utukufu mwanjisi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2017
- 2,830
- 2,417
Kiufupi, nimesafiri kwa mara ya kwanza safari ya mabasi ya usiku yaondokayo saa 2 usiku Dar es salaam na kuelekea Rombo. Kwa bahati nzuri au mbaya nimefanikiwa kufika muda wa saa 11 asubuhi hapa Mamsera hivyo nimepata kushuhudia mengi sana.
Vijana wamejaa kwenye kibanda muda huu wanaagiza tu pombe kali na pombe za kwenye chupa zina rangi ya njano, aisee nimesikitika sana mpaka nimejiuliza ni hawa hawa wachaga ninaowaaminia kwa utafutaji wakiwa mijini huku wanakuwa wapumbavu hivi.
Kunywa pombe saa 11 asubuhi hata kwetu Rungwe Kiwira huko hawafanyi upumbavu.
Ndugu zangu wachaga jiangalieni kwenye hili kwa ajili ya vizazi vyenu vijavyo bila hivyo mtapoteza nguvu kazi zote mbeleni huko.