CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Tunapoambiwa ATCL imepata hasara tusibeze sana. Kuna American Express na Delta Lines wanachungulia kaburi! Na Amar hapo UK British Airways imegubikwa madeni nusura izame! Tatizo lenu ni uzungu pori? Ni mashirika ya wenye mafuta kina EMIRATES, QATAR na wenzao Serikali zao zimenunua madeni. Baadhi ya matukio yaliyotikisa biashara ya usafiri wa anga duniani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita:
1. Global Economic and financial crisis (mtikisiko wa kiuchumi na kifedha ulioikumba dunia).
2. Marubani, wahudumu na watumishi viwanjani kugoma Mara kwa mara nchini Marekani, UK, France na Italy.
3. Kodi mpya (carbon tax) kugharamia uchafuzi wa anga.
4. Covid 19 restrictions on travel (masharti ya covid 19)
5. Gharama za utengenezaji ndege kuongezeka mno kutokana na ushindani Kati ya Airbus na Boeing kufuatia mahitaji ya usalama wa abiria.
6. Nchi kunyimana route (protectionism policies).
7. Uendeshwaji mbaya wa airline
8. Kubadilika kwa sura ya utalii. Mfano watalii wengi kuanza kujikita kutembelea nchi au eneo lao, kushuka ari ya kuona wanyama au milima n.k.
Hizi ndio sababu ya mashirika mengi duniani kuendeshwa kwa hasara. Sio lazima éti hasara pawepo na wizi
Licha ya mashirika kufanya vibaya hakuna nchi imefunga shirika lake. KLM ilitaka ijiuze kwa AIR FRANCE wananchi wakaandamana! Serikali ikalazimika kubeba madeni.
Alitalia ya Italy ilitangazwa imefilisika Papa akamwandikia barua Prime Minister kwamba Vatican hairidhii uamuzi! Serikali ikabeba Madeni. Mpaka leo Alitalia ipoipo tu. Ukipatiwa ticket ya Alitalia jiandae for cancellation wakati wowote. Mara nyingi watakuhalishia Easy Jet au Ryan Air.
Sasa kuna mijitu inadhani biashara ya ndege sawa na biashara ya kuuza mashokishoki Darajani!