Watanzania waogopeni hawa matapeli wa siasa

TAPELI HUYU HAPO NN

[emoji116] [emoji116] [emoji116]

Mgombea huyo wa urais wa CCM aliahidi kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi, kumaliza tatizo la wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo, kuhakikisha mama lishe hawabughudhiwi, kusimamia haki za wasanii, kulinda Muungano na usalama wa nchi.
Aliahidi kutoingilia utendaji kazi wa Bunge na Mahakama, kuheshimu mawazo ya vyama vingine vya siasa,

nini ambacho ajatimiza hapo. wakinamama sasa hivi hawasumbuliwi tena(mguse mama sokoni usikiea atakujibu nini), hakuna mwanafunzi anayelia mkopo, kazi za wasanii zinalindwa, amepambana na ufisadi mpaka mnaomba poo, mahaka tayari, other time will tell
 
Mjadala wa kitaifa!!??

Mjadala wa kuhusu taifa gani hilo ambalo wewe unaweza kuwa mtoa hoja/mzungumzaji?......Basi utakuwa mjadala wa taifa lile la " The Animal Farm!!"
Ujue kuna mda nawaza siku fisadi papa akaswekwa rumande hii ajira ya mtandaoni mtaipata kweli! Subirini mahakama yake ipo mbioni ajira yenu ndo mwisho!!
 
Jibu hoja IPTL kulipwa mil 400 za walipa kodi kila siku inakuingia akilini? Kuhusu mbowe hajawahi kuwa na Kinga yoyote, vyombo vya dola kibao mburuzeni mahakamani tatizo nini?

IPTL IMEANZISHWA NA RICHMOND YULE MZEE MLIYEMKUMBATIA ALIDHIINISHA TANESCO ILIPE 150,000,0000 KWA SIKU
 
Mkielezwa ukweli mnaleta propaganda nyingi! Changieni basi kwa hoja hamwezi siku zote zaidi ya matusi na kejeli

Wewe acha uki.laza hapa!

Kati ya mimi na wewe, nani analeta propaganda hapa?

Kama wewe fundi na unadhani unaelewa, leta ishu balanced zinazojadilika na siyo umbea wa kujadili watu hapa!!
 
Kwahyo ufisadi wa freeman ukianikwa ni umbeya? Ila ufisadi wa ccm ukianikwa ipate baraka zote!!
 
IPTL IMEANZISHWA NA RICHMOND YULE MZEE MLIYEMKUMBATIA ALIDHIINISHA TANESCO ILIPE 150,000,0000 KWA SIKU
Kwa sasa wanalipa kiasi gani kwa siku? Nani alikwambia IPTL imeanzishwa na RICHMOND? Pitia maandiko upate ufahamu halafu urudi tena hapa
 
Kuna watu mashuru wenye elimu zao ambao sizani kama wanalingana na wee kifikra kuna watu wana vyeo vyao wenye taaluma nzuri tuuh tunashare nao mawazo ya hapa na pale kuhusu taifa letu! Hivyo sitishwi na mfu wa fikra kama wewe
"sizani" ndio kitu gani huko shule ulienda kusomea ujinga?!
 
Kuna watu mashuru wenye elimu zao ambao sizani kama wanalingana na wee kifikra kuna watu wana vyeo vyao wenye taaluma nzuri tuuh tunashare nao mawazo ya hapa na pale kuhusu taifa letu! Hivyo sitishwi na mfu wa fikra kama wewe
Jiangalia tena
 
Ujue kuna mda nawaza siku fisadi papa akaswekwa rumande hii ajira ya mtandaoni mtaipata kweli! Subirini mahakama yake ipo mbioni ajira yenu ndo mwisho!!
Ww mahakama ya ccm hiyo mjipange kama sio wewe ni baba yako
 
nini ambacho ajatimiza hapo. wakinamama sasa hivi hawasumbuliwi tena(mguse mama sokoni usikiea atakujibu nini), hakuna mwanafunzi anayelia mkopo, kazi za wasanii zinalindwa, amepambana na ufisadi mpaka mnaomba poo, mahaka tayari, other time will tell
Uongooo labda huko kwenu
 
Ndugu wanajamvi,

Kwenye ukweli tunapaswa kuwa wakweli tuache itikadi zetu za kisiasa kwa kuwa naamini kuwa siasa siku zote inaishi ila watawala wanapita, kuna watu mienendo yao kisiasa inatia shaka kwa jinsi wanavofanya siasa zao.

Nimezisoma maandiko matakatifu na Qur'an na kunipa ujasiri,maarifa na hekima katika kuandaa hawa watu matapeli wanaowaadaa watanzania kwa nyakati tofauti, ebu tuangalie kila moja na utapeli wake;

1:TUNDU LISSU: Tukumbuke mnamo tarehe 15.sep.2007 CHADEMA kupitia katibu wao mkuu DK Slaa na lisu walitaja "A list of shame" pale mwembeyanga Tandika jijini Dar.Miongoni mwa mafisadi waliotajwa ni Edward Lowasa wakimuita fisadi papa.

Mwaka 2015 huyu huyu akijiunga na CHADEMA na kwa Bahati nzuri lisu akatamka kwenye viuga mbalimbali kuwa ile list yeye ndiye aliyeiandaa kuwa DK Slaa walishirikiana naye tuu kuisoma. Sasa hapo ndipo tunapatwa na ukakasi mkubwa na kuhoji hivi Tundu lisu atamwitaje lowasa shujaa wa mabadiliko lakini huyu ndiye waliyemuandama na tuhuma lukuki!

Akatembea naye kwenye mikoa tofauti tofauti kuelezea Lowasa alivo shujaa wa mabadiliko kweli kweli anasahau yote ya nyuma! Ata kama ni utumwa hii ni zaidi ya utumwa. Huyu huyu Tundu lisu alimwita Rais kikwete kuwa ni dhaifu na hapaswi kuliongoza Taifa lakini sasahivi amekuja mtu mkali anasema kuwa Rais kikwete ni bora na anafaa kuigwa! Hivi tutamueleweje Tundu lisu?

Kwangu Tundu lisu ni mtawala ambaye akishapata cheo huridhika na hataki mtu awe zaidi yake, Jimbo lake Singida mashariki hali ni mbaya kweli kweli Huduma za kijamii mbovu Sana lakini ata siku moja Tundu lisu hajawahi kwenda jimboni kuhamasisha au kuwawezesha vikundi mbalimbali vya akina mama na vijana.

Inasikitisha Sana mpaka mbunge mwenzake ELIBARIKI KINGU anatoka jimboni kwake kwa kuona hali mbaya iliopo kwenye jimbo la lisu na kwenda kuwawezesha vikundi vya akina mama. Lakini lisu amegeuka kuwa msemaji wa chama pale ufipa kazi ambayo ingestaili amwachie Tumaini makene, amegeuka kuwa mtengeneza propaganda za kupambana na MAGUFULI lakini hajui yule ni Rais siyo diwani au mbunge. Lisu badilika Siasa ni sayansi siyo propaganda na huo utapeli wako mwisho wako kisiasa inakuja usipobadilika.

2:FREEMAN MBOWE: Huyu mimi nawona ni mtu anayetumia siasa kufanikisha biashara zake, anawatumia akina lisu kufanikisha mambo yake.lakini hawa vijana hawashtuki, kama mnakumbuka mwalimu NYERERE aliwahi kusema ukiona chama kimevamiwa na wafanyabiashara ujue uhai wa chama ni ndogo. Wakati mwingine inabidi tufukue ata makaburi yaliyopita ili muone itusadie kwenye huu mjadala;

:KAULI HIZI 2014:

*ZITTO KABWE aanika ufisadi wa FREEMAN MBOWE - adai TUNDU LISU ni kifaranga hivyo amemtaka mama kifaranga atoke nje hadharani, pia amegusia kifo cha CHACHA WANGWE.

