Watanzania wengi ni wanafiki sana

Masikio Masikio

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
1,840
3,378
Jana kulikua na maandamano ya chadema yalikuwa yanalenga kuaddress kero tofauti tofauti na ilikua ni hiyari na sio lazima.

Mimi binafsi sikuandamana sababu watanzania ni wanafki na kumpigania mtu mpumbavu kama Mtanzania ni kupoteza muda na nguvu ila ila kamwe siwezi wabeza waliondomana kwa namna yeyote ile.

Ila ajabu kuna watu wanawabeza chadema mara hawakua na watu wengi walikua wachache, bodaboda walikua wachache na maneno mengine ya kashfa.

Ila watu hao hao wanaobeza maandamano ya jana utawakuata kwenye nyuzi nyingine hapa hapa jamiiforums wanailalamikia serekali
  • Kukatika umeme ovyo
  • Bidhaa zinapanda bei hovyo,
  • mara huduma kwenye ofisi za serekali zimekua mbovu,
  • mara kuna upendeleo wa ajira kwenye baadhi ya taasisi za serikali.
  • Ubovu wa miundombinu
Ajabu ikitokea mtu anapaza sauti anambeza halafu muda huo huo analalamika ugumu wa maisha hii inaonyesha ni jinsi gani alivyokua mnafki na hii ndio tabia ya watanzania wengi.

Hata kwenye maisha ya kawaida unaweza ukawa unampigania sana mtu ila akienda upande wa pili anakuponda vibaya mno.

Ndio katika yale matatizo matatu ya Nyerere aliyoyasema ujinga, umaskini na maradhi inatakiwa liongezeke la nne unafki
 
Hao cadema miaka yote hayujaona wakitatuwa kero hayta moja kwenye majimbo yao.

Kero ya ndani ya chama ya kuwa chama cha kifalme haijatatuliwa.
Walishawai kushika serekali TRA mapato yote wanapelekea serekali ambayo iko chini ya ccm tokea 1961 uhuru

Unalaumuje mtu ambaye hajawahi shika serekali mpe serekali ndo umlaumu
 
Ingawa nakubaliana kuwa kuna chawa wengi sijui ndio hao wanafiki pia lakini kwa vile dunia inabadilika na watu pia hubadilika!

Kwa mfano kuna watu wengi walimuunga mkono Samia alipoingia madarakani na leo hii hawataki hata kimsikia baada ya kuuza Bandari kwa Dp World; je utawaita hao watu wanafiki kwa kubadili msimamo wao?
 
Jana kulikua na maandamano ya chadema yalikuwa yanalenga kuaddress kero tofauti tofauti na ilikua ni hiyari na sio lazima



Ndo katika yale matatizo matatu ya nyerere aliyoyasema ujinga, umaskini na maradhi inatakiwa liongezeke la nne unafki
kwahiyo wanafiki wengi walibaki nyuma ya keyboard humu JF kwamfano fulani na fulani....

yaan wanahanasisha watu halafu wao hawajitokezi bila sababu...
 
Pamoja na hayo..naamini asilimia 95% ya wapinzani sio good faith actors.case and point angalia hama hama zao...Wana shida zao kama Mimi na ww,at the end of the day they won't care about the collective if their individual needs are met.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom