Je, Demokrasia ya Tanzania inaruhusu Misingi ya Uporaji Haki za Raia na Mali zao

Je, Demokrasia ya Tanzania inaruhusu Misingi ya Uporaji Haki za Raia na Mali zao

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,743
Reaction score
1,164
Tanzania, nchi yenye mamlaka kamili iliyosaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa hususani mikataba ya kulinda haki za binadamu na ulinzi wa rasilimali za umma imeacha misingi hiyo,na sasa inajinadi kuwa na Demokrasia yake na tamaduni zake.

Kwa kuwa lengo ni kukuza aina mpya ya Demokrasia ya Tanzania na utamaduni wake mpya,Haina budi sasa kuvunja mikataba ya Kimataifa na kujiondoa kwenye nchi zilizostaarabika kwa kuunda jumuiya ya nchi za Kiimla Duniani,ili kuikuza misingi ya tamaduni na Demokrasia yao!

Ili kuondoa dhana ya kuomba misaada kama kigezo Cha Demokrasia wakati wakiimplement Demokrasia yao ni vyema sasa kuvunja Mikataba yote ya amani iliyofunga na kujiondoa kwenye uwanachama wa umoja wa mataifa ili isiwe kigezo Cha kuwa mnufaika wa umoja huo.

Nachelea kusema hivi kutokana msisitizo wa Rais aliyehodhi mamlaka ya wananchi bila ridhaa yao kwa mujibu wa ibara ya 8 ya Katiba,kuendelea kuinadi Demokrasia yake mpya inayopingana na maudhui ya misingi ya Demokrasia.

Serikali yake inalazimisha wananchi kufuata aina mpya ya Demokrasia na utamaduni mpya kama anavyoinadi kwenye hotuba zake kwa Taifa,akiaminisha watu wazoe kuokota maiti Kila kukicha,kupora mali za umma,wazoe kutokosoa fikra sahihi za mtawala,kuteka watu,kuzua
taharuki na kudhoofisha umma kwa hofu ya tawala zisizoguswa.

Kwa muktadha tajwa hapo juu Watanzania wamegubikwa na gonjwa kubwa la Kisaikolojia Stockholm Syndrome,linaloathiri uwezo wa kuchanganua mambo kutokana na msongo wa mawazo wa kusababishiwa na kuzoea Hali ya vitisho na kuona Kila ovu ni msingi wa utawala wa mabavu,ukihoji utakufa!

Ndiyo maana mapokeo ya wananchi kuhusu Serikali na Demokrasia mpya yanswajenga katika Hali ya hofu na uoga kupindukia,kwa kujiuliza chini ya kapeti hii ndiyo Demokrasia tuliyoizoea!

Na kama ndiyo Demokrasia mpya ya Kitanzania watueleze upi utofauti wake na Demokrasia tuliyoizoea na kukubali kuingia mikataba ya kidunia kuitekeleza.

Kama ndivyo,kwanini tunatumia gharama kubwa ya kutengeneza kikundi Cha kuitetea serikali huko kwa mabeberu kwa msingi wa kutaka Kodi zao,ili kuimarisha ubaya wa serikali yetu.

Wakati wanafanya haya wanapaswa wakumbuke kuwa Mwalimu Nyerere alisistiza siasa na maisha ya watu kama kigezo Cha kuleta maendeleo,akataja mambo makuu manne ili tuendelee tunahitaji watu,ardhi,siasa safi na uongozi Bora,aliyesema haya akiamini misingi ya Demokrasia hii inayopingwa na watawala kwenye chama alichokiasisi.

Mfumo wa Demokrasia mpya hauonyeshi thamani ya kusimamia misingi ya haki ya asili ya watu,kama sehemu ya mkakati wa maendeleo,ndiyo maana kwao kupoteza halaiki ya watu ili kuzuia madai yao ya haki inaonekana ni jambo la kawaida sana katika utamaduni mpya unalazimishwa kuzoeleka

Demokrasia hii mpya imeweka uhuru wa mipaka,ambayo ni tabia za kidikitekta. Lakini pia imenyang'anya haki na mamlaka ya wananchi kuziweka serikali madarakani kwa mujibu wa katiba.

Kimetengenezwa chombo Cha uchaguzi kilichopewa mamlaka ya kumpigia kura kwa niaba ya wananchi,Hali iliyopelekea msingi wa ushindi wa 98% ya kura zaidi ya milioni 30,bila ya wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi.

Tume hiyo imetengeneza uhalali wa kuunda serikali kwa nguvu ya mtawala kinyume na Demokrasia halisi inayotoa mamlaka ya kuziweka serikali kuwa mikono mwa wananchi.

Hivyo utaona kuwa Utamaduni mpya unao nadiwa na watawala ndiyo chachu ya kutengeneza DEEP STATE iliyohodhi mamlaka ya watu,kuzuilia sauti za watu na kubuni mbinu mpya zaidi ya ukabaila inayotumika kupora ardhi kama mtaji wa wananchi na kuukabidhi kwa watu wachache wenye ukwasi mkubwa ambao Mwalimu aliuita mfumo wa Kishetani.

Tokeo hili limesababisha migogoro mingi ya kiutawala na kuwafanya wananchi kuwajibika kwa watawala, kinyume kabisa na takwa la Katiba ibara ya 8 kuwa serikali itawajibika kwa wananchi.

Hali hii inasababisha kudhoofisha uwezo wa wananchi kuihoji na kuikosoa serikali (untouchable government) kwa kuiogopa na kukubali kupokea mamlaka yao ya kikatiba,Hali inayopelekea kudhulumiwa haki za na kunyang'anywa ardhi kama kigezo Cha kudhoofisha uchumi wao,ikiwa ni mbinu ya kudhoofisha nguvu ya mapambano ya haki na kujikita kusaka fursa za maisha ya mkate wa siku,inayofungua wigo mpana wa uchawa ili mkono uende kinywani,bila kujali yanayoendelea nchini na kujua haki yao kama wananchi.

Ardhi imehodhiwa na serikali ambayo ndiye mdhamini mkuu na Moja ya kazi kubwa iliyojipa ni kuimilikisha kwa wawekezaji chini ya udalali wa serikali kuu.

Hali hii imezua migogoro isiyoisha dhidi umma uliodhulumiwa haki ya asili ya umiliki wa rasilimali hizo,mfano Ngorongoro na kwingineko kote,kwa kutumia nguvu ya vyombo vya dola vyenye uwezo wa kunyamazisha wananchi.

Matokeo yake maendeleo ya umma yanahodhiwa na kikundi kidogo Cha Deep State iliyojimilikisha uchumi wa nchi na madaraka ya serikali kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Tumeharibu msingi ya siasa za kistaarabu kwa kuigeuza siasa kuwa kimbilio la watu wachafu wenye miliki ya uovu unaolindwa na dola,tukisahau siasa ni mfumo wa maisha uliokubaliwa na watu katika kuendesha maisha yao.

Ndani ya siasa mpya na Demokrasia mpya unaibuka utamaduni usiojali maisha ya watu,wananchi wanauwawa ovyo,ardhi inaporwa,siasa ya utengano na uongozi usiothamini haki za asili za binadamu zaidi ya kulinda mfumo unao nufaisha wachache waliojipachika madaraka.

Hali hii ya uvunjivu wa makusudi wa haki za binadamu umewafungua macho watu na wahisani wakubwa wa nchi yetu na kuumizwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wa kunyang'anya uhai wa wananchi kwa sababu ya madaraka yaliyopora mamlaka ya wananchi.

imewakera wenzetu wa Ulaya na Dunia nzima waliostaarabika na kukubali kuwa sehemu ya umoja wetu,sasa wamesimama kujaribu kutibu gonjwa kubwa na cancer ya msongo wa mawazo inayowasumbua Watanzania ya kuogopa kuhoji matendo maovu ya serikali iliyokosa uhalali kwa kutochaguliwa na wananchi.

Mabunge ya Ulaya yanayotumia Kodi za wananchi wao wameliona hili baada ya kuondoa tambara lililofunika macho la 4R's, lililotumika kama kiini macho na kuhodhi mifumo ya kudhibiti watu,ardhi,siasa safi na uongozi unaotokana na wananchi.

Matukio yameathiri kwa kiwango kikubwa sana maisha ya wananchi kutokana na matendo yaliyokithiri ya utekaji umwagaji damu ni zaidi ya matukio yanayoendelea kwenye nchi zilizo vitani,yanatengeneza vikundi vya uhasi dhidi ya utaifa wao kwa sababu mtawala ameamua kuhodhi mpaka mamlaka ya uwezo wa akili za watu kufikiri.


Ni wakati sahihi kwa wananchi wenye afueni ya ugonjwa wa cancer ya hofu kupewa ushirikiano ili waweze kusimama na kuwatibu wenzao katika kujenga nguvu ya umoja itakayoondoa mfumo kandamizi unaokandamiza mamlaka ya wananchi.


Makundi mbalimbali ya haki za binadamu na asasi za kiraia zisimame imara kuungana na wenye mrengo wa kuikomboa nchi kwa kuwa vita hii ya uhuru wa mamlaka ya wananchi ni kubwa sana kuliko vita ya kumuondoa Mkoloni,ambaye Leo anaombwa misaada ili watukandamize kwa Kodi za wananchi wa Mataifa yao,katika kuneemesha familia za watawala na kuimarisha mifumo ya ukandamizaji.


CCM inatumika kama kichaka,lakini wenye mfumo wao wapo kazini wakichagizwa na mapambio ya wanachama wao wasiojia A Wala B lakini tukitaabika nao kwenye maisha ya kusababishiwa na watu wachache.


ANC kufikia hapo ilipo ilisimama kwa msingi ya umoja wa wanachama wao Kama alivyo Mzee Warioba bila kujali anguko la chama Chao katika kukemea maovu ya Watawala na kukirudisha chama kwa wananchi toka kwenye mikono michafu iliyoruhusu DEEP STATE kuhodhi mamlaka ya wanachama na nchi kwa umoja wake.


Vita hii ni kubwa,wenye akili timamu wataelewa lakini CCM oya oya wataendelea kuwa makaraibya zege na catapilla la kuwasafishia njia wachache waliosheheni ukwasi kwa njia haramu za kujinufaisha kutokana na kupora mali za umma.


Huu ni wakati wa mabadiliko ya kifikra kwa wananchi wote bila kujali vyama vyao,tukisimama imara kuikomboa nchi vyama vitapita mama Tanzania atabaki kwenye mikono salama,tuungane na wenye dhamira ya kweli bila kujali itikadi zetu za kivyama.


Saa ya ukombozi ni sasa.


Mungu ibarikia Tanzania,Mungu ibariki Tanganyika na watu wake
 
Daima nitaipambania nchi yangu ya Tanganyika mpaka kieleweke. Wahuni, mafisadi na wageni kutoka nchi jirani hawatakiwi kutuamulia hatma ya maisha yetu.
 
Back
Top Bottom