* Akizungumzia katika press conference ya CHADEMA na waandishi wa habari Leo, Mwanasheria mkuu Tundu lisu kuwa mkakati wa kuwafichua viongozi wasaliti ni wa siku nyingi ambapo chama kimenasa mawasiliano ya ZITTO KABWE tangu 2009 alipokuwa akiwasiliana na akina Denis Msack wa mwananchi.

* Lissu anasema njama hizo ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya ugaidi ambapo katika mahojiano yake na Star Tv akiwa na Mwigulu akukanusha, Pia aliandika kwenye Mtandao wa CHADEMA imtose Lwakatare. Lissu anaongezea kwa sasa ZITTO ana magari mawili (2) ya mkono pia alishiriki moja kwa moja kumzui mgombea ubunge jimbo la musoma vijinini ambapo yupo mkono.

:ZITTO AJIBU PIGO ( AMJIBU LISSU):

* Zitto; naamini pia mwaka 2005 mkono alimpa million 40 MBOWE ili asifanye kampeni musoma vijijini.

* Zitto; nadhani pia MBOWE alimwambia mwaka 2008 ( baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa ) mkono alimpa freeman Tsh. Milioni 40 za uchaguzi katika jimbo la Tarime ambapo kwenye chama akatoa mkopo.

* ZITTO: nadhani pia alimwambia mwaka 2010 Mkono alimpa MBOWE tsh milioni 200 pia MBOWE alimuambia lisu lissu kuwa Rostam alilipa milioni 100 Tshs. Kwa ajili za kampeni za DK slaa.

*ZITTO; hivi lisu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka conservative party?

* ZITTO; lissu amwambie aliyemtuma amwambie ukweli wote , Lissu ajue yeye ni kifaranga tuu, namtaka Mama kifaranga ajitokeze.

* ZITTO; namtaka ajitokeze aeleze aliingia deal gan na Sumaye kufuatia deni lake 2005. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya umma ilipo Club Bilcanas.

Kwahyo watanzania wezangu mnaona kabisa juu ya ubadhirifu wa freeman MBOWE, hajawahi kujibu hizo tuhuma ambazo zito alizielezea tofauti za propaganda za hapa na pale. Huyu ndiye mtetezi wa wanyonge na anasema ana uchungu na nchi hii tunamkosea ata mungu kutamka haya!

Huyu ndiye ana tuhuma juu ya matumizi mabaya ya ruzuku lakini tunapewa majibu mepesi kwenye masuala magumu! Huyu ndiye aliongoza mikakati ya kumuingiza chamani mtu waliyemuita fisadi papa na huyu ndiye aliyeongoza kumuingiza huyo huyo waliyemuita kasisi wa mafisadi kwenye kamati kuu ya taifa kwa njia za kutatanisha.

3: SAED KUBENEA: huyu alitumia mda mwingi kumchafua Edward Lowasa na vyombo vyake lakini ilipofika mda wa uchaguzi 2015 yeye na vyombo vyake alimsafisha na kuwa mweupe kiasi kwamba hajawa na tuhuma yoyote. Vyombo vyake vikawa vinaripoti mafuriko ya lowasa tuuh ufisadi akaupa kisogo.

Ni huyu aliyemwagiwa Tindikali mpaka ikahatarisha maisha uhai wa maisha yake, yaani KUBENEA ni bonge la ndumelakiwili sijawahi k uona Tanzania, umwagiwe Tindikali kwa kuripoti ufisadi wa mtu halafu mwisho wa siku unamshika mkono kuwa ni msafi ndiye shujaa wa mabadiliko hakika mlitaka kuuza Tanzania kwa bei rahisi sanaa.

Hii hapa gazeti la mwanahalisi ambaye mkurugenzi wake ni Said kubenea.lakini sasa ndio bosi wao wamemkumbatia na ndiye shujaa wa mabadiliko! Mungu saidia hii Tanzania nchi yangu.

Mimi kama mtanzania mzalendo ni haki yangu kikatiba kuwasema hadharani wale ambao wanataka kupotosha umma. Niwape salamu watu wa Singida mashariki kuwa 2020 nitakuwa na nyie begabega kumuondoa huyu tapeli lisu nitatembea kijiji hadi kijiji kuwaelezea utapeli wa Huyu jamaa.

