Rose Mayemba
JF-Expert Member
- May 7, 2012
- 721
- 1,017
Watu hawajaijua vizuri demokrasia, kila mtu anajaribu kugusa juu juu tu ili mradi apate pa kuanzia.
Kinachowatesa watanzania wengi ni mfumo, maisha waliyoishi hapo awali ni ya uoga na unafiki mkubwa, uongo na uzandiki ndivyo vilivyowakuza na kutawala maisha yao. Ona walivyokosa uelekeo, hawawezi tena kuishi maisha yao bali ya wale waliowatangulia na kuwarithisha uozo wao.
Walikotoka kumewashinda maana walioko wameacha kabisa kuhangaikia maslahi ya wananchi bali ya matumbo na familia zao, wakatafuta njia mbadala ya kuyaishi maisha yao lakini kwa bahati mbaya wakahama na tabia zao( uoga, uongo, unafiki na uzandiki) kuelekea makazi mapya. wapo waliojirekebisha na kuishi kama walivyoyakuta maisha ya ugenini japo pia wapo ambao hawakuelewa dhamira ya kuhama kwao kutoka walikotoka.
Wapo pia tuliozaliwa nao, ambao wamekiuka misingi ya familia kwa sababu waliruhusiwa kucheza na wenzao wawapo nje ya geti letu, kwa bahati mbaya wamerudi nyumbani na tabia za ajabu zisizofikirika, na kwa kuwa wamekiuka na kuvunja maadili ya familia tunawatupia walimwengu atusaidie kulea wakijirekebisha milango bado itakuwa wazi.
Tupo kwenye Operation kali ya kuondoa wale wote waliokuja kwenye nyumba yetu kimakosa, wakiweza warudi walikotoka au watafute makazi mengine mapya. Hapa tutaanzia ngazi ya chini kabisa ya ukoo wetu mpaka mwisho wake, tutapembua pumba zote na kuhakikisha tunabaki na ngano safi bila kujali itatugharimu kiasi gani.
NIA YA KUFANYA HAYA YOTE TUNAYO, SABABU ZA KUFANYA HIvI TUNAZO NA UWEZO WA KUYATEKELEZA HAYA TULIYOYADHAMILIA TUNAO...
Demokrasia ni gharama sana na tutainunua hata ingekuwa ghari kiasi gani. Demokrasia inapozidi kukua ni ghari zaidi lakini hatutajali kugharimu hata maisha yetu lakini ipatikane.
DEMOKRASIA NI UHURU WA MAWAZO UNAOZINGATIA MISINGI NA KANUNI ZA WAPENDA DEMOKRASIA HAO.