MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 705
Waungwana,
Nimekuwa nikiwaza jambo moja.
Ni kwa sababu gani sisi - Watanzania, wazawa - tumeamua kwamba soko la simu za mkononi liwe kwenye miliki ya wageni au baadhi ya wazawa wakishirikiana na wageni. Sipati jibu kwa nini imekuwa hivyo.
Hata hivyo, sijakata tamaa, kwani najua kwamba simple arithmetics zinatuwezesha kuwa na kampuni ya simu za mkononi ambayo umiliki wake ni wa Watanzania wazawa kwa 100%.
Ukianzia, kwa mfano, hapa JF. Kuna wanachama milioni kadhaa. Sema tuanzishe kampuni ambayo itakuwa na wanahisa 1,000,000/- ambao watanunua hisa kwenye DSE.
Tuseme kwamba thamani ya hisa moja itakuwa ni Tshs 10,000/-.
Ukifanya hesabu za haraka haraka, Tshs 10,000/- times 1,000,000 shareholders unapata Tshs. 10,000,000,000.
Amount hii ni ndogo sana kwa kuanzia, au inatosha?
Nawaombeni maoni yenu.
Haiwezekani kupata Watanzania milioni moja, walioko ndani na nje ya nchi, wakawekeza Shs. 10,000/- kila mmoja, katika kununua hisa kwenye kampuni hii, ili tuwe na uwezo wa kushindana kikamilifu? Hakika tutawateka wateja wote, kwani hii itakuwa kampuni ya wazawa, SIO ya makaburu na wageni wengine wachumia-tumbo! Wakishatosheka wanaingia mitini, kwani Tanzania imegeuzwa kuwa Shamba la Bibi!
-> Mwana wa Haki