Watanzania waogopeni hawa matapeli wa siasa

Watanzania waogopeni hawa matapeli wa siasa

Ufisadi wa Mbowe nendeni mkaujadili huko ofisi ndogo za CCM mtaa wa Lumumba mpange namna ya kumpiga kisiasa kwa sbb kiaheria wala hakuna kitu hapo!!

Wewe unashindwa kujenga hoja za kujadili shina la RUSHWA na UFISADI ambalo limelelewa na kumwagiliwa maji na SERA za CCM for 55+ years tangu uhuru unatuletea upupu huu wa mtu aliye nje kabisa ya system eti Mbowe, Lissu na wengine kina nani sijui....

Unajua ni kwa nini wengine tunakuona wewe ni taka taka kabisa?

Ni kwa sbb, you think the most JF members are ignorant and stupidy as you are!!

I am sorry to say this, but, you deserve to be told the truth!!
Upo kiitikadi mno na siasa zako zimejaa hisia, ufisadi wa freeman umeelezwa na ulisemwa kitambo lakini hajawahi kukana katakata! Hivi nikikuuliza hela ambazo Lowasa alilipa kipindi anaingia CHADEMA na ikasemekana mhe. Kazikomba na kuamisha nje ya nchi utasemaje?
 
Ndugu wanajamvi,

Kwenye ukweli tunapaswa kuwa wakweli tuache itikadi zetu za kisiasa kwa kuwa naamini kuwa siasa siku zote inaishi ila watawala wanapita, kuna watu mienendo yao kisiasa inatia shaka kwa jinsi wanavofanya siasa zao.

Nimezisoma maandiko matakatifu na Qur'an na kunipa ujasiri,maarifa na hekima katika kuandaa hawa watu matapeli wanaowaadaa watanzania kwa nyakati tofauti, ebu tuangalie kila moja na utapeli wake;

1:TUNDU LISSU: Tukumbuke mnamo tarehe 15.sep.2007 CHADEMA kupitia katibu wao mkuu DK Slaa na lisu walitaja "A list of shame" pale mwembeyanga Tandika jijini Dar.Miongoni mwa mafisadi waliotajwa ni Edward Lowasa wakimuita fisadi papa.

Mwaka 2015 huyu huyu akijiunga na CHADEMA na kwa Bahati nzuri lisu akatamka kwenye viuga mbalimbali kuwa ile list yeye ndiye aliyeiandaa kuwa DK Slaa walishirikiana naye tuu kuisoma. Sasa hapo ndipo tunapatwa na ukakasi mkubwa na kuhoji hivi Tundu lisu atamwitaje lowasa shujaa wa mabadiliko lakini huyu ndiye waliyemuandama na tuhuma lukuki!

Akatembea naye kwenye mikoa tofauti tofauti kuelezea Lowasa alivo shujaa wa mabadiliko kweli kweli anasahau yote ya nyuma! Ata kama ni utumwa hii ni zaidi ya utumwa. Huyu huyu Tundu lisu alimwita Rais kikwete kuwa ni dhaifu na hapaswi kuliongoza Taifa lakini sasahivi amekuja mtu mkali anasema kuwa Rais kikwete ni bora na anafaa kuigwa! Hivi tutamueleweje Tundu lisu?

Kwangu Tundu lisu ni mtawala ambaye akishapata cheo huridhika na hataki mtu awe zaidi yake, Jimbo lake Singida mashariki hali ni mbaya kweli kweli Huduma za kijamii mbovu Sana lakini ata siku moja Tundu lisu hajawahi kwenda jimboni kuhamasisha au kuwawezesha vikundi mbalimbali vya akina mama na vijana.

Inasikitisha Sana mpaka mbunge mwenzake ELIBARIKI KINGU anatoka jimboni kwake kwa kuona hali mbaya iliopo kwenye jimbo la lisu na kwenda kuwawezesha vikundi vya akina mama. Lakini lisu amegeuka kuwa msemaji wa chama pale ufipa kazi ambayo ingestaili amwachie Tumaini makene, amegeuka kuwa mtengeneza propaganda za kupambana na MAGUFULI lakini hajui yule ni Rais siyo diwani au mbunge. Lisu badilika Siasa ni sayansi siyo propaganda na huo utapeli wako mwisho wako kisiasa inakuja usipobadilika.


2:FREEMAN MBOWE: Huyu mimi nawona ni mtu anayetumia siasa kufanikisha biashara zake, anawatumia akina lisu kufanikisha mambo yake.lakini hawa vijana hawashtuki, kama mnakumbuka mwalimu NYERERE aliwahi kusema ukiona chama kimevamiwa na wafanyabiashara ujue uhai wa chama ni ndogo. Wakati mwingine inabidi tufukue ata makaburi yaliyopita ili muone itusadie kwenye huu mjadala;

:KAULI HIZI 2014:

*ZITTO KABWE aanika ufisadi wa FREEMAN MBOWE - adai TUNDU LISU ni kifaranga hivyo amemtaka mama kifaranga atoke nje hadharani, pia amegusia kifo cha CHACHA WANGWE.

* Akizungumzia katika press conference ya CHADEMA na waandishi wa habari Leo, Mwanasheria mkuu Tundu lisu kuwa mkakati wa kuwafichua viongozi wasaliti ni wa siku nyingi ambapo chama kimenasa mawasiliano ya ZITTO KABWE tangu 2009 alipokuwa akiwasiliana na akina Denis Msack wa mwananchi.

* Lissu anasema njama hizo ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya ugaidi ambapo katika mahojiano yake na Star Tv akiwa na Mwigulu akukanusha, Pia aliandika kwenye Mtandao wa CHADEMA imtose Lwakatare. Lissu anaongezea kwa sasa ZITTO ana magari mawili (2) ya mkono pia alishiriki moja kwa moja kumzui mgombea ubunge jimbo la musoma vijinini ambapo yupo mkono.

:ZITTO AJIBU PIGO ( AMJIBU LISSU):

* Zitto; naamini pia mwaka 2005 mkono alimpa million 40 MBOWE ili asifanye kampeni musoma vijijini.

* Zitto; nadhani pia MBOWE alimwambia mwaka 2008 ( baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa ) mkono alimpa freeman Tsh. Milioni 40 za uchaguzi katika jimbo la Tarime ambapo kwenye chama akatoa mkopo.

* ZITTO: nadhani pia alimwambia mwaka 2010 Mkono alimpa MBOWE tsh milioni 200 pia MBOWE alimuambia lisu lissu kuwa Rostam alilipa milioni 100 Tshs. Kwa ajili za kampeni za DK slaa.

*ZITTO; hivi lisu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka conservative party?

* ZITTO; lissu amwambie aliyemtuma amwambie ukweli wote , Lissu ajue yeye ni kifaranga tuu, namtaka Mama kifaranga ajitokeze.

* ZITTO; namtaka ajitokeze aeleze aliingia deal gan na Sumaye kufuatia deni lake 2005. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya umma ilipo Club Bilcanas.

Kwahyo watanzania wezangu mnaona kabisa juu ya ubadhirifu wa freeman MBOWE, hajawahi kujibu hizo tuhuma ambazo zito alizielezea tofauti za propaganda za hapa na pale. Huyu ndiye mtetezi wa wanyonge na anasema ana uchungu na nchi hii tunamkosea ata mungu kutamka haya!

Huyu ndiye ana tuhuma juu ya matumizi mabaya ya ruzuku lakini tunapewa majibu mepesi kwenye masuala magumu! Huyu ndiye aliongoza mikakati ya kumuingiza chamani mtu waliyemuita fisadi papa na huyu ndiye aliyeongoza kumuingiza huyo huyo waliyemuita kasisi wa mafisadi kwenye kamati kuu ya taifa kwa njia za kutatanisha.

3: SAED KUBENEA: huyu alitumia mda mwingi kumchafua Edward Lowasa na vyombo vyake lakini ilipofika mda wa uchaguzi 2015 yeye na vyombo vyake alimsafisha na kuwa mweupe kiasi kwamba hajawa na tuhuma yoyote. Vyombo vyake vikawa vinaripoti mafuriko ya lowasa tuuh ufisadi akaupa kisogo.

Ni huyu aliyemwagiwa Tindikali mpaka ikahatarisha maisha uhai wa maisha yake, yaani KUBENEA ni bonge la ndumelakiwili sijawahi k uona Tanzania, umwagiwe Tindikali kwa kuripoti ufisadi wa mtu halafu mwisho wa siku unamshika mkono kuwa ni msafi ndiye shujaa wa mabadiliko hakika mlitaka kuuza Tanzania kwa bei rahisi sanaa.

Hii hapa gazeti la mwanahalisi ambaye mkurugenzi wake ni Said kubenea.lakini sasa ndio bosi wao wamemkumbatia na ndiye shujaa wa mabadiliko! Mungu saidia hii Tanzania nchi yangu.

Mimi kama mtanzania mzalendo ni haki yangu kikatiba kuwasema hadharani wale ambao wanataka kupotosha umma. Niwape salamu watu wa Singida mashariki kuwa 2020 nitakuwa na nyie begabega kumuondoa huyu tapeli lisu nitatembea kijiji hadi kijiji kuwaelezea utapeli wa Huyu jamaa.

Mimi si mkazi wa pale ila nimepatwa na uchungu wanaopata wale watu, nitashirikiana na mgombea yoyote atakayeweka nia tofauti na CHADEMA kuhakikisha huyu tapeli anaondoka arudi ufipa akaenezee propaganda zake kwa kuwa ndiyo kipaji chake.

Tumempata Rais muadilifu na mchapakazi ambaye nchi zingine zinamlilia lakini hawa matapeli wanataka kutuvuruga kichwa yafaa tuwapuuze kabisaa.

Safari ya kuelekea uchumi wa kati bado inaendelea;

Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli Tanzania.

SIMON MATO.
0762189733

Tushachelewa wamejaa katika serikali yetu hao matapeli
 
Upo kiitikadi mno na siasa zako zimejaa hisia, ufisadi wa freeman umeelezwa na ulisemwa kitambo lakini hajawahi kukana katakata! Hivi nikikuuliza hela ambazo Lowasa alilipa kipindi anaingia CHADEMA na ikasemekana mhe. Kazikomba na kuamisha nje ya nchi utasemaje?

Sema sasa ili ujue nitasemaje!

Mbona unataka kuleta ubishi wa watoto wa chandimu hapa?

Unaniuliza "nikisema utasemaje" wakati hata hujasema!!

Wewe sema tu halafu uone na mimi nitasemaje.

ONYO: Usilete umbeya, unatuhumu basi hakikisha unaweka na ushahidi wa nyaraka za uthibitisho wa tuhuma zako hapo. Unless huna, funga ndomo lako!!
 
Mkuu uliowaandikia waraka mbona wameshaandika barua ya kujiuzulu na wamemkabidhi mwenyekiti wenu!!!!
 
Sema sasa ili ujue nitasemaje!

Mbona unataka kuleta ubishi wa watoto wa chandimu hapa?

Unaniuliza "nikisema utasemaje" wakati hata hujasema!!

Wewe sema tu halafu uone na mimi nitasemaje.

ONYO: Usilete umbeya, unatuhumu basi hakikisha unaweka na ushahidi wa nyaraka za uthibitisho wa tuhuma zako hapo. Unless huna, funga ndomo lako!!
Ingekua ni umbea basi angekana kipindi kile ZITO ameyaongea ila kwa kuwa anajua ni ukweli ndo maana kaa kimya mpaka Leo nakushangaa wewe unakuwa kuwadi wa matapeli!
 
Mimi sina mda na huyo lowasa wako, wewe na wapumbavu wenzako, kapeleke kijiwenu huo upumbavu kwa wapumbavu wenzio
Usimchokozi nyuki kwenye wakati huna dalili za kupata moto wa kumzuia! Acha kuweka hisia kaka kwenye mijadala utaumia sanaa
 
Mbona sijawaona wabunge wa ccm?
Kwa sbb nyie ni malaika hamkosei. Mnatutesa sana tangu uhuru tunahangaika na madawati. Ajira mesitisha, kiufup maisha yamekuwa magumu sana.
Hao watu ninawakubali sana mpaka kesho kutwa. Viva CHADEMA



sishangai kwa sababu hata shetwani unamkubari
 
Tapeli ni mmoja tu serikali ya CCM iliyoingia madarakani miongo kadhaa na haijawahi kuwafikisha wananji popote zaidi ya kuwa pango na kichaka cha wezi na ahadi feki.

Na hayo yote uliyoandika hapo juu japo sijayasoma zaid ya kichwa cha habari!

Ni Matunda ya CCM kwahiyo wacha kutubabaisha na propaganda za mitandaoni fanya kazi.



yani wewe mbulula sijui!!! kumbe hujasoma habari halafu unakoment?? wewe ni GT kweli??? halafu eti mnatala mpewe nchi!!! common!!!
 
Usimwamini mwanasiasa hata siku moja hata akiwa baba ako maana siku zote yeye huweka maslahi mbele maslahi yake binafsi mfano mzuri ni Lisu,Mbowe na wabunge kibao wa Ccm wote wale wale
 
Wana wewwseka kusikia kipenzi cha watanzania yuko bukoba kwa wahanga wa tetemeko. Iptl mzee kalipeni hela mnadaiwa
 
Mnajua maana ya kirefu cha jina la simon mato?yaani simon matope.Uzi umekaa kimatope matope
 
Upo kiitikadi mno na siasa zako zimejaa hisia, ufisadi wa freeman umeelezwa na ulisemwa kitambo lakini hajawahi kukana katakata! Hivi nikikuuliza hela ambazo Lowasa alilipa kipindi anaingia CHADEMA na ikasemekana mhe. Kazikomba na kuamisha nje ya nchi utasemaje?
Tukumbushane tu, sisiem walitoa sh ? Kwa dr mihogo na prof.
 
Unahitaji kuwa mwendawazimu kuendelea kuwaunga mkono Chadema baada ya sarakasi zile za 2015. In short CCM ina miaka mingi ya kutawala na wanajua namna ya kuwa handle wapinzani hasa kipindi hiki ambacho huko upinzani wamejaa mamluki ambao wamefanikiwa kudhibiti kasi ya wazalendo wa kweli. Nawashauri vijana ambao bado wana matumaini na hawa wanasiasa wajali maisha yao hadi tutapopata watu serious na si wapiga deal ndio msimame kuing'oa CCM madarakani lakini si kupitia akina Mbowe na Lissu.
 
Unahitaji kuwa mwendawazimu kuendelea kuwaunga mkono Chadema baada ya sarakasi zile za 2015. In short CCM ina miaka mingi ya kutawala na wanajua namna ya kuwa handle wapinzani hasa kipindi hiki ambacho huko upinzani wamejaa mamluki ambao wamefanikiwa kudhibiti kasi ya wazalendo wa kweli. Nawashauri vijana ambao bado wana matumaini na hawa wanasiasa wajali maisha yao hadi tutapopata watu serious na si wapiga deal.
Hongera sanaa mkuu! Tupo bega kwa bega kuwapinga hawa matapeli wa siasa
 
Back
Top Bottom