watatu.

“Wanasadikiwa kuwa walikuwa ni familia moja na walikuwa saba wakielekea msibani ambapo watatu walifariki na wengine walipata majeraha kwa niaba ya Serikali nitoe pole nyingi niwaombee wapone haraka tunaungana na familia hiyo kuomboleza msiba huo ambapo baadhi ya majeruhi wapo katika Hospitali ya Kanda ya Kusini wakipatiwa matibabu,” amesema Kanal Abbas.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Mtaki Kurwijila alidhibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni Mwanaidi Selemani Ahmed (51), Mohamed Mfaume Mtumanuma (60) na Niale Ally (32) wote wakazi wa Wilaya ya Mtwara.

MWANANCHI
 
View attachment 2799192
Watu watatu wa familia moja wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana mkoani Mtwara huku ikibanikia watatu hao ni familia moja waliokuwa wanakwenda kwenye maziko jijini Dar es Salaam...
Tuna jamii ambayo haijali Wala haitaki kuheshimu ustaarabu wa barabarani ,tutaoshia kufyekwa hivyo hivyo.
 
Mungu awafanyie wepesi majeruhi na awape faraja, Marehemu wapumzike kwa amani.
 
Mi nasema tena, hizi siyo ajali. Kusafiri barabarani nchi hii kumekuwa kama ugonjwa endemic wenye mortality rate kabisa.
 
Barabara hizi ni konyo sana, unaweza ukawa unaendesha zako kistaarabu kabisa unafata sheria na discipline ya juu kwenye barabara ila mwendawazimu mmoja na papara zake za mwendo anakuwaisha kwa sir God.
 
Ila chuma za dangote nazo zinahusika sana na ajali ya njia hiyo ya mtwara.
 
Back
Top Bottom