Watanzania wenzangu, biashara ya usafiri wa anga (ndege) sio kama Uber jamani

Nimesoma komenti kadhaa hapo juu nahisi wote wanaweza kujibu kuwa "ZIUZWE TU"

Maana hakuna binadamu anayemaliza kipindi chake duniani akaacha taswira nzuri, wote ni kulaumiwa tu but mwisho wa siku hayupo.

Rais gani aliwahi kuendesha nchi kwa kufuata ilani ya uchaguzi ambayo chama ilitembea nayo?
 
Tunapoambiwa ATCL imepata hasara tusibeze sana. Kuna American Express na Delta Lines wanachungulia kaburi! Na Amar hapo UK British Airways imegubikwa madeni nusura izame! Tatizo lenu ni uzungu pori? Ni mashirika ya wenye mafuta kina EMIRATES, QATAR na wenzao Serikali zao zimenunua madeni. Baadhi ya matukio yaliyotikisa biashara ya usafiri wa anga duniani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita:

1. Global Economic and financial crisis (mtikisiko wa kiuchumi na kifedha ulioikumba dunia).
2. Marubani, wahudumu na watumishi viwanjani kugoma Mara kwa mara nchini Marekani, UK, France na Italy.
3. Kodi mpya (carbon tax) kugharamia uchafuzi wa anga.
4. Covid 19 restrictions on travel (masharti ya covid 19)
5. Gharama za utengenezaji ndege kuongezeka mno kutokana na ushindani Kati ya Airbus na Boeing kufuatia mahitaji ya usalama wa abiria.
6. Nchi kunyimana route (protectionism policies).
7. Uendeshwaji mbaya wa airline
8. Kubadilika kwa sura ya utalii. Mfano watalii wengi kuanza kujikita kutembelea nchi au eneo lao, kushuka ari ya kuona wanyama au milima n.k.

Hizi ndio sababu ya mashirika mengi duniani kuendeshwa kwa hasara. Sio lazima éti hasara pawepo na wizi

Licha ya mashirika kufanya vibaya hakuna nchi imefunga shirika lake. KLM ilitaka ijiuze kwa AIR FRANCE wananchi wakaandamana! Serikali ikalazimika kubeba madeni.

Alitalia ya Italy ilitangazwa imefilisika Papa akamwandikia barua Prime Minister kwamba Vatican hairidhii uamuzi! Serikali ikabeba Madeni. Mpaka leo Alitalia ipoipo tu. Ukipatiwa ticket ya Alitalia jiandae for cancellation wakati wowote. Mara nyingi watakuhalishia Easy Jet au Ryan Air.

Sasa kuna mijitu inadhani biashara ya ndege sawa na biashara ya kuuza mashokishoki Darajani!
" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fstatic.xx.fbcdn.net%2Fimages%2Femoji.php%2Fv9%2Ft7f%2F1%2F16%2F1f60a.png&hash=efe739e1e11105d2cb04b5162bb1658d" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> <img src=" title="" width="" height="" />
Kabla ya hapo mlimshauri hivyo alienunua?!!
Kwa nchi masikini zina faida gani?
 
Marehemu hajamaliza hata siku 2 kaburini umeshaanza kusema shirika lake lililotengeneza faida ya bil 28 mwaka jana mwaka huu limetengeneza hasara?
Corona imeharibu sana biashara... Na kulingana na kipindi ambacho ripoti ya mkaguzi inahusika.. ndo kipindi ambacho hali imekuwa tete.
ATCL ukilinganisha na mashirika mengine nahisi ina unafuu mkubwa sana.
Tuendelee kulisapoti shirika letu
 
Kabla ya corona hizo ndege zilikuwa zinaenda wapi? Na baada ya corona zilishindwa kwenda zilikokuwa zinaenda?

2017/2018 na 2018/2019 kipindi ambacho CAG alifanya ukaguzi wa hesabu za ATCL kulikuwa na covid? Au hujasoma hata ripoti yenyewe?

Mwaka jana Magyfuli kwa kinywa chake alisema ATCL imefanya faida ya bil 28. Alikuwa anatudanganya?

Mwaka jana ATCL wametoa gawio serikalini. Walikuwa wanatudanganya?
 
