Mkuu hii topic yako tuiweke kwenye kundi gani naona kama NYEPESI vile.wakuu hili jambo nimelifatilia kwa muda mrefu sasa
wengi wetu hapa jf tunapenda sana zile topic nyepesi hasa za mapenzi,utani na jokes,dini na nyingine kama hizo
ikitokea topic ya kuumiza kuchwa kufikiri wachache sana wanajitokeza
hii inanifanya niukubali usemi wa rais mstaafu mkapa kwamba watanzania ni wavivu wa kufikiri
kwa ujumla "watanzania tunapenda starehe"
hatupendi kuumiza kichwa na hata kufanya kazi tunafanya kwa kutimiza wajibu, asilimia kubwa ni uvivu ndio umetawala katika kufanya kila kitu
watanzania walio wengi wanapenda kufanya kazi kidogo ila kupata faida kubwa na muda mwingi wa kustarehe
ndio maana mkuu unaona topics nyingi zinazoshambuliwa kwa wingi ni za mambo ya mapenzi, porojo za siasa, udaku, utani nk
hili lina athiri sana thamani ya JF coz hata jukwaa ambalo limetengwa kujadili mambo ya technology au afya unakuta watu wanaamua kuchangia mada husika katika hali ambayo wao itawafurahisha bila kujali umuhimu wa mada yenyewe.
Siyo lazima kila hoja iwe ya kisiasa. Kuna forum nyingi hapa JF kama za uchumi, teknolojia, elimu, n.k. Lakini siyo popular. Mimi ningetegemea kwenye teknolijia, kwa mfano, watu wawe wanapashana taarifa kuhusu concepts/ideas walizoziona au wanazofikiria ambazo zinaweza kutekelezwa katika mazingira yetu na kusaidia vijana kumpambana na ukosefu wa ajira na umasikini kwa ujumla. Badala yake watu wanapeana mbinu za kuchakachua gadgets, sofware, n.k. Kama wewe unao ujuzi kama huo kwa nini usiutumie in a positive way and make money in the process.Mkuu...unaweza kuwa sahihi..ila tambua kuwa kumekuwa na uchangiaji wa kishabiki zaidi kwenye mada nzito...unakuta hoja ipo ya msingi ila mtu ataipinga tu kwa kuwa haiendani na itikadi yake...
Utaona kuwa ukitaka Thread yako watu waipende andika pumba zozote kuiponda CCM...utaona likes kibao badala ya kujadili kwa kujenga.
Siyo lazima kila hoja iwe ya kisiasa. Kuna forum nyingi hapa JF kama za uchumi, teknolojia, elimu, n.k. Lakini siyo popular. Mimi ningetegemea kwenye teknolijia, kwa mfano, watu wawe wanapashana taarifa kuhusu concepts/ideas walizoziona au wanazofikiria ambazo zinaweza kutekelezwa katika mazingira yetu na kusaidia vijana kumpambana na ukosefu wa ajira na umasikini kwa ujumla. Badala yake watu wanapeana mbinu za kuchakachua gadgets, sofware, n.k. Kama wewe unao ujuzi kama huo kwa nini usiutumie in a positive way and make money in the process.
Mkuu utakubaliana na mimi kuwa sisi watanzania ni watu wepesi sana?je ndio maana tunashindwa kushindana na wakenya?