Mimi si mkazi wa pale ila nimepatwa na uchungu wanaopata wale watu, nitashirikiana na mgombea yoyote atakayeweka nia tofauti na CHADEMA kuhakikisha huyu tapeli anaondoka arudi ufipa akaenezee propaganda zake kwa kuwa ndiyo kipaji chake.

Tumempata Rais muadilifu na mchapakazi ambaye nchi zingine zinamlilia lakini hawa matapeli wanataka kutuvuruga kichwa yafaa tuwapuuze kabisaa.

Safari ya kuelekea uchumi wa kati bado inaendelea;

Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli Tanzania.

SIMON MATO.
0762189733
Haya umemaliza kazi unayo haki ya kulipwa nenda kachukue buku 7 zako kwa kwa mkuu wako wa kitengo, Olesendeka, uende nyumbani.
 
Tapeli ni mmoja tu serikali ya CCM iliyoingia madarakani miongo kadhaa na haijawahi kuwafikisha wananji popote zaidi ya kuwa pango na kichaka cha wezi na ahadi feki.

Na hayo yote uliyoandika hapo juu japo sijayasoma zaid ya kichwa cha habari!

Ni Matunda ya CCM kwahiyo wacha kutubabaisha na propaganda za mitandaoni fanya kazi.
Hata mimi sijasoma nilihisi kichechefu vile
 
Ujue kuna mda nawaza siku fisadi papa akaswekwa rumande hii ajira ya mtandaoni mtaipata kweli! Subirini mahakama yake ipo mbioni ajira yenu ndo mwisho!!

Kimtokacho mtu, ndicho hasa kiujazacho moyo wake na ndivyo hasa alivyo yeye!!

Wewe kama ndiye uliyeajiriwa kufyatua upuuzi na ujinga mitandaoni, ni vyema na ni haki yako, maana labda pengine ndiyo uhuru wenyewe wa kusema chochote huo.

Wengine mzee tuko very self independent hatushikiwi akili na mtu awaye yeyote kama fikra zako zinavyokutuma

Ukileta hoja zilizosimama utapata tu support yangu, nitakuunga mkono. Na ukileta hoja yenye upogo, the same way, tutakuchapa vilivyo na kukupinga kwa nguvu zote!!
 
Ujue kuna mda nawaza siku fisadi papa akaswekwa rumande hii ajira ya mtandaoni mtaipata kweli! Subirini mahakama yake ipo mbioni ajira yenu ndo mwisho!!

Swali la kizushi..

Hivi huyu SALVA RWEYEMAMU alikuwa Mchochezi au Msema kweli ni mpenzi wa Mungu?
.........................…........................................................
Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

::Huyu Ndiye Pombe Magufuli::

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
 
Kwahyo ufisadi wa freeman ukianikwa ni umbeya? Ila ufisadi wa ccm ukianikwa ipate baraka zote!!

Ufisadi wa Mbowe nendeni mkaujadili huko ofisi ndogo za CCM mtaa wa Lumumba mpange namna ya kumpiga kisiasa kwa sbb kiaheria wala hakuna kitu hapo!!

Wewe unashindwa kujenga hoja za kujadili shina la RUSHWA na UFISADI ambalo limelelewa na kumwagiliwa maji na SERA za CCM for 55+ years tangu uhuru unatuletea upupu huu wa mtu aliye nje kabisa ya system eti Mbowe, Lissu na wengine kina nani sijui....

Unajua ni kwa nini wengine tunakuona wewe ni taka taka kabisa?

Ni kwa sbb, you think the most JF members are ignorant and stupidy as you are!!

I am sorry to say this, but, you deserve to be told the truth!!
 
Swali la kizushi..

Hivi huyu SALVA RWEYEMAMU alikuwa Mchochezi au Msema kweli ni mpenzi wa Mungu?

Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

::Huyu Ndiye Pombe Magufuli::

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
[emoji13] [emoji13] [emoji13] ucho......

[emoji111]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom