Watanzania Wengi ni Wavivu? The Moment of Truth!

Allien

JF-Expert Member
Jul 6, 2008
5,546
1,861

Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?

Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:

  • Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
  • Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
  • Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
  • Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
  • Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
  • Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
  • Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
  • Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
  • Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
  • Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
n.k, nk.

Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.

Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?

Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana
 
Kuna ka ukweli fulani . . . . .

Nafahamu wadau wengi baada ya kunywa chai hotelini asubuhi, akifika ofisini inabidi apitie baadhi ya magazeti akimaliza ndiyo aanze kazi.

Yuko jamaa yangu moja huko nyuma aliwahi kukutana na Rais Mstaafu BWM kuhusu wazo fulani la kuongeza ajira kwa vijana na kujijengea mitaji . . . . Model ya huyo jamaa kwa mujibu wake ingeweza kuleta ajila milioni 3 katika miaka mitatu na kujenga mtaji wa TZS trilioni 6. BWM baada ya kumsikiliza jamaa yangu (ilikuwa kabla ya kampeni za Uchaguzi 2005), akamwambia . . . . .

"Kijana mimi nakupongeza sana na nakutia moyo uendelee . . . Kitendo cha wewe tu kufikiria ajira milioni 3 na mtaji wa trilioni 6 ni mafanikio tayari. Nasikitika katika watendaji wangu serikalini wengi hawana uthubutu na ni wavivu kuwajibika. Ni asilimia kidogo sana chini ya kumi ndiyo hasa nawategemea . . . . . "

Hii kwa kiasi fulani ina ukweli fulani. Na ndiyo maana hadi leo Tanzania bado tunasuasua katika kupiga hatua kubwa za kimaendeleo pamoja na rasilimali na nafasi zote tulizonazo.

Yataka mapinduzi ya fikra ili kasi ya maendeleo tuyatakayo yaweze kuja.

Kuna mtu aliwahi kusema: Mathalani hata tukibadilishana nchi e.g. Waingereza wao waje TZ na sisi tuende UK . . . Baada ya miaka mitano TZ itakuwa juu zaidi na UK itakuwa ama iko palepale, ama imeendelea kidogo sana ama imeporomoka.

Si vibaya tukijifanyia self analysis tuna matatizo gani kama watanzania tukiwa watu binafsi.
 
INASIKITISHA SANA!
wengi hawajui kuwa muda ni rasilimali... wengi hufikiria kupoteza muda ili siku iishe...wengi hukwepa kufanya kazi waliyoomba wenyewe bila kulazimishwa.Siku wakisimamishwa kazi ndio wa kwanza kulalamika na kutafuta mchawi.Hata hivyo utamaduni huu huonekana zaidi kwenye ajira ya umma maana sekta binafsi hawaendekezi upuuzi huu.
 
Ni kweli tuna kundi kubwa la watu wavivu (kama mimi). Lakini kama viongozi wangekuwa wanawajibika, wangekuwa na uwezo wa kukemea wasiowajibika. Kwa vile viongozi wengi ni watawala wasiowajibika, watawaliwa nao tumelemaa. Watanzania wanatakiwa kusahau kuwa maendeleo yao yatatokana na uongozi bora (ambao haupo). Kwa hali ya sasa maendeleo ya Mtanzania yatatokana na kila mmoja kuchukia hali aliyonayo na kuamua kubadilika. Ni vigumu kwa Tanzania kubadilika kama kundi.
 
Sio siri Wabongo tuu wavivu. Na mimi binafsi nakiri kwa binafsi yangu ni mvivu. Nilipoachishwa kazi za kuajiriwa serikalini, nikajiajiri mwenyewe mwaka 2002. Ilinibidi kuamka mapema kuliko wakati wa ajira rasmi. Kazi ya kujiajiri ilipochanganyia sasa nimeajiri watu mpaka dereva. Kuamka asubuhi ziwezi tena na kuna siku hata afisini sikanyagi. Kisa ni uvivu tuu. Sasa nachagua kazi na kupanga bei kama unataka niitee ukishindwa bei yangu niache.

Wengi wa watumishi wa umma mshahara ni fixed. Hata ufanye kazi kwa bidii vipi, huwezi kuongeza hata sentano.

Mashirika ya ajira za kimaifa yanalijua hili tatizo la uvivu wa Watanzania na zinapotokea nafasi za ajira tukagombea na Wakenya na Waganda, kama tunasifa sawa, anatangulia Mkenya then Mganda na Mtanzania ni wamwisho kufikiriwa.

Watanzania hatuna moyo wa kujituma kufanya bidii katika kazi. Katika mahangaikoya ujana niliwahi kufanya kazi London kweny site fulani ya ujenzi. Kukawa na fatiki ya kupandisha vifaa ngorofa ya 10 kwa ngazi. Tulikuwa vibarua wengi warusi mswahili peke yangu. Nilishuhudia jamaa wanapiga job kila wakipanda trip tatu mimi moja. Kumbe kuna supervisor anatick kila trip za mtu. Hatimaye niliachishwa kazi. Kisa ni uvivu tuu.

Lile neno ili tuendelee tuna hitaji watu, maana yake nguvu kazi ya kufanya mambo. Hapa tunapozungumza migodini wabongo ni manual labor tu wataalamu wote wageni. Mahotelini mameeneja wote wakenya. Huko Zanzibar hata wahudumu, wakenya. Waalimu wa academy ndio usiseme.

Katika media power ya wakenya inajulikana. Hata ITV kwenye programing yake, kichwa chao ni Mkenya, Macharia Koigi. Makampuni makubwa ya matangazo ni ya wakenya. Kisa Watanzania tuu wavivu.
 
Mambo yanayochangia uvivu ni pamoja na kuhisi kuwa wew sio mmiliki au hauna hisa ktk kampuni husika, mshahara mdogo, motisha hasi kama dharau kutoka viongozi wa ngazi za juu, kukatishana tamaa ( mfano%2
 
Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?

Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:

  • Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
  • Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
  • Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
  • Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
  • Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
  • Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
  • Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
  • Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
  • Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
  • Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
n.k, nk.

Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.

Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?

Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana

Allien, hebu fikiria hili pia: Kuna Watz wanalipwa tu 'net salary' - hawana NSSF, hakuna overtime katika kazi, hakuna cha sikukuu (Xmas, Mwaka Mpya, Idd, etc are just like other week days), akienda likizo anatumia mshahara wake (yaani, hakuna hela ya likizo), mshahara haufanyiwi marekebisho miaka nenda rundi na kufukuzwa kazi ni muda wowote na akiugua matibabu ni juu yake.

Kwa hali hii, inawezekana mambo mawili: 1. Mfanyakazi anaweza kuwa mwaminifu sana ("kufanya kazi kwa woga") ili kutetea kibarua chake na hatimaye anaweza kupata 'nerve breakdown' - depression. 2. Au anaweza kuwa sugu kwa lolote litakalotokea na hapo ndipo inawezekana kutumia muda kwa namna ambayo haizalishi kwa sababu anajua 'afterall' ameshajitoa kiasi cha kutosha - ame'sacrifice' mengi katika ajira yake.

Nionavyo mimi, mfumo wa kazi kwa hapa Tz unachangia kuwa na hali hiyo unayoisema 'rather than' kufikiria kuwa Watz wengi ni wavivu. Kwa bahati mbaya, sheria na mazingira ya kazi sehemu nyingi kwa hapa Tz hayampi mfanyakazi tija au motisha.

Baadhi wanafanya kazi bora iende - kwa mazoea tu. Hebu niambie mwalimu ambaye hajalipwa malimbikizo yake miaka nenda rudi na akitaka kitu mpaka akope, atakuwa na moyo gani wa kufanya kazi kwa bidii? Askari anayelipwa shillingi laki moja kama ni mpelelezi au traffic police ni kitu gani kitamfanya afanye kazi kwa bidii kuliko kuomba rushwa? Kuna mifano mingi kama hii. Nina hakika sheria na mazingira ya kazi yakiboreshwa Watz watachapa kazi kwa bidii tu.

Kitu kingine ni malupulupu ya vigogo. Kigogo ana malupulupu mengi mno: akienda semina donge nono kuliko anavyokuwa ofisini. Je, kitu gani kitamfanya huyu kigogo asikazanie semina kuliko huduma anayoitoa ofisini mwake?

Ninachoshauri mimi ni kwamba - watu walipwe 'decently' kwa kazi wanayoifanya na kuwe na mchanganuo mzuri wa kazi - job description, maana wengine wanafanya kazi kwa kudhania kuwa huenda hiyo wanayoifanya ndiyo kazi yao wakati siyo. Wegnine wanafanya hata kazi za mabosi wao bila wao kujua na kumfanya bosi 'ale kuku' tu.

Lakini mtu akifanya kazi katika hali ya 'insecurity' - akijua baada ya kustaafu atakuwa maskini wa kutupwa - huyo lazima ataendelea kutafuta miradi binafsi na siyo kosa lake bali mazingira ndiyo yanayomfanya hivyo.

Kuhusu hali ya kilimo vijijini. Sehemu ninayotoka ni wavuvi na wakulima. Uvuvi umebaki wa watu wenye mitaji mikubwa - wanatumia mashine na wanavua katikati ya ziwa - mwendo wa zaidi ya saa 1 kwa mashine. Huko wana 'patrol boats' na hawataki wamwone mvuvi mdogo wa makasia kwani wanadhani ndiye anayewaibia nyavu zao. Wakimkuta anapigwa au kutumbukizwa kwenye maji.

Na huyo mvuvi mdogo anaambiwa anunue nyavu zenye matundu makubwa (yaani sawa na zile zinazotumiwa na wavuvi wenye mitaji mikubwa katikati ya ziwa asikoweza kwenda kuvua na huko ndiko wanakopatikana samaki wakubwa tu). Je, ataishije? Ataweza kufanya haya:1. Ataanza kuvua kwa kutumia sumu usiku muda ambao siyo rahisi kugundua uhalifu huo 2. Au atakuwa kibarua tu wa wavuvi wakubwa - maana hawezi kufanya zaidi ya hayo mawili.

Kwa mkulima, akivuna wanunuzi wanamfuata shambani na gunia moja na nusu la kwake wao wanafanya gunia moja na wananunua kwa bei ya chini kabisa. Hao wanunuzi wanakuwa na usafiri kabisa na huyo mkulima hana na hasa ukizingatia kuwa barabara zinapitika kwa musimu tu. Hivyo, hata angezalisha chakula kingi kiasi gani, akiuza anapata hela kidogo tu isiyoweza kutosheleza mahitaji ya familia yake.

Lakini anaambiwa mjini kuna lami, majumba mazuri na ajira zinapatikana. Huyu naye anaweza kujaribu haya: 1. Anaweza kuendelea na kilimo chake hicho na ataendelea kuwa maskini. 2.Au anaweza kushawishika kwenda mjini na kuwa kibarua kwa makampuni ya ujenzi, konda wa daladala, mlinzi wa usiku nk.

Tungetaka kuboresha maisha ya wakulima tungewafanya wao wenyewe ndio wapange bei kupitia vyama vyao na kulingana na kazi wanayoifanya. Kwa bahati mbaya hapa kwetu hilo halipo na mara nyingi serikali inapanga bei bila kuzingatia gharama wanazoweka na ugumu wa kazi na upatinaji wa soko la mazao yao.

Sasa kwa hayo uvivu uko wapi? Mimi bado naamini mazingira ndiyo yanayowafanya watu wakate tamaa na kupunguza bidii kwa vile wanaona hakuna sababu ya kuweka nguvu nyingi kwa kitu wanachofaidi kidogo. Sisi tusiojua 'how much people suffer' na tunaochangia matatizo yao dio tunaoona ni wavivu.

Kuna hii story: An industrialist travelled along a lakeshore, where he found a fisherman resting in his swinging chair and smoking a pipe after fishing all night without catching anything. Then, the industrialist said, "Hi! What are you doing? You should be working and earning your living!"

The fisherman asked, "And then?" He replied, "You should be earning a lot of money and buying your necessities." "And then," the fisherman asked again. "You should have built a nice house and married a beautiful wife," he replied. "And then," asked the fisherman. "You should be resting and enjoying life," he replied.

Then, the fisherman asked him, "What do you think I am doing now (since he was also resting and enjoying life - smoking a pipe)!"
 
Last edited:

Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?

Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:

  • Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
  • Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
  • Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
  • Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
  • Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
  • Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
  • Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
  • Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
  • Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
  • Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
n.k, nk.

Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.

Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?

Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana

Mkuu nadhani hii naweza kuuita moja kati ya thread zilizogusa ukweli unaouma. Hii ni tabia ambayo ni moja ya vikwazo vikubwa kabisa kwa maendeleo ya Tanzania. "sisi" ni wavivu, lakini sio wa kufikiri kama anavyosema Mkapa, lakini ni wavivu wa kazi. Nimeamua kusema sisi kwa makusudi na sio kusema wao na mimi kujiweka pembeni kwa sababu na mimi ni mmoja kati ya watanzania. Na baada ya kufanya kazi kidogo na watu wanaofanya kazi ndio nikaona ukweli huu.
Sisi kazini tuna-attend lakini hatufanyi kazi tunavyotakiwa, we hardly work instead of working hard. Na kibaya zaidi hata wanaofanya kazi kuna wengi tu wanashindwa kumanage mapato yao, wanajua kutummia ovyo, lakini hawezi kuhakikisha jasho lao la leo linawasaidia kesho. Huu ni ukweli tukemee sana mabaya yanayofanywa lakini tujirekebishe pia.
 
Magobe T:

Kuna haja ya kufanyia utafiti jambo hili. Lakini uzoefu wangu wa kazi unaonyesha kwamba hao wanaolipwa kidogo uliowataja ndio wanachapa kazi zaidi na waheshimiwa ndio wanachukua muda mwingi sana kwenye chai na msosi!!
 
Siyo kwamba Watanzania ni wavivu. Watanzania wanahitaji elimu,wafahamu jinsi ya kufanya kazi efficiently,kwa ufanisi.
Tena wafundishwe na Watanzania wenzao. Ni kama wakati ule walipokuja Wamisionari wazungu,hawakupokelewa vyema. Walipigwa mishale na Waafrika. Lakini walipowafundisha mapadre Waafrika kuwasaidia kufanya Uinjilishaji,ndipo Dini ikaanza Afrika,Dini ya Kikristu.
Kwa hiyo kinachohitajika,ni Mwafrika ajifunze pysics,hesabu,udaktari,n.k.,ndipo itakuwa rahisi kwa Mwaafrika kuyakubali mambo hayo. Mambo yote unayo dhani yana faida katika nchi za nje,ambayo Mtanzania anaweza kufaidika nayo,nenda kajifunze mambo haya ,halafu,uje uwafundishe Watanzania.
 
Magobe T:

Kuna haja ya kufanyia utafiti jambo hili. Lakini uzoefu wangu wa kazi unaonyesha kwamba hao wanaolipwa kidogo uliowataja ndio wanachapa kazi zaidi na waheshimiwa ndio wanachukua muda mwingi sana kwenye chai na msosi!!

Kitila Mkumbo, mbona wanaosema Watz ni wavivu ni haohao waheshimiwa wenyewe? Mimi nimejaribu kuelezea kitu gani kinaweza kuathiri utendaji kazi wa hao watu wadogo na pia vigogo. Na ninayosema siyatoi kichwani.

In fact, nimekuwa nikifanya kazi na hawa watu wa chini na hasa kutetea haki zao kwa muda mrefu tu. Na mimi nimwenyewe natoka kijijini na ninajua jinsi gani watu wanachapa kazi lakini mazingira yenyewe yanawakatisha tamaa.

Nadhani ukisoma vizuri ninachojaribu kukielezea utaona vizuri point yangu dhidi ya 'sweeping statement' Watz wengi ni wavivu.
 
Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?

Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:

  • Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
  • Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
  • Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
  • Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
  • Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
  • Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
  • Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
  • Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
  • Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
  • Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
n.k, nk.

Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.

Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?

Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana

Mkuu tupo pamoja sana na hili suala naliunga mkono asilimia 100 kwa maana sisi watanzania ni wavivu.

Lakini kwa upande mwingine nafikiri serikali na mfumo mzima wa Uongozi sio wa JK tuu hili lilikuwepo kuanzi kwa Nyerere hapakuwa na "PUSH FACTORS" Mfano; wenzetu wa UK ukiangalia ingali wavivu lakini mfumo wa maisha umeweza kuwabana na kulazimisha watu wafanye kazi na Serikali kupitia sera zake "BILLS" ndio mechanism tosha ya watu kufanya kazi

Ukiangalia USA nafikiri wenzangu waliopo huku wanaweza kunisaidia hili ila ninachofahamu GHARAMA ZA HUDUMA ZA MATIBABU NA OTHER BILLS ndio zinawafanya watu kusukumika.

Kiukweli Uvivu ni nature ya mwanadamu yeyote ila kama anakuwa fixed kwenye mfumo fulani nafikiri hili linaweza kupungua na pengine kuisha kabisa.

Issue nyingine nafikiri, kama serikali nafikiri hawanabudi kubadili Mfumo wa Malipo kwa wafanyakazi wote na ikiwezekana nafikiri ingekuwa njema zaidi kama kungekuwa na malipo kulingana na muda na siku ( SALARY PER HOUR) nafikiri hii italeta ufanisi na ushindani hasa kwa wale wanaotoka Vyuoni na wanaojidai wa Experience makazini. Izingatiwe lazima kuwe na kipaumbele kwa baadhi ya kazi hasa kwenye malipo kama Walimu, Polisi, Wanajeshi, Madaktari na Jeshi la Magereza na badala ya malipo kwa saa wanaweza kuwa na malipo kwa Mwezi kama ilivyo sasa.

Kwa Tanzania nadhani wote sisi ni mashahidi, watu wengi wanasubiria mwisho wa mwezi kwa maana wengi wao wanazuga tuu kuvuta siku, HAKUNA PUSHING MECHANISM YEYOTE na KAZI HAZINA USHINDANI waliopo ndio wanaona kama ndio wamefika na wasio makazini wanaona kama wanaonewa.

Nafikiri, Watanzania hasa Serikali yetu haina budi kuangalia upya na kujipanga kwenye masuala haya .
 
Mkuu nadhani hii naweza kuuita moja kati ya thread zilizogusa ukweli unaouma. Hii ni tabia ambayo ni moja ya vikwazo vikubwa kabisa kwa maendeleo ya Tanzania. "sisi" ni wavivu, lakini sio wa kufikiri kama anavyosema Mkapa, lakini ni wavivu wa kazi. Nimeamua kusema sisi kwa makusudi na sio kusema wao na mimi kujiweka pembeni kwa sababu na mimi ni mmoja kati ya watanzania. Na baada ya kufanya kazi kidogo na watu wanaofanya kazi ndio nikaona ukweli huu.
Sisi kazini tuna-attend lakini hatufanyi kazi tunavyotakiwa, we hardly work instead of working hard. Na kibaya zaidi hata wanaofanya kazi kuna wengi tu wanashindwa kumanage mapato yao, wanajua kutummia ovyo, lakini hawezi kuhakikisha jasho lao la leo linawasaidia kesho. Huu ni ukweli tukemee sana mabaya yanayofanywa lakini tujirekebishe pia.

Si kweli kwamba watanzania ni wavivu.Ni jinsi muundo wa kazi na uchumi kijumla ulivyo nchini.Mbona watanzania wanaofanya kazi nchi za nje kwenye mashirika hata serikali za nje ni wachapa kazi barabara?
Matatizo makubwa ni mfumo wa uajiri, mtu aliyeajiriwa na sekta binafsi hataweza kuwa mvivu kama ilivyoandikwa, maana yuko monitored na uzalishaji wake unawiana moja kwa moja na kipato chake.
Ajira ya umma ndiyo yenye matatizo maana ajira hii haina monitoring kutoka ngazi za juu hadi chini.Mishahara haiko pinned to production na work output.
Hivyo mtu afanye kazi au asifanye mshahara wake uko pale pale.
Kuna wajanja kwenye ajira ya umma ambao wana ajira zaidi ya moja na kuokea mishahara zaidi ya mmoja!!
Hakuna uangalizi hakuna usimamizi katika ajira za umma.
Kwa upande mwingine analia wale waliojiajiri. Mtu aliyejiajiri haileti maana yoyote kuwa mvivu, unamtegea nani.Ukitega ni lazima biashara yako inakufa.
Kuna watanzania wanachapa kazi kweli kweli hasa katika sekta binafsi-just look around you.
 
Kwanza namshukuru sana mwanzilishi wa hii thread ,ni kitu cha msingi sana hiki na ndio msingi wa maendeleo yetu kama all condition ziko costant (No ufisadi)

Mimi kwa upande wangu naona hii imechangiwa sana na misiformation ambazo watu wanapata kuhusu inchi zilizoendelea,inaonekanga kuwa watu wanao ishi inchi zilizoendela wanakula kuku tu kama livyozoea kusemwa.Kwa msingi hii nadhani kuna haja ya wabongo ya kuona jinsi watu wanavyofanya kazi ktk mazingira yao ya kazi.Wataona jinsi gani watu walivyo serious na kazi pamoja na muda inagawa tayari infrastructure ziko stable na social service lakini bado watu wanafanya kazi kwa bidii na kwa njia hiyo ndio walivyofika hapo walipo.
Wache kuwaonyesha tamthilia zinazooshesha maisha baada ya kazi tu inaonekana kama watu hawafanyi kazi kwenye hizo tamthilia na maisha ndivyo yanatakiwa kuwa ,na wabongo kwa kuiga fashion na mambo kama hayo wako juu.
Sasa nadhani kama hatuna budi kujua kwa kweli hata kiwanja maendelea hayakuja kirahisi na kwetu sisi yataletwa na sisi wenyewe.

Tumekuwa tunasema kuwa ufisadi unachangia kutotia moyo watu kuwa na bidii hasa mtu ukijua unafanya kazi kwa bidii kisha kunawatu wanakuja chota kodi zenu na juhudi zako inakuwa kazi bure ,lakini hebu tu assume no ufisadi ,inabidi tuzoee kuchapa kazi na si rahisi ni ngumu hata kiwanja ndivyo watu wanavyo ishi .
 
Hili la kusema Watanzania wavivu mimi sikubaliani nalo hata siku moja. Uvivu wa Watanzania unasababishwa na kulipwa ujira mdogo sana ambao hauendani na gharama halisi za maisha. Unasababishwa na kuona viongozi mafisadi wakikupua kila kona na kuifisadi nchi na kujilimbikizia utajiri uliokithiri wakati asilimia kubwa ya Watanzania ikiendelea kuishi katika umaskini wa kutisha pamoja na kuwa tumejaliwa rasilimali chungu nzima.

Inakuwaje basi Watanzania hao hao waliozaliwa, kulelewa, kusoma (at least 1st degree) Tanzania hadi ukubwani na tayari wameshajenga tabia ya uviviuvivu wanapoenda nchi za magharibi utendaji wao wa kazi unasifiwa sana katika nchi mbali mbali zikiwemo US, UK, Canada n.k.

Ni kitu gani basi kinachowafanya Watanzania hawa wanapokuwa katika nchi za watu utendaji wao ni mfano wa kuigwa!? Si watoro kazini, hawachukui sick leaves kila kukicha, si walalamishi pia ni very reliable kiasi ambacho kinawafanya waajiri waombe kama unaweza kuwaleta Watanzania wengine (wenye qualifications zinazotakiwa) ili waje kuchapa mzigo mahali hapo.

Miaka michache iliyopita tulikuwa tunaongoza kwa kuzalisha korosho duniani, katani na tulikuwa katika tano bora katika pamba na kahawa na Wakulima waliokuwa wanalima mazao yale ni hawakuwa Wakenya, Waganda, Wamarekani bali walikuwa Watanzania. Walipoingia vyama vya ushirika na kuanza kuwatapeli na kuwakopa wakulima basi tukaporomoka vibaya sana. Hebu niambie mkulima gani aliyetapeliwa na kukopwa mazao yake atapata motisha wa kuzalisha zaidi msimu unaofuata!?

Wale wazungu pale TANESCO wa kutoka Net Group Problems walioletwa na fisadi Mkapa walikuwa wanalipwa kati ya $20,000 na $25,000 achilia mbali marupurupun pamoja na kuwa walikuwa hawajui chochote kile kuhusu umeme. Lakini kwa kuwa wana ngozi nyeupe basi Mkapa akaona wanastahili kulipwa mshahara mkubwa kisai hicho lakini ikija kwa Mtanzania mwenzetu basi lazima tumlalie!!!

Angalia pale Buzwagi na kwenye migodi yetu mingine bada ya kuja 'wawekezaji' wananchi walitegemea kupata ajira kupitia wawekezaji kulipwa fidia nzuri na hatimaye kuinua viwango vyao vya maisha. Lakini wapi!!! Wamelaliwa fidia zao na kulipwa kiduchu, ajira zinatolewa kwa wazungu wenzao hata wafagizi wanatoka nje ya nchi.

Tunasikia kila kukicha kwamba TRA inakusanya mapato makubwa kutokana na kodi lakini bado mishahara ya Watanzania ni midogo mno, hospitali zetu hazina madawa, vitanda na vifaa vya kileo, bado wanafunzi wanasoma katika shule ambazo hazina madawati, madarasa, walimu, vyoo n.k. umeme wetu bado ni wa shida kubwa, maji pia yanapatikana kwa alinacha. Tunategemea kweli mfanyakazi au mkulima kama huyu utendaji wake uwe mzuri pamoja na kutingwa na mawazo chungu nzima kuhusu maisha yake ya kila siku yeye na familia yake?

Tusijidhalilishe jamani na kujishusha hadhi, Watanzani si wavivu bali ni viongozi wetu ndiyo kwa kiasi kikubwa wanachangia uvivu wa Watanzania maana Watanzania wanaona keki ya Taifa inaliwa na wajanja wachache akina Mkapa, Rostam Aziz, Mramba, Chenge, Magufuli, Manji, Subhash, Jeetu Patel, Yona na wengineo na wageni kwa wizi wa migodi yetu, kuiba nyumba za serikali, kuingia mikataba ya rasilimali zetu ambayo haina maslahi kwa Watanzania n.k., wakati Watanzania walio wengi wanaishi maisha yaliyojaa ufukara wa kutisha. Aah aah hili sikubaliani nalo kabisa.
 
Sikubaliani na hii dhana ya kuwa watanzania ni wavivu, ninachofahamu ni kuwa watanzania hawako serious na kazi za umma. Ukimkuta kaajiriwa katika kampuni ya binafsi, au kama anafanya shughuli zake binafsi utagundua kuwa mtanzania ni mchapaji kazi mzuri sana. Hebu fuatlia watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi uone jinsi wanavyobeba maboksi bila kujali. Ukinikuta nikiwa kazini na maboksi yangu ninayobeba hapa huwezi kuamini kuwa ni mimi niliyekuwa mhandisi wa shirika moja la umma pale Tanzania nikiwa nafika kazini saa tatu na kwenda kupata supu saa nne na kurudi kiwandani saa tano, na kwenda lanchi saa sita na kurudi kazini tena saa saba na nusu na kufunga kazi saa nane na nusu badala ya saa 10 jioni.

Tatizo lililopo Tanzania ni mfumo mbovu wa uongozi na usimamizi tu. Kama viongozi wa kazi hawako serious ni dhahiri hata wafuasi pia hawatakuwa serious. Nadhani swali la kujiuliza ni kwa nini mfumo wetu wa usimamizi na uongozi uko vile katika taasisi zote za umma.

Nina mfano kuwa mwaka 1983-1984 nilikuwa nafanya kiwanda fulani. Nilianza kazi nikiwa chini ya waliokuwa wanaitwa ma-Tx. Baada ya muda, mkataba wao ukaisha wakarudi makwao na kukabidhi kiwanda kwa wabongo. Ingawa mafundi na watendaji kazi kule production line walibaki ni wale wale ila mameneja wote walibadilishwa; vile vile mishahara ya wafanyakzi wa production line na mafundi ilipunguzwa ili kuingizwa katika scheme iliyokuwa inajulikana kama SCOPO. Kilichotokea ni kuwa utendaji wa kazi kiwandani pale ulidorora sana na wizi wa bidhaa zinazozalishwa ukakua sana hadi kiwanda kikafa kabisa. Nakumbuka kuwa badala ya kufanya kazi watu walikuwa wanatumia muda mwingi sana kutongozana wakati wa kazi (kiwanda kilikuwa na wasichana wengi zaidi ya wanaume) na kusimuliana jinsi ya kuvusha "mizigo" kwenda kuuza mitaani. Na hivyo pia mameneja wetu nao walikuwa wakifanya mambo hayo hayo hivyo uzalishaji ukawa secondary.

Katika experience yangu hiyo, ninachoona ni kuwa mfumo wa uongozi na usimamizi ndio uliobadilika na kusababisha utendaji wa kazi nao kuharibika.
 
...yote ilianzia na jamii kuathiriwa na tamaa ya kujipatia pesa ya haraka haraka bila jasho.

kumbukumbu yangu, hali hii ilianza kipindi cha utawala wa Mwinyi, ambapo Gap baina ya watawala na wananchi ilizibwa na 'misheni town', ambao ili mambo yako yakae sawa, walikuwa Go-in-between the two, nao kufaidika na '10%'.

...Tofauti ya watanzania wa mwaka 1983 kurudi nyuma ilikuwa watafutaji angalau wapate hela ya kula na familia. Watanzania wa miaka ya 1984 na kuendelea mpaka 2008 longolongo miingi, pesa mbele bila jasho na kuendekeza starehe na anasa.

Kwa wale tuliosota enzi za foleni za kaya, mgao wa petroli na dizeli, foleni ya mikate ya siha, curfew ya kuzurura na gari baada ya jumapili saa nane, kipindi kireefu kukosa rights za kuangalia TV stations zaidi ya TVZ, kutosikiliza Radio Stations zaidi ya RTD na Sauti ya Tanzania Zbar nk, imepelekea Generation 'fulani' kuwa kama mahabusu waliofunguliwa na kuuona mwezi...

Bahati mbaya, Kikazi kipya nacho kinapotelea humo humo kwenye Bongo flava, miss urembo, miss maungo, miss kisura, nk... pesa ya haraka haraka!

nadhani, kweli Kuna haja ya kurudisha JKT, kila kijana wa aliye na umri kuanzia 16yrs apitie mafunzo ya lazima ya kujenga taifa si chini ya miezi tisa, naamini akili zitachangamka kidogo, la sivyo taifa linaangamia!
 
Back
Top Bottom