Well said,
Ungeonekana wa maana sana kama ungeongelea pia kuhusu skendo na uovu unafanywa ndani ya chama chako na siyo tu kuponda kuhusu Lissu, Freeman na wengineo.
Ifike muda tuwe tunaweka mbali maslahi ya uchama katika mambo ya msingi ambayo yataleta faida katika taifa letu.
Pia siku nyingine usisahau kuongelea mabaya na faida ya viongozi, skendo zinazowakumba hao viongozi wa CCM.
Hakika siku ambayo utakuwa neutral kuongelea mabaya ya huku na kule watu wengi sana watakuelewa Mkuu.
Ingawa vijana wa cdm wakisema wakosoe na kuanika yanayofanywa na wale watu....hakika hawachelewi kuitwa wachochezi. Na ukiangalia mwanzoni umesema kwa mujibu wa katiba una haki ya kuwasema watu dhidi ya ufisadi wanaofanya.
Je katiba inawalinda nyie tu na siyo vijana wa upande wa upinzani? Mpaka hapo nahisi utakuwa ushapata hoja yangu wewe mleta hili bandiko.
Kitu kingine ni kwamba tuliambiwa kuwa mahakama za mafisadi zimeanzishwa lakini mpaka sasa hivi kuna watu wapo ambao wana skendo nyingi za ufisadi. Je wamefungiliwa mashitaka?
Wale watu waliosemwa kuhujumu uchumi kwa kuficha sukari wako wapi? Walifunguliwa mashitaka? Au ilikuwa ni danganya toto?
Vipi kuhusu sakata la billion 320 atazilipa nani? Ni wale waliofanya ufisadi na wakaja na maneno yao ya dharau kuwa ni hela ya mboga?