Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,060
Kati ya biashara ngumu na sophisticated ni pamoja na biashara ya usafiri wa anga. Makampuni makubwa kabisa ya ndege yenye wataalam wenye weledi na uzoefu, kuna wakati wanaishia kupata hasara. Kama hao wanafeli, itakuwaje kwa nchi kama Serikali ya Tanzania ambayo haijawahi kuendesha mradi wowote kwa faida?
Serikali ya Tanzania haina historia ya kuwa na uwezo wa kuendesha biashara yoyote kwa ufanisi na mafanikio:
1) kwenye simu, Serikali ilishindwa
2) kwenye viwanda Serikali ilishindwa
3) Kwenye madini, Serikali ilishindwa
4) kwenye usafiri wa mabasi, Serikali ilishindwa
5) kwenye umeme, mpaka leo hii tunashuhudia, imeshindwa
6) kwenye usafiri wa majini, Serikali ilishindwa
Serikali ikiingia kwenye ushindani wa biashara huwa inashindwa moja kwa moja, lakini angalao wananchi huwa wanapata huduma iliyokusudiwa.
Serikali inapo monopolize biashara, kwanza itapata hasara, na wananchi mtateseka kwa kukosa huduma.
Wale wa umri wangu wanayakumbuka yafuatayo:
1) wakati wa mwanzo, viwanda vyote vilipokuwa chini ya Serikali, sukari ilikuwa shida, bia shida, sigara shida, sabuni shida, chumvi shida, kuunganishwa simu ilikuwa shida, usafiri ilikuwa shida, kanga ilikuwa shida, betri za radio ilikuwa shida, n.k.
2) sasa hivi baada ya utawala wa Magufuli kuwafukuza fastjet, bei ya tiketi za ndege hazishikiki. Wakati fastjet kama ukiwahi kukata tiketi, kulikuwepo mpaka ticket za sh 80,000. Leo hata tiketi ya sh. 200,000 ATCL hupati.
3) tuna reli ya TAZARA inayofanya safari kati ya Dar mpaka Kaprimposhi, Zambia, ikipitia Tunduma, Mbeya, Makambako, Ifakara mpaka Dar. Kutokana na kawaida ya Serikali kuendesha miradi yote vibaya, reli hiyo haina msaada wowote. Wafanyabiashara bado wanaona aheri kutumia malori kuliko kusafirisha kwa treni ukakutane na ukiritimba wa Serikali. Kama TAZARA ingekuwa inaendeshwa kwa ufanisi, mahindi, mbao, viazi kutoka Mbeya, Njombe, Mafinga hata Songea, vyote vingesafirishwa kwa TAZARA, lakini kwa atitude za watendaji wa Serikali na mashirika ya umma, wengi hawapendi kutumia reli hiyo.
Sasa tuna ndege hizi za ATCL, zinafanya usafiri wa anga bila mshindani yeyote, bado zinaishia kwenye hasara. Na hakika nawahakikishieni, hata reli mpya inayojengwa, kama itaendeshwa na Serikali, itaishia kwenye hasara tu.
Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kuendesha kwa faida hata genge la nyanya. Iache biashara zote ziendeshwe na Sekta binafsi. Ni aheri ndege zetu zote pamoja, reli ya TAZARA na SGR itakapomalizika, vikodishwe kwa sekta binafsi kwa uendeshaji. Bila hivyo tutegemee miradi hiyo kuwa na hasara wakati wote, na hu⁵duma duni.