Allien
JF-Expert Member
- Jul 6, 2008
- 5,546
- 1,861
Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk
Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?
Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:
- Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
- Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
- Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
- Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
- Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
- Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
- Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
- Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
- Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
- Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.
Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?
Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana