Watanzania Wengi ni Wavivu? The Moment of Truth!

kweli wa tz ni wavivu sana hasa kwenye usomaji wa vitabu hata magazeti hawasomi, siyo wavivu kwenye suala la uzazi tu
 
Habari zenu wanajf wote kwa ujumla wakiwemo mods,

naomba tupate mawazo kwenye hili suala.
leo asubuh nikiwa kwenye kisusafiri naelekea kazini nimesikia East africa radio wakiuliza '' watanzania ni wavivu katika utendaji wa kazi katika nyanja zote au?''compared to kenye and uganda
bahati mbaya sikuweza kusikiliza maoni ya wachangiaji.
nimeamua nililete apa jf tupate mawazo.

Nenda kwenye Facebook page yao utapata maoni yao. Hapa JF huwa tunajadili siasa kwa kwenda mbele tu.
 
mkuu ni kweli wtz 2mekuwa wavivu sana but sio wote wenye tabia kama hzo. Kuna watz wengine wdnajituma sana ktk kazi zao,wabunifu sana ukilinganisha na wa2 wa Malawi au msumbiji. Ni nchi ambazo nime wai tembelea na nika tathimini maendeleo ya mtu mmojamoja na wa2 jinsi walivyo jiari wenyewe bado wtz 2po juu zaidi yao. Cjajua bado kenya na uganda kuji2ma kwao kupoje.
 
Nenda kwenye Facebook page yao utapata maoni yao. Hapa JF huwa tunajadili siasa kwa kwenda mbele tu.

wakati mwingine uwe unajaribu kunyamaza kama hauna cha kuchangia.
ile radio ni ya mtanzania ndo anamiliki, so sioni sababu ya wewe kusema tupeleke facebook jambo kama hili. au wewe mwenzetu unasikiliza n akufuatilia leo nep katamka nini,nani kavuliwa gamba,wapi mnapanga mashambilizi ya green guard, nyumba gani mchome. some other times try to tune your mind in other matters.
 
wakati mwingine uwe unajaribu kunyamaza kama hauna cha kuchangia.
ile radio ni ya mtanzania ndo anamiliki, so sioni sababu ya wewe kusema tupeleke facebook jambo kama hili. au wewe mwenzetu unasikiliza n akufuatilia leo nep katamka nini,nani kavuliwa gamba,wapi mnapanga mashambilizi ya green guard, nyumba gani mchome. some other times try to tune your mind in other matters.

Nakujua wewe
 
CCM imetufanya tuwe wavivu wa kufikiri, yaani kuwa na mtindio wa kufikiri - karne ya sayansi ya techlologia - hakuna maji na umeme? unategemea mtanzania huyu awe na akili ya kufikiri?

Muda mwingi tunafikiri kujikimu na maisha yetu ya kila siku - Sukari imepanda, Maji dumu sh 500, Umeme hakuna, Unga bei hadi mia 900, Foleni barabarani, shilling inashuka thamani kila kukicha, ugali mama ntilie buku mbili unusu, hospitali madawa hakuna, shule za kayumba na zile za kata hoyvo hovyo - tunahaha huku na huko kuwatafuti watoto wetu shule nzuri - sasa unategemea akili ya kufikiri itatoka wapi kwa mtiririko huu wa matatizo yote haya?

50% ya watanzania wanakula mlo mmoja na navyojua mimi mtu anayeweza kufikiri ni yule aliyeshiba vizuri.
 
Watanzania siyo wavivu ila mazingira ya kazi ndiyo yanawafanya waonekane hivyo angalia watz wanaofanya kwenye private sector na ughaibuni wanafanya kazi sana na wanaperform vizuri
 
Habari zenu wanajf wote kwa ujumla wakiwemo mods,

naomba tupate mawazo kwenye hili suala.
leo asubuh nikiwa kwenye kisusafiri naelekea kazini nimesikia East africa radio wakiuliza '' watanzania ni wavivu katika utendaji wa kazi katika nyanja zote au?''compared to kenye and uganda
bahati mbaya sikuweza kusikiliza maoni ya wachangiaji.
nimeamua nililete apa jf tupate mawazo.

Ni kweli kabisa, nenda kwenye maofisi ya kuhudumiwa, kwanza watajifanya hawakuoni, labda wana browse internet, kucheza na simu, kupiga zogo, au kuzungukazunguka tu bila maana yoyote, wale wanaowahudumia wateja, wako slow mpaka utasema kweli waliomba kufanya hizo kazi au wamelazimishwa!
Barabarani watu wanatembea pole pole mno, wengine wamekaa tu kwenye vivuli wakiangalia magari na kusifia ufisadi, mpira na wizi!
Hakuna anaejituma, wanaamini wana muda wote duniani, kuabudu hela za bure, utapeli na ujanja ujanja tu wa maisha.
Wanaouza bodhaa hawajali wala kuumia kama stock imeisha, wanafurahia kabisa kukueleza kitu ukitakacho kimeisha, siajabu kimeisha kama wiki na zaidi, hakuna replenishing of stock wala nini!
Tuna matatizo wakuu!
 
Kila nchi ukienda viongozi wanadai kuwa wananchi wao wavivu. Ukweli unabakia kuwa hata huko Kenya, Uganda na nchi nyingine yoyote lazima ukienda utaona wageni wanafanyakazi kuliko Wazawa hata Ughaibuni. Hata Kenya ukienda utaona wakenya Wavivu lakini kwa Watanzania waishio huko Lazima wahangaike ili wapate mkate. hata hapa Tanzania wageni ili waishi maisha mazuri lazima wajitume ili waishi kwa kuwa hawana Ndugu. Hata watanzania waishio wanapiga mzigo hata wa kuosha vyombo ili mradi wapate pesa ya kulipia pango na kuishi
 
Sera za ujamaa zimetuathiri sana, tumetegemea zaidi kufanyiwa vitu na serikali, sasa tumeingia kwenye mfumo wa kibepari tukiwa na mawazo na kijamaa, so tunabaki kulalamika tu wageni wakichukua kazi zetu, wengi wetu sio aggresive na ntunaogopa kujaribu mambo mapya. Hii yote ni sababu ya mifumo mibovu na sera mbaya pamoja na elimu isiyoendana na wakati! Hii ni sifa mbaya sana kwetu maana hatuaminiki, mtu anaona bora aajiri mgeni kuliko mtanzania maana "watanzania ni wavivu"!
 
Hata mimi nilisikia discussion hii.Kwa bahati mbaya watanzania wengi waliotoa mawazo yao walikubaliana na motion iliyo kuwa inakuwa discussed kwamba watanzania ni wavivu.Ukweli ni kwamba watanzania sio wavivu ila serikali imewatelekeza wananchi wake kwa kutowapatia au kuwawekea miundombinu sahihi ya kuweza kujiendeleleza.Hata wale tunaowaita wajasiri wa kutafuta mali nao wanaibiwa mchana kweupe,malighafi bei juu,kwa hiyo faida wanayopata ni ni ndogo sana.Wakulima bei ya inputs ni kubwa mno,wakati mazao yao wanayauza kwa bei ndogo.Wafanyakazi nao wanaibiwa na serikali yao kwa kutozwa kodi kubwa na kulipwa mishahara midogo,watatokaje?Na mikakati hii imepangwa ili kutufukarisha.Naomba Watanzania tusikubali mawazo kwamba sisi ni wavivu,kwa sababu yanaingizwa kwa siri ili tukubali kwamba we are to blame for our situation.We are not lazy,ila mikakati imewekwa makusudi ili tubaki kuwa maskini tuwe rahisi kutawala.Kumbuka sio rahisi kumtawala mtu mwenye uwezo,but you can manipulate a poor person as you wish.
Habari zenu wanajf wote kwa ujumla wakiwemo mods,

naomba tupate mawazo kwenye hili suala.
leo asubuh nikiwa kwenye kisusafiri naelekea kazini nimesikia East africa radio wakiuliza '' watanzania ni wavivu katika utendaji wa kazi katika nyanja zote au?''compared to kenye and uganda
bahati mbaya sikuweza kusikiliza maoni ya wachangiaji.
nimeamua nililete apa jf tupate mawazo.
 
ukiondoa udhaifu wa serikali yetu ukweli unabakia palepale kuwa tamko la serikali ni la kweli!
Ni waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda (tena siku hiyo nakumbuka hakulia) aliseyesema kuwa 3/4 (robo tatu) ya waajiriwa wa serikali hawafanyi kazi maofisini bali ni porojo na majungu.
Tunachokiona kikizalishwa kwa maana hiyo kinazalishwa na 1/4 (robo) ya wafanya kazi.
Na sekta binafsi yaweza pia kuwa hivyo hivyo japo hali sio mbaya sana.
(usishangae na mimi nafanya kazi saa ngapi kama sasa hivi niko jf!!!)

Kwa maana hiyo sisi ni WAVIVU wa kazi na kufikiri ndio kabisaaa!!
 
Lakini imethibitishwa na mikataba yetu tunayosaini kila mara inayoonesha kuwa
anayetia saini huwa hasomi kilichoandikwa ndani. Rejea mikataba yote katika nchi hii...

Siyo mikataba tu, hata GN mheshimiwa raisi amesaini nyingi tu bila kusoma na baadae kujikuta alichokusudia sicho.

Mfano wa hivi karibuni ni uanzishwaji wa wilaya mpya ya butiama. Wakati akidhani makao makuu yake yatakuwa butiama kumbe watu wametupia nyamisisi pale kati na yeye kwa kutosoma akasaini bila kujua.
 
Back
Top Bottom