Watasambaratishwa, watakwisha wote.....

Watasambaratishwa, watakwisha wote.....

Watanzania unafiki ndo unatufanya turudi nyuma kila siku kuogopana na kulindana, mtu mkweli kama lema kwangu atabaki shujaa wa maisha yangu yote

kaka umenena iliyokweli toka rohoni.
pamoja saaaana!!!
 
Watu hawajaijua vizuri demokrasia, kila mtu anajaribu kugusa juu juu tu ili mradi apate pa kuanzia.

Tupo kwenye Operation kali ya kuondoa wale wote waliokuja kwenye nyumba yetu kimakosa, wakiweza warudi walikotoka au watafute makazi mengine mapya. Hapa tutaanzia ngazi ya chini kabisa ya ukoo wetu mpaka mwisho wake, tutapembua pumba zote na kuhakikisha tunabaki na ngano safi bila kujali itatugharimu kiasi gani.

NIA YA KUFANYA HAYA YOTE TUNAYO, SABABU ZA KUFANYA HIvI TUNAZO NA UWEZO WA KUYATEKELEZA HAYA TULIYOYADHAMILIA TUNAO..
Demokrasia ni gharama sana na tutainunua hata ingekuwa ghari kiasi gani. Demokrasia inapozidi kukua ni ghari zaidi lakini hatutajali kugharimu hata maisha yetu lakini ipatikane.

DEMOKRASIA NI UHURU WA MAWAZO UNAOZINGATIA MISINGI NA KANUNI ZA WAPENDA DEMOKRASIA HAO.
Mawazo hasi kama haya ndiyo yanayojenga makundi na mifarakano ndani ya CHADEMA.

Kuna watu wengine kama wewe wanafikiri CHADEMA ni yao na ndiyo nyumba yao wakiwa ndiyo Baba na Mama huku wale wengine wakiwa ni watu wa KUJA, KUJILETA au KULETWA.

Hebu fikiria mtu anayedhani CHADEMA ni yake halafu wewe wa 'KUJA' umwambie kuwa anachokifanya hakifai na kiko nje ya taratibu, kanuni, itifaki na katiba. Kwanza hawezi hata kukusikiliza na ukizidisha kelele atakachofanya ni kukufukuza kwenye chama "chake" katika misingi hiyo hiyo ya uvunjifu wa taratibu, kanuni, itifaki na katiba na huwezi kupata nafasi ya rufaa wala msamaha. Rufaa na msamaha utatoka wapi wakati hukumu ni batili.

Mentality kama hizi haziwezi kukifanya chama kikawa na demokrasia pana inayowafikia wale wenye inferiority na mtazamo huu.

Chama ambacho kina misingi ya demokrasia, wanachama ndiyo wenye chama na katika wanachama hao, hakuna anayejulikana kama niwa KUJA, KUJILETA NA KULETWA kwa sababu kila mwanachama ana haki na uwezo uliosawa. Hakuna kura za VETO ndani ya vyama vya demokrasia. Hakuna kura inayoyoizidi kura ya mwingine na hata maamuzi lazima yafanyike kwa kura au makubaliano ya wanachama.

Hii uliyoleta hapa ni pumba kisiasa hasa pale unaposimama kwenye majukwaa na kudai CHADEMA ni chama cha Demokrasia na Maendeleo.
 
Rose Mayemba,
Zogo lilianzia hapa.....
CCM-NCCR-TLP-CHADEMA sasa hapa Godbless J Lema atarudi wapi?
Huyu Mwehu akajibu hivi....
atarudi kwenye kazi yake ya ujambazi
Mimi nikamchapa na hili kofi.....
Hahahaha...mwenyekiti wenu akimaliza kipindi chake cha uongozi atarudi kwenye kazi yake ya kutoa mbwa bandani
Wewe unakuja na hili.... wapi wapi?
rudia tena kusoma na kisha urudie tena naona hujanielewa
 
Last edited by a moderator:
Mawazo hasi kama haya ndiyo yanayojenga makundi na mifarakano ndani ya CHADEMA.

Kuna watu wengine kama wewe wanafikiri CHADEMA ni yao na ndiyo nyumba yao wakiwa ndiyo Baba na Mama huku wale wengine wakiwa ni watu wa KUJA, KUJILETA au KULETWA.

Hebu fikiria mtu anayedhani CHADEMA ni yake halafu wewe wa 'KUJA' umwambie kuwa anachokifanya hakifai na kiko nje ya taratibu, kanuni, itifaki na katiba. Kwanza hawezi hata kukusikiliza na ukizidisha kelele atakachofanya ni kukufukuza kwenye chama "chake" katika misingi hiyo hiyo ya uvunjifu wa taratibu, kanuni, itifaki na katiba na huwezi kupata nafasi ya rufaa wala msamaha. Rufaa na msamaha utatoka wapi wakati hukumu ni batili.

Mentality kama hizi haziwezi kukifanya chama kikawa na demokrasia pana inayowafikia wale wenye inferiority na mtazamo huu.

Chama ambacho kina misingi ya demokrasia, wanachama ndiyo wenye chama na katika wanachama hao, hakuna anayejulikana kama niwa KUJA, KUJILETA NA KULETWA kwa sababu kila mwanachama ana haki na uwezo uliosawa. Hakuna kura za VETO ndani ya vyama vya demokrasia. Hakuna kura inayoyoizidi kura ya mwingine na hata maamuzi lazima yafanyike kwa kura au makubaliano ya wanachama.

Hii uliyoleta hapa ni pumba kisiasa hasa pale unaposimama kwenye majukwaa na kudai CHADEMA ni chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Naona unalazimisha kutokuelewa, kila jambo lina msingi na kila msingi una kanuni na taratibu zake. haijalishi ulikuwepo ama u wakuja tu lakini kuzingatiwa kwa kanuni na taratibu zilizopo ndio matokeo ya mapatano yenu. Na si dhambi kupokea mawazo kutoka mahali pengine na kama wapo wanaoyafanya haya basi ni katika tu mapungufu ya uumbwaji wao. naomba unielewe na wala usinilishe maneno siko kwa ajii ya makundi na hakuna kundi ninalolitumikia ila sitakaa kimya kunena jambo lolote ambalo naamini ni msingi wa yale ninayoyaamini....hao wenye makundi na unauhakika na uwepo wa makundi yao waeleze tu kwa jia njema watakuelewa.
 
Paka keshakuwa pakashume ameunda urafiki na panya na kuanza hujuma, dawa nikuwatimua wasaliti wote.
 
Mawazo hasi kama haya ndiyo yanayojenga makundi na mifarakano ndani ya CHADEMA.

Kuna watu wengine kama wewe wanafikiri CHADEMA ni yao na ndiyo nyumba yao wakiwa ndiyo Baba na Mama huku wale wengine wakiwa ni watu wa KUJA, KUJILETA au KULETWA.

Hebu fikiria mtu anayedhani CHADEMA ni yake halafu wewe wa 'KUJA' umwambie kuwa anachokifanya hakifai na kiko nje ya taratibu, kanuni, itifaki na katiba. Kwanza hawezi hata kukusikiliza na ukizidisha kelele atakachofanya ni kukufukuza kwenye chama "chake" katika misingi hiyo hiyo ya uvunjifu wa taratibu, kanuni, itifaki na katiba na huwezi kupata nafasi ya rufaa wala msamaha. Rufaa na msamaha utatoka wapi wakati hukumu ni batili.

Mentality kama hizi haziwezi kukifanya chama kikawa na demokrasia pana inayowafikia wale wenye inferiority na mtazamo huu.

Chama ambacho kina misingi ya demokrasia, wanachama ndiyo wenye chama na katika wanachama hao, hakuna anayejulikana kama niwa KUJA, KUJILETA NA KULETWA kwa sababu kila mwanachama ana haki na uwezo uliosawa. Hakuna kura za VETO ndani ya vyama vya demokrasia. Hakuna kura inayoyoizidi kura ya mwingine na hata maamuzi lazima yafanyike kwa kura au makubaliano ya wanachama.

Hii uliyoleta hapa ni pumba kisiasa hasa pale unaposimama kwenye majukwaa na kudai CHADEMA ni chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Sikutegemea kuwa chama makini kingefika mahali kila mtu akawa msemaji wa chama. sijui huyu Rose ni nani huko CDM.
 
Mkuu, hata mimi sifahamu cheo chake zaidi ya kusoma hoja zake na kujibu kadri ya uwezo wangu. Ninatumaini kadri mnyukano huu usio na tija kwa CHADEMA unavyoendelea ndivyo tutaona na kusikia mengi.

Yangu ni macho na masikio.
 
sicho nilichokiandika ia nitakujibu kwa kadiri niwezavyo, kwa hii hoja yako ambayo haipo kwenye bandiko langu ni kwamba. chadema ni chama cha wananchi na haya wala si matamko ya chama huu ni mtazamo.
 
huna haja ya kunifahamu maana haitakusaidia
 
Kweli ndio maana wengine waki wakitoa mawazo yao yenye mtizamo usio ungwa mkono na wakubwa wao wanapigwa MATOFALI nakuenguliwa uanachama kabisa! Ili wengine wasijaribu... HIZI NI ENZI ZA " ZIDUMU FIKRA ZA MWALIMU"
 
sicho nilichokiandika ia nitakujibu kwa kadiri niwezavyo, kwa hii hoja yako ambayo haipo kwenye bandiko langu ni kwamba. chadema ni chama cha wananchi na haya wala si matamko ya chama huu ni mtazamo.
.
Tupo kwenye Operation kali ya kuondoa wale wote waliokuja kwenye nyumba yetu kimakosa, wakiweza warudi walikotoka au watafute makazi mengine mapya. Hapa tutaanzia ngazi ya chini kabisa ya ukoo wetu mpaka mwisho wake, tutapembua pumba zote na kuhakikisha tunabaki na ngano safi bila kujali itatugharimu kiasi gani.
Ok, mpo kwenye operation wewe na nani?! Mmetumwa na nani na kwa maslahi ya nani?
 
Rose Mayemba Na kwa vile hiyo nyumba yenu ni ya wote, kuna watu waliokuja kutoka nje, wakasaidia katika ujenzi, na kuna hao watoto waliozaliwa, wakakulia, wakashiriki kuijenga, sasa imekuwa ghorofa, imekuwa imara, kumeibuka ubaguzi kwa upendeleo wa baadhi ya watoto kuwaona kama watoto wa ndoa, na wengine kuwaona kama wana haramu, hivyo mnawatufutia sababu ya kuwatimua kama I/Abrahamu alivyomtimua Hagai na mwanawe Ismail!.

Mkiamua hivyo na kujiona nyumba ni yenu, kujiona kuna wenyewe na wakuja, then, mkimgusa yule mwanenu mpedwa wenu, sisi tunaopendezwa nae, huku nyinyi mkimuonea kijicho kwa mafanikio yake, hivyo kumuundia visa na vituko vya kila aina ili aikimbie nyumba!, au kuamua kumtimua!, mkae mkijua, ataondoka na kulichomoa lile jiwe la msingi kwenye kona nyumba yunu ilipoegemea, hivyo hilo ghorofa lenu litabomoka, muanze upya!.

Nyumba ikibomoka, kuna ambao hawana pengine popote pa kwenda, ndio watalia na kusaga meno!.

Sisi watazamaji, tunawasubiria tuu ile 2015, kuwapa hongera kwa kujaribu tena, na pole kwa kulizwa!.

Nyumba zote unazoziona imara, zimeimarishwa kwa uvumilivu, ustahimilivu na kukubali managing divesity ya watu wenye mawazo tofauti!.

Kwa hii nyumba yetu, hiyo mitoto mnaidekeza na kuivimbisha mabichwa kuwa hao ndio watoto wa ndani, kwa kufikiri ndio mnaisaidia!, mnaipoteza, na ndio hiyo hiyo mitoto, inakuja kuwabomolea nyumba yenu, mlioijenga kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa zikiwemo damu na maisha ya watu!.

Sisi wengine sio wakubwa kihivyo, ila ni wakuu!, asiyesikia la mkuu..!.

Endeleeni.

Pasco.
 
Last edited by a moderator:
Sikutegemea kuwa chama makini kingefika mahali kila mtu akawa msemaji wa chama. sijui huyu Rose ni nani huko CDM.
Gag, kiukweli, kuna mijitu imevimba mibichwa, inajisikia kama hicho chama ni chao, with all the rights kuwaema wengine kwa mafumbo!. Idadi ya wanaohitaji kuadabishwa ni kubwa kuliko nilivyofikiria!.

Pasco.
 
Kwani mbwa koko habweki???!!!!

Ila tofauti yake na trained dog ni ipi?????!!!!
 
Back
Top Bottom