Tunapoambiwa ATCL imepata hasara tusibeze sana. Kuna American Express na Delta Lines wanachungulia kaburi! Na Amar hapo UK British Airways imegubikwa madeni nusura izame! Tatizo lenu ni uzungu pori? Ni mashirika ya wenye mafuta kina EMIRATES, QATAR na wenzao Serikali zao zimenunua madeni. Baadhi ya matukio yaliyotikisa biashara ya usafiri wa anga duniani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita:

1. Global Economic and financial crisis (mtikisiko wa kiuchumi na kifedha ulioikumba dunia).
2. Marubani, wahudumu na watumishi viwanjani kugoma Mara kwa mara nchini Marekani, UK, France na Italy.
3. Kodi mpya (carbon tax) kugharamia uchafuzi wa anga.
4. Covid 19 restrictions on travel (masharti ya covid 19)
5. Gharama za utengenezaji ndege kuongezeka mno kutokana na ushindani Kati ya Airbus na Boeing kufuatia mahitaji ya usalama wa abiria.
6. Nchi kunyimana route (protectionism policies).
7. Uendeshwaji mbaya wa airline
8. Kubadilika kwa sura ya utalii. Mfano watalii wengi kuanza kujikita kutembelea nchi au eneo lao, kushuka ari ya kuona wanyama au milima n.k.

Hizi ndio sababu ya mashirika mengi duniani kuendeshwa kwa hasara. Sio lazima éti hasara pawepo na wizi

Licha ya mashirika kufanya vibaya hakuna nchi imefunga shirika lake. KLM ilitaka ijiuze kwa AIR FRANCE wananchi wakaandamana! Serikali ikalazimika kubeba madeni.

Alitalia ya Italy ilitangazwa imefilisika Papa akamwandikia barua Prime Minister kwamba Vatican hairidhii uamuzi! Serikali ikabeba Madeni. Mpaka leo Alitalia ipoipo tu. Ukipatiwa ticket ya Alitalia jiandae for cancellation wakati wowote. Mara nyingi watakuhalishia Easy Jet au Ryan Air.

Sasa kuna mijitu inadhani biashara ya ndege sawa na biashara ya kuuza mashokishoki Darajani!
😊
(..) Umesahau gharama yakurekebisha ndege iliyopaki ni kubwa kuliko ndege yenye route za kila wakati
 
Kabla ya corona hizo ndege zilikuwa zinaenda wapi? Na baada ya corona zilishindwa kwenda zilikokuwa zinaenda?

2017/2018 na 2018/2019 kipindi ambacho CAG alifanya ukaguzi wa hesabu za ATCL kulikuwa na covid? Au hujasoma hata ripoti yenyewe?

Mwaka jana Magyfuli kwa kinywa chake alisema ATCL imefanya faida ya bil 28. Alikuwa anatudanganya?

Mwaka jana ATCL wametoa gawio serikalini. Walikuwa wanatudanganya?
Faida ya bil 28 ,haiingii akilini ni mazingaumbwe kwa routes gani sasa?
 
Hatuwezi kurusha Boeing safari za ndani labda sisi ni matajiri sana
ndege aina hiyo inafahamika ni ya masafa marefu na kwa faida basi ilitakiwa kupata safari nyingi sana za nje
bila hivyo hasara tutapata daily
Ndege inawezekana tulikuwa tunaelekea huko kama nchi lakini tuliharakisha sana na ni wazi KQ,EAL, Rwandair,EK,SAL, nna wengineo watakuwa tayari kutuachia hizi route na si tupige walau deiwaka?
nikiri mm si mjuvi sana naamini huku kuna wataalamu wa anga ningeomba kujuzwa tu
ni kwanini ndege za ATCL au ni njia gani hutumika kupata route? kama DXB-DAR,JRO-NBO na kwingine
 
Ohh ndio maana nilisikia nchi nyingi hazijihusishi directly zaidi ya kuachia mashirika binafsi kama precision air na fastjet wafanye hiyo biashara ili fedha za serikali zifanye mambo mengine yanayoleta impact kubwa kiuchumi.

By the way, Ningeomba unipe uelewa, je kama nchi tunapata faida gani kubwa mbali na "national pride" , inayotufanya tuservice hilo deni kuliko kuwekeza katika sekta nyingine.

Nilikuwa nimepanga kutokujihusisha na mijadala ya kisiasa, imebidi nijitokeze katika huu mjadala.

Mjadala huu umechukua sura ya kisiasa hasa baada ya ripoti ya CAG kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara.

Mleta mada kaliweka suala la ATCL kiuchumi zaidi ila wewe Eyce unatafuta majibu ya hoja zako kisiasa.

Tanzania katika awamu mbalimbali za Serikali zimekuwa na mikakati ya msingi ya kiuchumi. Sera ya Kilimo kwanza ilikuwa na inakusudia kujitosheleza kwa kilimo. Sera ya viwanda inakusudia kujitosheleza kwa bidhaa muhimu kwa mahitaji ya kila siku na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Ili kufanikisha hayo imelazimika kuimarisha miundo mbinu dhabiti ya usafirishaji (ardhini, majini na angani) kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Wengi wetu humu JF hatujui vichocheo vya kiuchumi na hata kama tunajua, kwa sababu tunazozijua, tunajitokeza kubeza ununuzi wa ndege. Nina uhakika miaka ijayo faida ya kununua ndege zetu wenyewe leo itakuwa dhahiri.

Kwa mfano, baada ya kujitosheleza chakula na bidhaa, Sera ijayo ni ya uuzaji bidhaa nje ya nchi. Hili haliwezi kufanikiwa kwa faida bila kuwa na usafiri wa anga ulio imara. Kama utakumbuka hadi leo mazao yetu na madini husafirishwa kupitia Kenya, je, tuendelee hivyo hivyo kwa bidhaa za viwanda vyetu vinavyojengwa?
 
Tunapoambiwa ATCL imepata hasara tusibeze sana. Kuna American Express na Delta Lines wanachungulia kaburi! Na Amar hapo UK British Airways imegubikwa madeni nusura izame! Tatizo lenu ni uzungu pori? Ni mashirika ya wenye mafuta kina EMIRATES, QATAR na wenzao Serikali zao zimenunua madeni. Baadhi ya matukio yaliyotikisa biashara ya usafiri wa anga duniani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita:

1. Global Economic and financial crisis (mtikisiko wa kiuchumi na kifedha ulioikumba dunia).
2. Marubani, wahudumu na watumishi viwanjani kugoma Mara kwa mara nchini Marekani, UK, France na Italy.
3. Kodi mpya (carbon tax) kugharamia uchafuzi wa anga.
4. Covid 19 restrictions on travel (masharti ya covid 19)
5. Gharama za utengenezaji ndege kuongezeka mno kutokana na ushindani Kati ya Airbus na Boeing kufuatia mahitaji ya usalama wa abiria.
6. Nchi kunyimana route (protectionism policies).
7. Uendeshwaji mbaya wa airline
8. Kubadilika kwa sura ya utalii. Mfano watalii wengi kuanza kujikita kutembelea nchi au eneo lao, kushuka ari ya kuona wanyama au milima n.k.

Hizi ndio sababu ya mashirika mengi duniani kuendeshwa kwa hasara. Sio lazima éti hasara pawepo na wizi

Licha ya mashirika kufanya vibaya hakuna nchi imefunga shirika lake. KLM ilitaka ijiuze kwa AIR FRANCE wananchi wakaandamana! Serikali ikalazimika kubeba madeni.

Alitalia ya Italy ilitangazwa imefilisika Papa akamwandikia barua Prime Minister kwamba Vatican hairidhii uamuzi! Serikali ikabeba Madeni. Mpaka leo Alitalia ipoipo tu. Ukipatiwa ticket ya Alitalia jiandae for cancellation wakati wowote. Mara nyingi watakuhalishia Easy Jet au Ryan Air.

Sasa kuna mijitu inadhani biashara ya ndege sawa na biashara ya kuuza mashokishoki Darajani!
" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fstatic.xx.fbcdn.net%2Fimages%2Femoji.php%2Fv9%2Ft7f%2F1%2F16%2F1f60a.png&hash=efe739e1e11105d2cb04b5162bb1658d" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> <img src=" title="" width="" height="" />
Serikali ilitangaza kujitoa kwenye biashara ikauza mashirika.

Kizabizabina cha kurudi tena kwenye biashara hizi, tena biashara complex, kimetoka wapi?
 
Ohh ndio maana nilisikia nchi nyingi hazijihusishi directly zaidi ya kuachia mashirika binafsi kama precision air na fastjet wafanye hiyo biashara ili fedha za serikali zifanye mambo mengine yanayoleta impact kubwa kiuchumi.

By the way, Ningeomba unipe uelewa, je kama nchi tunapata faida gani kubwa mbali na "national pride" , inayotufanya tuservice hilo deni kuliko kuwekeza katika sekta nyingine.
Wamarekani wenyewe walioanzisha usafiri wa ndege na wenye mashirika makubwa ya kutengeneza ndege kama Boeing mpaka leo hawana shirika la ndege la taifa.

Unafikiri wao ni wajinga walivyoachia biashara hii iwe ya sekta binafsi?
 
Watu wenye akili waliona hili mapeeema sana wakawa wanaongea bungeni wabunge wa ccm waliwazomea !!!!! Sasa bado makampuni ya madili mliowapora migodi yao wakati mikataba mlipitisha kwa kusema ndiooooooooo haya madege yatashikwa tuuu
 
Nilikuwa nimepanga kutokujihusisha na mijadala ya kisiasa, imebidi nijitokeze katika huu mjadala.

Mjadala huu umechukua sura ya kisiasa hasa baada ya ripoti ya CAG kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara.

Mleta mada kaliweka suala la ATCL kiuchumi zaidi ila wewe Eyce unatafuta majibu ya hoja zako kisiasa.

Tanzania katika awamu mbalimbali za Serikali zimekuwa na mikakati ya msingi ya kiuchumi. Sera ya Kilimo kwanza ilikuwa na inakusudia kujitosheleza kwa kilimo. Sera ya viwanda inakusudia kujitosheleza kwa bidhaa muhimu kwa mahitaji ya kila siku na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Ili kufanikisha hayo imelazimika kuimarisha miundo mbinu dhabiti ya usafirishaji (ardhini, majini na angani) kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Wengi wetu humu JF hatujui vichocheo vya kiuchumi na hata kama tunajua, kwa sababu tunazozijua, tunajitokeza kubeza ununuzi wa ndege. Nina uhakika miaka ijayo faida ya kununua ndege zetu wenyewe leo itakuwa dhahiri.

Kwa mfano, baada ya kujitosheleza chakula na bidhaa, Sera ijayo ni ya uuzaji bidhaa nje ya nchi. Hili haliwezi kufanikiwa kwa faida bila kuwa na usafiri wa anga ulio imara. Kama utakumbuka hadi leo mazao yetu na madini husafirishwa kupitia Kenya, je, tuendelee hivyo hivyo kwa bidhaa za viwanda vyetu vinavyojengwa?

kwa nini unadhani kila mtu akiwa na mawazo fulani bhasi yupo kisiasa. Nilichofanya ni kuuliza ili nijibiwe ila wewe umeamua kunihukumu pasipo kujua , huwa sipo katika thread za kutetea vyama humu na nimeshiriki kama wewe ulivyoamua kushiriki leo..

Pia kama unaujua uchumi bhasi vitu basic kama opportunity cost na scale of preference si mgeni navyo, ni vitu muhimu na ndicho nilichoulizia.

just a simple economic concept.. Unapoamua kutumia pesa yako kufanya investment A mfano kununua ndege, kuna faida unazikosa kama ungefanya investment B labda kutengeneza kiwanda cha packages au kuongezea thamani bidhaa za za kilimo, uvuvi au ufugaji....

kama investment tayari ina hasara ilhali kuna sekta kama utalii ambazo zimeonesha mafanikio makubwa bila kuwa na national airline. tena kama horticulture ama uvuvi bado inakua kwa kutumia ndege za mizigo za nje na si za abiria. plus Nchi nyingi nimesikia zinafanya hivi je, was it necessary kununua tena by cash

kama wewe unaelewa uchumi vizuri, ulitakiwa kunionesha necessity ikibidi na data labda toka shirika limefufuka kuna sekta flani zimenufaika au zimekua tofauti na hapo nyuma lilipokuwa halipo..ili kuonesha hata potential yake tu na mimi nipate kuelewa.. was i wrong
 
Wamarekani wenyewe walioanzisha usafiri wa ndege na wenye mashirika makubwa ya kutengeneza ndege kama Boeing mpaka leo hawana shirika la ndege la taifa.

Unafikiri wao ni wajinga walivyoachia biashara hii iwe ya sekta binafsi?
exactly na ndicho nilichotaka kuelewa zaidi kutoka kwa mtoa mada au yoyote mwenye uelewa zaidi katika hili,

ikibidi aseme labda kumekuwa na impact gani kiuchumi toka 2015 hadi leo ili ionekane walau justification ya hasara inayopatikana kwa taifa

only that mkuu
 
Kama biashara ya usafiri wa ndege haina faida kama ulivyo elezea kwamba mashirika mengi yanapata hasara, kulikuwa na ulazima gani wa kununua zile ndege hili ATCL ifufuke?

Inaonekana una washangaa wananchi kulalamika ATCL inatia taifa hasara badala ya kuwashangaa wale walioenda kufufua shirika ambalo linaingizia taifa hasara.
 
exactly na ndicho nilichotaka kuelewa zaidi kutoka kwa mtoa mada au yoyote mwenye uelewa zaidi katika hili,

ikibidi aseme labda kumekuwa na impact gani kiuchumi toka 2015 hadi leo ili ionekane walau justification ya hasara inayopatikana kwa taifa

only that mkuu
Ni vigumu kupata maelezo ya kiuchumi ku justify.

CEO wa ATCL kakubali kwamba ripoti ya CAG inayoonesha loss iko sahihi.

Ndege ziliendeshwa kisiasa zaidi, kwa amri kutoka juu,hakuna justification ya kiuchumi.

Serikali za wajanja wanaojua biashara Wamarekani hazipo kwenye biashara ya ndege.

Zimeiachia sekta binafsi.
 
Back
Top Bottom